UTANGULIZI
Hivi karibuni tumeshuhudia Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania likifanya mabadiliko ya sheria ya fedha, (The Finance Act) na kuongeza kifungu namba 46A, kifungu kidogo(1) kinachosema kwa tafsiri isiyo rasmi; “Kutakuwa na tozo zitakazokatwa kwenye miamala ya fedha kwa njia ya simu zitakazoanzia Tsh. 10 mpaka 10,000.”
Mabadiliko haya ya sheria ya fedha yameleta tafrani na sintofahamu kubwa kwa umma wa watanzania. Wengi wameitafsiri sheria hii kuwa ni sheria kandamizi. Wakati huo huo, waziri mwenye dhamana Mh. Mwigulu Lameck Nchemba amekuwa akilitolea ufafanuzi suala hili kwamba tozo hizi zitakuwa na tija kwa maendelo ya taifa letu hasa kupeleka maendeleo mjini na vijijini.
Andiko hili linajikita kwenye kujadili athari zinazoweza kujitokeza kutokana na tozo hizi kwa uchumi wa Tanzania. Haya ni Mawazo/maoni huru ya mtanzania mwenye kiu ya maendeleo ya taifa lake.
KIINI CHA MADA
Ni dhahiri kwamba serikali ina malengo mazuri sana juu ya kuweka tozo hizi kwani kwa mujibu wa waziri wa fedha, mapato yatakayopatikana kutokana na tozo hizi yatakwenda kumalizia majengo ya zahanati mbalimbali ambazo hazijakamilika katika nchi yetu, kuinua sekta ya elimu kwa kujenga madarasa katika shule za msingi na sekondari, pamoja na kuimarisha sekta ya ujenzi kwa kujenga barabara za mitaa.
Pamoja na malengo mazuri ya kuanzishwa kwa tozo hizi, je, ni nini athari yake katika uchumi wa nchi yetu? Zifuatazo ni athari zinazoweza kujitokeza kutokana na kuanzishwa kwa tozo hizi;
Kuyumba kwa biashara ya miamala ya fedha kwa njia ya simu. Hii inatokana na jinsi watanzania walio wengi walivyolipokea suala hili. Wengi wameilalamikia Serikali kutokana na sheria hii na wengine wameenda mbali zaidi na kusema sheria hii ni kandamizi. Ni kwa sababu kwa mujibu wa maoni ya wengi tozo hizi ni kubwa sana kwani mteja anapofanya muamala hukatwa kiasi kikubwa cha fedha.
Imepelekea baadhi ya watanzania kuona ni afadhali mtu afunge safari kwenda kupeleka pesa anapotaka ifike kuliko kuituma kwa njia ya simu. Hii ni kwa sababu gharama ya kusafiri inaonekana kuwa ndogo ukilinganisha na gharama ya kutuma pesa husika kwa njia ya simu. Wengine wanasema ni afadhali warudi katika njia za zamani za kutuma pesa kama vile kwa njia ya mabasi kama wanavyotuma mizigo ya kawaida.
Hii ni dhahiri kwamba biashara ya miamala ya fedha kwa njia ya simu ikiwa ni Tigo-pesa, M-pesa, Airtel Money, HaloPesa, T-Pesa n.k itayumba sana kwa sababu kutokana na kuongezeka kwa tozo hizi, watanzania walio wengi wataacha kutumia huduma hii kwa kushindwa kumudu gharama hizi na kutafuta njia mbadala.
Kuongezeka kwa tatizo la ukosefu wa ajira.
Ikumbukwe kwamba biashara ya miamala ya fedha kwa njia ya simu yaani Tigo-pesa, M-pesa, Airtel Money, HaloPesa na T-Pesa, ni moja kati ya biashara zilizowapatia ajira vijana wengi wakitanzania hasa kijana wa kipato cha chini.
Hivyo ni wazi kwamba kuyumba kwa biashara hii kutapelekea vijana wengi kukosa ajira kwani biashara nyingi zitafungwa. Hii itapelekea tatizo sugu la ukosefu wa ajira kuongezeka katika taifa letu.
Kupungua kwa mapato ya Serikali yatokanayo na biashara ya miamala ya fedha kwa njia ya simu.
Wafanyabiashara wa biashara hii hulipa kodi kwa Serikali kupitia mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) lakini pia katika halimashauri za miji, wilaya, manispaa na majiji ambapo biashara husika ipo. Endapo biashara hii itayumba na wafanyabiashara wakaamua kufunga biashara zao, ni dhahiri kwamba Serikali itakosa mapato.
Kuongezeka kwa hali ngumu ya kimaisha kwa watanzania, hasa watanzania wa kipato cha chini.
Ikumbukwe kwamba, licha ya kuwa nchi yetu imeingia katika daraja la nchi za uchumi wa kati, lakini bado watanzania walio wengi wanaishi chini ya dola moja ya kimarekani, hii inaonesha wazi kwamba kipato cha watanzania walio wengi bado ni kidogo sana hivyo, watanzania walio wengi watashindwa kumudu gharama hizi za tozo zilizoanzishwa.
Huduma hii ya kufanya miamala ya fedha kwa njia ya simu, kwa muda mrefu imerahisisha maisha ya watanzania walio wengi na kuwapunguzia ukali wa maisha. Hivyo basi ikiyumba basi maisha ya watanzania walio wengi yatayumba pia.
Kuyumba kwa makampuni ya simu.
Ni wazi kwamba makampuni ya simu yanategemea sana biashara ya miamala ya fedha kwa njia ya simu ili kuweza kujiendesha.
Kutokana na kuanzishwa kwa tozo hizi ambazo zinapelekea biashara hii kuwa ngumu na kuyumba kutokana na mwitikio hasi wa watanzania, ni dhahiri kwamba makampuni ya simu yatayumba hata kupelekea kushindwa kujiendesha. Hii ni hatari kubwa sana kwa uchumi wa nchi yetu.
HITIMISHO
Baada ya kujadili baadhi ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na tozo mpya za miamala ya fedha kwa njia ya simu, napenda kuishauri Serikali yetu pendwa na sikivu na hasa waziri mwenye dhamana Mh. Mwigulu Lameck Nchemba kukaa tena upya na kulitazama suala hili kwa jicho la tatu. Ni suala ambalo kimsingi lina nia njema kwa taifa letu lakini ni gumu kiutekelezaji.
Kuna haja kabisa ya ama kupunguza viwango vya tozo hizi au kuachana nazo kabisa na kutafuta vyanzo vingine vya mapato vitakavyoweza kukidhi malengo haya ya Serikali. Nchi yetu imejaaliwa kuwa na rasilimali, na maliasili nyingi ambazo zikitumiwa vizuri zinaweza kutuvusha na kutufikisha pale tunapotaka kufika. Serikali inashauriwa kulitazama upya suala hili na kuja na suluhu stahili mapema iwezekanavyo.
Nawasalimu nyote kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
BLESSING RUSESEGWA (+255712112597)

Upvote
5