Athari za mishahara duni ya Watumishi wa Umma

ukithubutu kula rushwa au hela ya serikali utaitapika kwa pua sio mdomo.
usicheze na rushwa au hela ya serikali, kama unabisha jaribu uone
 
ukithubutu kula rushwa au hela ya serikali utaitapika kwa pua sio mdomo.
usicheze na rushwa au hela ya serikali, kama unabisha jaribu uone
Mbona wao hawakutosheka wakakimbilia kwenye siasa?!
 
Mbona wao hawakutosheka wakakimbilia kwenye siasa?!
bora na wewe ukimbilie huko huko angalu utasalimika kuliko kujaribu kula rushwa au kuchezea hela ya serikali utaumia bure uache watoto wako wanakulilia.
 
Hiyo mishahara ni shs ngapi

Weka Salary slip hapa za wafanyakazi..
Mbona una hasira sana? Kuna nongwa gani mtu kutoa maoni yake. Unamuambia akae kimya kama nani?

Mnataka muwe mnasikia mapambio tu na nyimbo za utukufu za kumsifia dikteta wenu. Hovyo kabisa.
 
Kingine ni mishahara midogo husababisha motisha ndogo ya kufanya kazi.

Wafanyakazi wanasema serikali ina pretend kuwalipa mishahara, na wao wafanyakazi wana pretend kufanya kazi.
Na huu ndiyo ukweli mchungu. Kwa sasa kazi inafanyika kwa kulazimishana na pia kwa kutishana! Maana wanafahamu fika upuuzi wanao ufanya kwa wafanyakazi.
 
Hiyo mishahara ni shs ngapi

Weka Salary slip hapa za wafanyakazi

Ukubwa wa hela kwako unaanzia shs ngapi?...
We acha upoyoyo, wewe kila siku hapa Salary scale za waalimu na manesi TGTS na TGHS respectively zinawekwa hapa utanaka ref. ipi zaidi?
 
watakuwa wamekusikia mkuu
 
Point ni zilezile mwaisa

Low capital
Poor gornment support
Poor infracture

Apo ndo Q-Net ,, Smile we care ,, Wanaponyoosha watu
 
Atujamkosea Mungu kupita kiasi hicho Hadi atususe hivyo
Kipindi cha JK kuna time tulikaa na washkaji, tukawa tunaponda utawala wake ulivyokuwa wa ovyo.

Mimi nikawaambia, huyu ana makosa mengi, lakini msishangae ajaye akiwa mbaya kuliko huyu.

Wakacheka na kuona kama utani, wakasema kama ulivyosema wewe, kwamba hapa tulipo tumefika rock bottom. Ukianguka mpaka chini, huwezi kuanguka chini zaidi.

Nikawaambia, tulieni muyaone.

Guess what?

Tumepigwa daflao mpaka wanamtamani JK sasa hivi.

Time will tell.
 
Hivi kati ya watumishi wa umma, watumishi wa sekta binafsi, na wakulima, ni kundi lipi linapata mapato mazuri zaidi kwa wastani?
Nauliza tu jamani nieleweshwe
 
Mwanaume gani wewe??una gubu
 
Unaweza kuambiwa hiyo mi nne ikiisha, inaanza mingine kumi ya kulia na kusaga meno.
Mkuu Wewe endelea kufaidi dunia huko uliko. Waachie kilio wenye msiba wao. Usiwakatishe tamaa zaidi.

Hii nchi ilishakuwa ya hatari tangu awali. Nyerere aliposema kwa katiba hii anaweza kuja dikteta mbaya sana, Watanzania walipuuza wakijua “ulaji mezani kwako” waliouzoea utaendelea kama kawa hivyo hakuna haja ya kuhangaika na masiasa.

Tena miaka ile ukiuliza habari za mshahara au pensheni unaonekana kama kibwengo fulani hivi; umefulia kweli kweli. Kazi ya maana ilikuwa ni ile yenye “ulaji” mkubwa. Mishahara karibia yote ilikuwa peanuts. Wafanyakazi hasa serikalini wamshukuru sana JK (awamu ya 4) kwa kuhuisha mishahara na pensheni za sekta ya umma mpaka kufikia kuwa kigezo cha kuvutia ajira hizo. Kiasi cha watumishi wengi kusahau habari za rushwa na fojari za risiti. Watu wakaanza kujadili mishahara na pensheni serikalini!

Leo hii watu wanamdai Magufuli ajira, vyeo, nyongeza za mshahara kwa vile Kikwete aliongeza thamani kubwa katika vipato hivyo vya watumishi wa umma kwa namna ambayo haikufikirika huko nyuma. Waliotumikia awamu za 1 hadi 3 wanajua. JK aliposema “mtanikumbuka” alipokuwa akiaga tukacheka sana nadhani alijua kuhusu “yajayo”. Eti “nawaletea chuma hiki; kinatema cheche!” 😂 Bila shaka aliiangalia ile “wage bill” ya sekta ya umma ilivyokuwa na ukubwa wa kutisha akajua chuma kikishakamata hatamu hatua namba moja kitawahi Hazina na kufyekelea mbali maslahi kibao.

Safari ya kurejea awamu za 3 > 1 ndio ilishaanza tena huku sekta za umma na binafsi zikizidi kusinyaa. Haitakaa itokee mishahara iongezwe serikalini Labda selectively kwa “wateule” na “watu maalum”. Kwenye siasa nako ni sauti moja tu ndiyo inayosikika sasa ikihanikizwa na miangwi ya kila aina na shadidi za mapambio ya kusifu na kuabudu. Hakika kama Watanzania wataendelea kukwepa wajibu wao wa kisiasa, basi ni mi-kumi zaidi ya kilio na kusaga meno. Hakuna namna. 😢
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…