SoC02 Athari za siasa katika Utawala wa Sheria

SoC02 Athari za siasa katika Utawala wa Sheria

Stories of Change - 2022 Competition

fikirakali

Member
Joined
Sep 15, 2014
Posts
15
Reaction score
18
Katika siku za hivi karibuni limeibuka wimbi la watu wanaodai kuwa siasa ni kila kitu katika maisha. Je ni kweli kuwa siasa ni zaidi ya sheria ambayo ndio uti wa mgongo katika utawala bora?

Kwa Jicho pevu kabisa naweza kusema hapana si kweli kuwa siasa ni zaidi ya sheria. Ili kupata utawala bora tunahitaji siasa inayozingatia sheria ili kufikia lengo la utawal bora.

Siasa ni nini?
Siasa ni itikadi ya mtu au kundi la watu wenye lengo la kushika mamlaka, itikadi hii hupitia katika mgandamizo na mchujo maalumu ili kupata mwanasiasa ambae atabeba lengo kuu.

Sheria ni nini?
Sheria ni taratibu zilizowekwa katika maandishi ambazo hutoa mwongozo wa nini kifanyike katika utaratibu upi na nini kisifanyike, pia hutoa suluhisho kama jambo litakuwa kinyume.

Utawala bora ni nini?
Utawala bora ni utawala unaozingatia sheria.

Ni kwa kiasi gani siasa zimekuwa kikwazo kwa utawala wa sheria?

Ili kufikia malengo yao, wanasiasa wamekuwa wakitumia mbinu nyingi, moja ya mbinu yao kubwa ni kuipindsha sheria na wakati mwingine kutumia nafasi zao kuleta sheria ambazo zitakuwa rafiki kwao bila kujali matakwa ya Katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama.

Kwa mfano kupata na kutoa habari ni takwa la kikatiba lakini utaona sheria ya habari iliyotungwa mwaka 2016, mwaka mmoja tu baada ya Rais wa awamu ya tank kuingia madarakani. Malalamiko yamekua mengi na hii ni kutokana na kutozingatia katiba inataka mini juu ya upatikanaji wa habari.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom