Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
MkuuMkuu Wewe endelea kufaidi dunia huko uliko. Waachie kilio wenye msiba wao. Usiwakatishe tamaa zaidi.
Hii nchi ilishakuwa ya hatari tangu awali. Nyerere aliposema kwa katiba hii anaweza kuja dikteta mbaya sana, Watanzania walipuuza wakijua “ulaji mezani kwako” waliouzoea utaendelea kama kawa hivyo hakuna haja ya kuhangaika na masiasa.
Tena miaka ile ukiuliza habari za mshahara au pensheni unaonekana kama kibwengo fulani hivi; umefulia kweli kweli. Kazi ya maana ilikuwa ni ile yenye “ulaji” mkubwa. Mishahara karibia yote ilikuwa peanuts. Wafanyakazi hasa serikalini wamshukuru sana JK (awamu ya 4) kwa kuhuisha mishahara na pensheni za sekta ya umma mpaka kufikia kuwa kigezo cha kuvutia ajira hizo. Kiasi cha watumishi wengi kusahau habari za rushwa na fojari za risiti. Watu wakaanza kujadili mishahara na pensheni serikalini!
Leo hii watu wanamdai Magufuli ajira, vyeo, nyongeza za mshahara kwa vile Kikwete aliongeza thamani kubwa katika vipato hivyo vya watumishi wa umma kwa namna ambayo haikufikirika huko nyuma. Waliotumikia awamu za 1 hadi 3 wanajua. JK aliposema “mtanikumbuka” alipokuwa akiaga tukacheka sana nadhani alijua kuhusu “yajayo”. Eti “nawaletea chuma hiki; kinatema cheche!” [emoji23] Bila shaka aliiangalia ile “wage bill” ya sekta ya umma ilivyokuwa na ukubwa wa kutisha akajua chuma kikishakamata hatamu hatua namba moja kitawahi Hazina na kufyekelea mbali maslahi kibao.
Safari ya kurejea awamu za 3 > 1 ndio ilishaanza tena huku sekta za umma na binafsi zikizidi kusinyaa. Haitakaa itokee mishahara iongezwe serikalini Labda selectively kwa “wateule” na “watu maalum”. Kwenye siasa nako ni sauti moja tu ndiyo inayosikika sasa ikihanikizwa na miangwi ya kila aina na shadidi za mapambio ya kusifu na kuabudu. Hakika kama Watanzania wataendelea kukwepa wajibu wao wa kisiasa, basi ni mi-kumi zaidi ya kilio na kusaga meno. Hakuna namna. [emoji22]
Habari ya mishaahara kuwa midogo na watu kutegemea rushwa serikalini inanikumbusha story moja ya enzi za "Fagio la Chuma" la Mzee Ruksa.
Mzee Ruksa, Rais Ali Hassan Mwinyi, mwenyewe alihadithia habari hii katika hotuba kuonesha ukubwa wa tatizo la rushwa.
Alisema kwamba, alikuwa na ndugu yake mmoja anafanya kazi serikalini. Sasa yule ndigu yake, akawa na tuhuma fulani kazini. Akasimamishwa kazi ili ufanyike uchunguzi. Wakati kasimamishwa kazi, analipwa mshahra wote kama kawaida.
Sasa huyo jamaa aliyesimamishwa kazi, akamfuata Mzee Ruksa. Akamwambia Mzee, nakulililia sana. Tafadhali nirudishe kazini, hali ni mbaya nina familia na watoto.
Sasa Mzee Rushwa akamuuliza huyo ndugu yake, wewe umesimamishwa kazi unalipwa mshahara au mshahara hawakulipi?
Ndugu yake akamjibu mshahara analipwa kama kawaida.
Mzee Ruksa akashangaa sana. Akamuuliza tena. Sasa kama mshahara analipwa kama kawaida, tatizo liko wapi?
Ikabidi jamaa afunguke. Akasema kwamba huo mshahara wake ni mdogo sana na siku zote si wa kuutegemea, yeye anachotegemea ni ma deal anayoyafanya akiwa kazini. Na bila kuwa kazini hata akilipwa huo mshahara, hayo ma deal (rushwa) hawezi kufanya.
Basi Mzee Mwinyi akawa kapatq elimu fulani kuhusu ukubwa wa suala la rushwa serikalini.