Athari za mishahara duni ya Watumishi wa Umma

Mkuu

Habari ya mishaahara kuwa midogo na watu kutegemea rushwa serikalini inanikumbusha story moja ya enzi za "Fagio la Chuma" la Mzee Ruksa.

Mzee Ruksa, Rais Ali Hassan Mwinyi, mwenyewe alihadithia habari hii katika hotuba kuonesha ukubwa wa tatizo la rushwa.

Alisema kwamba, alikuwa na ndugu yake mmoja anafanya kazi serikalini. Sasa yule ndigu yake, akawa na tuhuma fulani kazini. Akasimamishwa kazi ili ufanyike uchunguzi. Wakati kasimamishwa kazi, analipwa mshahra wote kama kawaida.

Sasa huyo jamaa aliyesimamishwa kazi, akamfuata Mzee Ruksa. Akamwambia Mzee, nakulililia sana. Tafadhali nirudishe kazini, hali ni mbaya nina familia na watoto.

Sasa Mzee Rushwa akamuuliza huyo ndugu yake, wewe umesimamishwa kazi unalipwa mshahara au mshahara hawakulipi?

Ndugu yake akamjibu mshahara analipwa kama kawaida.

Mzee Ruksa akashangaa sana. Akamuuliza tena. Sasa kama mshahara analipwa kama kawaida, tatizo liko wapi?

Ikabidi jamaa afunguke. Akasema kwamba huo mshahara wake ni mdogo sana na siku zote si wa kuutegemea, yeye anachotegemea ni ma deal anayoyafanya akiwa kazini. Na bila kuwa kazini hata akilipwa huo mshahara, hayo ma deal (rushwa) hawezi kufanya.

Basi Mzee Mwinyi akawa kapatq elimu fulani kuhusu ukubwa wa suala la rushwa serikalini.
 
If you think money can't buy happiness go and ask the homeless and the jobless...

#YNWA
 
Mkuu lack of vision ya hawa wahuni inairudisha nyuma sana Nchi yetu. Mtu mmoja tu kwa sababu ana Phd fake ya kuunga unga basi kila kinachotoka kinywani mwake hata kama kinakiuka sheria na taratibu mbali mbali za nchi ni sheria ya Nchi na kinapigiwa makofi kama yote.

Kajisemea Jenerali Ulimwengu tumerudi nyuma miaka 50, mimi naona tumerudi nyuma miaka 70 na miaka mitano ijayo kutakuwa na vilio vya kusaga na meno kwani Watanzania wengi wataingia kwenye kundi la ufukara wa kutisha.
Mark my words Mkuu unless there is a huge change in the leadership and the direction of our beautiful country.


 
Kuna Wapumbavu ndani ya maccm na hii Serikali haramu ambayo 2024 wanaweza kabisa kuanza kampeni ya nguvu ya kumshawishi huyo anayejiita mwendawazimu aendelee mitano mingine au kuongeza awamu kwa miaka miwili.

Katiba ya Nchi imeshachezewa sana, imeshadharauliwa sana ni kama vile hatuna katiba ni bora liende tu chochote kitakachotoka kinywani kwa nanihii basi ni sheria mpya ya Nchi.

Inasikitisha sana lakini Tanzania na Watanzania tunapitia kipindi kigumu sana ambacho wengi hatukutegemea kukiona.
Hili lisitokee tafadhali 10 inatosha.
 
Ukweli mtupu na hata mwaka huu hatatoa nyongeza ya mishahara labda kwa wajeda tu ili wasije kumgeuka. Kwahiyo, tutarajie vilio zaidi kutoka watumishi na hata wasio watumishi kwani uchumi teyari umevurugwa.

Kwakuwa ameshaharibu uchumi, tusitarajie eti ataongeza mishahara ya wafanyakazi maana hela sasa hana, hivyo ataishia kutisha watu au kuendelea kuwapa watumishi matumaini hewa ya kuboresha masilahi yao kama ambayo amekuwa alifanya tangu aingie madarakani.
 
Reactions: BAK
Umejitahidi Sana lakini sijui Kama hao watumishi wa umma wamekuelewa. Ili wskuelewe inabidi wastaafu halafu wakutane na adha za dunia hii........ Ila kwa mbaaaalsomo linaanza kuwaingia kwa namna Bei ya vitu vinavyopanda bila kushuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…