Athari za Mkopo wa Biashara, Baada ya kukopa mkopo wa biashara kutoka Benki, nimejikuta katika hali ngumu sana

Athari za Mkopo wa Biashara, Baada ya kukopa mkopo wa biashara kutoka Benki, nimejikuta katika hali ngumu sana

Tatizo sio mkopo ndugu tatizo ni ile riba ndo inakufanya uwe maskini

Muumba ameshakataza biashara za riba ila binadamu hawasikii na huna la kuwaambia

Juzi nilimsikia askari mmoja anasema kuna mwenzangu anataka kukopa 22M ila kaambiwa arudishe 34M
34-22=12M sasa huu ni unyonyaji bora utafute chako kwa njia nyengine tu lkn si kwa hii mikopo umiza
 
mkopo wako wa 110 ulichukua lini?na ulikua unafanya biashara gani?
Katika maisha hua inafikia kipindi inakulazimu kuanza upya bila wewe kupenda,
Kubali kuanza upya brother tupo wengi sana tuliopitia hali za namna hii na tupo tayari kuanza upya kitu cha msingi ni kwamba umetambua na kuelewa hautoweza kulipa hilo deni kutokana na changamoto za kibiashara ,ninakushauri anza upya au Kwa namna hii.
1-Hiyo nyumba tafuta mteja bargain nae uiuze Kwa bei unayoitaka wewe hata kama documents zote zipo benk hakikisha mteja umempata wewe na sio benk wakuuzie na madalali wao utapoteza zaidi kwasababu once ukitafuta mteja wa kuinunua utauza Kwa bei unayoitaka wewe na sio Kwa matakwa ya benki ,faida ya hii ni kwamba lazima utabaki na kiasi kingine cha fedha ambacho utakitumia kama mbegu tena then ukiwa free zaidi kifedha.
2-Nasisitiza usitoe room ya benk kuuza hiyo nyumba,isipokua anza kutafuta mteja wewe mwenyewe ili kuepusha uhuni wa madalali kwani itakupa msongo zaidi kutokana na kupoteza kila kitu bila kuambulia chochote.
3-Pesa utakayoipata kutoka kwenye mauzo hayo baada ya kulipa pesa yote unayodaiwa moja Kwa moja bila kuchelewa hakikisha unatafuta kiwanja ili uanze ujenzi taratibu wa nyumba ya familia bila kusahau kulipa kodi walau hata ya mwaka mmoja au miaka miwili ili familia isiteseke then pambana hopefully utatoboa.
Maisha ni kamali hakuna ajuaye Kesho ya mtu ni wito wangu kwako kutokurudi nyuma na usikubali kushindwa Mungu akubariki na atupe moyo wa uvumilivu na azidi kutuongoza kuelekea mafanikio 🙏
 
Utajiri namba Moja Duniani ni kua na uwezo wa kukopesheka, Fanya Kila namna uwe na uwezo wa kukopesheka hata kama sio pesa nyingi



Juzi tu Elon musk tajiri namba Moja Duniani alisema yeye utajiri wake mwingi upo kwenye hisa za kampuni zake, akasema Hela cash hata Dola milioni 10 anaweza asiwe nayo, hayo madollar bilioni zote mnazoona zipo kwenye hisa za kampuni zake sio kwamba ziko bank zimekaa tu, na akasema ana mikopo mingi tu..... Hawa kina mo, bakhressa watazidi kua na Hela Sana maana wakipata propasal wanaingia bank chap wanavuta pesa ya mkopo wanaanzisha viwanda/kazi mpya....


Shida kubwa bank zetu riba sio rafiki kabisa, tunalia tenda za ndani zote wanapewa wageni, Sasa una kampuni inatokea tenda asilimia zaidi ya tisini za kampuni wanategemea mikopo kuendesha kazi zao, unaenda bank unakutana na riba 18%, lazima uweke bei ambayo utamudu kulipa huu mkopo, unakutana na kampuni za china kwao wanapewa mikopo Kwa interest ya 4%, mkipeleka proposal zenu we unaonekana una gharama Sana maana hapo mkopo unakubana, serikali wanatoa tenda Kwa wageni maana bei zao zinakua nafuu..


Kuna kipindi mo dewji alizungumzia hili, akadai matajiri wengi wa Tanzania wanachukua mikopo south Africa Kwa interest rate ya 6-8%
Hio 18% ni riba ndogo sana ,kwa mikopo ya biashara baadhi ya bank wana charge mpaka 27%..
 
110 million, dhamana nyumba ya familia na ipo mjini😭
Marejesho ya milioni 10 kwa mwezi,uko vizuri,huwezi kopesheka kama huna sifa za kukopesheka.

Pambana ulipe mkopo ,acha Kutafuta huduma za mtandaoni,hazita lipa deni
 
Biashara imeenda ndivyo sivyo au?

Anyways, biashara haiwezi kukua bila mikopo, ila kopa kimkakati.
 
Deni linakopwa tayari upo kwenye movement ila tofauti na hapo lazima ulie tu.
 
Back
Top Bottom