Athari za Uchaguzi Mkuu, Azam TV wapandisha bei za vifurushi?

Mitano Tena!
Na hapa ni mwanzoni tu.
 
Mimi nashangaa watu mnahangaika na ving'amuzi vya Azam..
But ishu kubwa saivi ni kupanda kwa mafuta ya kula yanayomgusa kila mtu..
Mwanzoni nikikuwa nachukua ndoo ya lita 20 kwa bei ya jumla kwa tsh 56k saivi ninavyozungumza ndoo ni Tsh 69k kwa bei ya jumla kwa mtu anayenunua kuanzia ndoo 5 na Tsh 72k kwa mtu anayechukua chini ya ndoo 5 kwa hyo imebidi nipandishe bei kutoka Tsh 3500 kwa lita hadi 4000 na ninavyozungumza bado yanazidi kupanda bei wao wapo kimya tu..
Ama kweli tunalipia gharama za uchaguzi..
 
Hiyo bei bado iko chini sana ukilinganisha na baba la pay TV Dstv! Besides, tupo uchumi wa kati! [emoji846]
 
Uchaguzi Mkuu umeingiaje hapo Mkuu?
Au ni hasira za kukosa Jimbo?
Jitieni jeuri na majibu ya midomo juu kama bata maji ... ila mkae mkijua mpaka March 2021 tutaongea lugha moja!

Tena lugha moja ya kuelewana "MAISHA MAGUMU"
 
Hiyo bei bado iko chini sana ukilinganisha na baba la pay TV Dstv! Besides, tupo uchumi wa kati! [emoji846]
Usizungumze mambo ya dstv wasidanganye kusema wamepunguza wakati wamepandisha naamia Star, Azam nilikuwa napenda Azam two nitajizuia kuwaza maigizo maisha yamebana
 
Kila kitu kitapanda bei wafanyabiashara wote wanarudisha hela zao walizoichangia CCM wakati wa kampeni kwa idhini ya Mhutu mwenyewe .
 
Hatulipii gharama za Uchafuzi bali tunalipia ujinga wa mitano mingine tukijua mitano iliyopita ilikuwa hovyo watu tukaishi kama mashetani kwa sababu biashara nyingi zilifungwa na wafanya biashara na waajiriwa wao wakakosa vipato halali na vya uhakika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…