Nakupongeza kwa maoni na mtazamo wako, tofauti ya wachezaji wawili kwa msimu ujao ndio utawezesha hilo?10 players tulishindwa nini? Wachezaji wa kigeni ni hasara kwa taifa hili, kwanza hao makocha wana mkakati wamepewa wa kuwanoa wazawa na sharti la kuwapa namba au wako huru kuamua wapangeje first eleven zao, mapato na matumizi ya hao wachezaji wa kigeni uwiano ukoje? mfano mauzo ya jezi OG wanamvuto wowote?je wanatumika kibiashara? Malengo mafupi, ya kati na muda mrefu ya kusajili hao wageni kwa vilabu, ligi, na tff ni yapo, na je kuna review program ya kuangalia matarajio ya kuwa na wageni kila msimu na tathimini ya mrejesho ipo? Hivi tuna uhalali wa kujifananisha na mataifa yapi na kwa vigezo vipi kwa faida ipi na malengo yapi na je hayo ndio yafananayo na tunaotaka kufanana nao?