Atheists wameanza kuwa na uchungu na misimamo yao

Atheists wameanza kuwa na uchungu na misimamo yao

Mkuu Ahmet

Hapo umefanya ujumuishaji. Sio kweli kwamba wote wanapenda kubishana, humu jf wapo wengi tu, ila wachache ndo wanajitokeza.

Hata watu wa dini wapo humu wabishi kweli kweli na wanatumia hadi matusi, na wengine wanapigana wao kwa wao(uislamu vs ukristo)

Vita iendelee.
Sina hoja hapa😅😅
 
Ni mtazamo wako, kwaiyo we ukipinga uwepo wa Mungu, mimi naathirika wapi?

Nipe ushahidi kuwa na-apply projection or any kind of defense mechanism?

Hiyo assumption yako uliyoitumia kufikiri natumia projection ndivyo vivyo hivyo nasisi tunaoamini kuwa Kuna Mungu.
Ulimwengu kuwezekana kuwa na uchungu kwa yeyote ni ushahidi kwamba Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote hayupo.

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote angekuwepo, asingeumba ulimwengu unaowezekana kuwa na uchungu kwa yeyote.

Kwa hivyo, unaposema atheists wana uchungu, hata ikiwa kweli atheists wana uchungu, uchungu huo ni ushahidi wa kutokuwepo Mungu, ha hoja yako, ya kwamba atheists wananuchungu, badala ya kuwanyanyapaa atheists, inazidi kutoa ushahidi kwamba atheists wako sahihi na Mungu hayupo.

Unaelewa na kukubali hilo?
 
Nameelewa hoja yako na naikataa
 
Kama kweli naamini katika Mungu ukweli wa kuamini, kivipi nitakuwa na hasira au kumchukia mtu ambae naamini ataadhibiwa Kwa kutoamini kwakwe?
 
Kuna aina tofauti za jinsi watu wanavyoamini au kutoamini uwepo wa Mungu...

1. Kuna lile kundi kubwa la imani ya Dogmatism, ambao ni wenye kufuata dini, hawa wameshamezeshwa hivi vitu tokea wakiwa wadogo na ni vigumu kuwaambia kuwa aidha hakuna Mungu au kama yupo basi sio Mungu wa imani zao.

2. Kundi hili ni wale ambao wamepitia hizi dogmatism na kung'amua kuwa hakuna ukweli wowote wa uwepo wa mungu baada ya kutumia maandiko ya hizi dini kutafakari uwepo wa nayeamini kuwa ni muumba yote , mkuu wa yote na mwenye uwezo wa yote lakini hathibitishiki kwa kuwa waumini wenyewe wanawezaje kuteseka na maafa, majanga na shida lukuki, za kidunia ambayo inasemwa yeye ndio kazitengeneza na wakati huo yeye yupo na ni mkuu wa yote lakini hawasaidii waumini wake.

3.Kuna hili la tatu,
Haliamini ` dogmatism ya uwepo wa Mungu , na vilevile halitumii dogmatism ya uwepo wa Mungu kupinga uwepo wake, bali linatafakari kwa sheria za kisayansi za kiulimwengu (laws of the universe) bila kuhusisha imani ya dini yeyeto.....
Hili nitarudi kujadili na the greatest Kiranga
Alamsiki...
 
Nameelewa hoja yako na naikataa
Hujaikataa, umesema tu kwamba umeikataa.

Kuikataa hoja hapa inakubidi utoe hoja kuipinga hoja yangu, uchambue mantiki yake, uoneshe unaikataa hoja yangu kwa hoja gani, kwa mantiki gani, kwa mapungufu gani yaliyo katika hoja yangu.

Kama mimi nilivyochambua hoja yako na kuonesha mapungufu ya kimantiki katika hoja yako.

Wewe hujafanya hivyo.
 
1.Labda Sentient being ni nini?
Je kipi kina sifa za sentient na kipi hakina?

Ndio maana nikakushangaa unaposema nimeshindwa kujibu?

Embu tuangalie maana kwa Karne za Sasa

Sentience means having the capacity to have feelings. This requires a level of awareness and cognitive ability. There is evidence for sophisticated cognitive concepts and for both positive and negative feelings in a wide range of non human animals.
Concern yangu ni kwamba kwanini una hitimisha kwamba fungus na Bakteria sio sentient beings?

Na nimeuliza hivyo Kwasababu,...hata kwenye sayansi hakuna hitimisho la namna hiyo it's still debatable,
wewe unahitimisha kwamba fungus na Bakteria sio sentient beings wakati hauwezi kupima kama wana capacity yoyote ya kupata feelings,. Huoni unakua ume force kupata hitimisho ambalo sio kweli 100%?.
Sasa fungi Ina cognitive ability na awareness?
Wewe umejuaje kama fungi hana cognitive ability? umefanya research yoyote? Umetumia njia gani kwenye tafiti yako iliyokufanya uone hana cognitive ability?
NB: mpaka sasa tunavyoandika hapa hakuna hitimisho la jumla la kisayansi duniani linaloonyesha kwamba fungi hana cognitive ability.
Na hii inatoka kwenye mzizi wako wa hoja kusema Atheist wangekuwa hawamuamini Mungu basi wasingekula na vikorombwezo vingine.

Je, Backteria Wana mhitaji huyo mnaye msema,
Mzizi wa hoja yangu sio huo....

Bali hoja yangu imetoka pale ulipouliza ➡️,... Je, Bakteria na fungus wanamhitaji Mungu kwenye maisha yao.? Nikakuambia inafaa hilo swali uwaulize hao viumbe wenyewe ndiyo wana majibu sahihi zaidi..elewa neno "Viumbe"
 
Hivi kwanini Hawa atheists wa JF wamekuwa na uchungu sana pindi mtu unapozungumzia uwepo wa Mungu na jambo jengine linalohusiana na Imani?

Yaani wanautetea huo u-atheism wao kwamba kama hukuufuata basi Kuna adhabu itakukuta. Mambo yamebadilika sasa yaani wao ndio wanaongea Kwa uchungu kuliko watu wenye kuamini Mungu. Tunaoamini uwepo wa Mungu tumetulia tuli na tumeridhika na Imani yetu.

Sasa huwa najiuluza kama wewe huamini Mungu, Wala maisha baada ya kifo, kwanini utumie nguvu kubwa kuwaamisha watu katika hilo. Ni kweli Imani katika Mungu huleta vita, umaskini na Migongani? Hata kama kweli but dunia hii ingekuwa mbaya zaidi bila Imani katika Mungu. Kwasababu hofu ya Mungu Kwa kiasi kikubwa imefanya watu walimit baadhi ya matendo yao.

Si kweli kwamba Imani katika Mungu huleta umaskini. Angalia nchi kama UAE, Qatar, Saudi Arabia na nyengine nyingi asilimia kubwa ya raia wake wanaamini katika Mungu. Hata hizo nchi nyingi ambazo zina atheists wengi, zilipata maendeleo kipindi raia wake wengi walikuwa waamini Mungu, angalia nchi za Ulaya na Amerika.

Angalia hata mabilionea wetu wakina Mo Dewj, Rostam Aziz, Bakhresa na wengine wanaamini katika Mungu. Tajiri namba Moja Afrika ni muumini wa uwepo wa Mungu. Na wamefanikiwa kuliko atheists.

Sasa nini kinawasukuma hawa mabwana kuwa na uchungu sana pindi mtu aletapo habari za Mungu, miujiza na maisha baada ya kifo. Tena wengine hawalali, ni kama marobot, wako active muda wote, ukiandika tu mada kuhusu mambo ya Mungu, basi watakujibu kwa ma-essay marefuu kukupinga.

Kama unaamini hakuna Mungu basi relax kwasababu unaamini hakuna kitakachotokea. Umesha-confirm kile unachokiamini kwanini utake kuwa-drag watu katika msimamo wako.

Kama unahisi kuamini hivyo unavyoamini Kuna faida, basi tumia hiyo fursa wewe, make changes, boresha maisha yako alafu waache wenye kuamini katika tabu zao, na kutapeliwa kwasababu mimi naamini utakuwa na nafasi kubwa ya kufanya makubwa katika group la wajinga wengi kama mnavyosema.
Atheist ni wajinga tu ni watu walojiamulia kuendekeza matamanio yao huku wakisema hakuna MUNGU

Mbona wazazi wanawajua? Baba zao na mama zao wanawajua hlf wanakwambia hamna MUNGU huu ni upumbavu wa kiwango cha SGR
 
Umeongea vizuri sana. bila imani ya mungu, dunia pangekuwa mahali pabaya sana.

Hiyo ni imani tu. Ila Mungu hayupo. Angekuwepo angetimiza ahadi zake. Kuna watu wanaomba usiku na mchana dunia pawe mahali pa amani, lakini ndiyo kwanza uovu unazidi.

Ina maana hasikii?

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Na wanajiona wana akili kuliko watu wote duniani hapa- wanaongeaga wakijionesha jinsi walivyo na uelewa kuliko wengine na matusi juu...hata hapa ukipitia comments kuna matusi tayari....Kuna shida sehemu kwa hawa watu, sio bure
 
Point sana!!!

If God doesn't exist, why even bother about anything at all?

Kiranga
Infropreneur
Aisee Kwahio kwa Logic yake you do Good because its the will of the Gods na sio its good because of the will of Gods..., Kwa logic yako hio ndio maana leo watu wanafanya mabaya na kujipa justification wana-qoute vijimistari vya kwenye Imani yao....

Binafsi kama kweli mbingu ipo na huko takuwa na watu ambao I can not stand them here (hypocrites, hubrus na judgmental) wakati tunaimba na kusifu siku nzima huku tunawachoma moto so called wabaya ambao ni ndugu zetu na marafiki zetu huku tunachekelea ni bora Imani ya Wasabato iwe kweli na nikifa nilale wala nisiamke kamwe ( I can't see any good about such life)

By the way kwa logic ya mleta Mada sababu kwa Imani yake sasa hivi anafahamu (sio kuamini tu) kwamba jua / mizimu sio Mungu basi hatakiwi kuchangia mada ya kutokuwepo kwa Mizimu Mungu...
 
Hivi kwanini Hawa atheists wa JF wamekuwa na uchungu sana pindi mtu unapozungumzia uwepo wa Mungu na jambo jengine linalohusiana na Imani?

Yaani wanautetea huo u-atheism wao kwamba kama hukuufuata basi Kuna adhabu itakukuta. Mambo yamebadilika sasa yaani wao ndio wanaongea Kwa uchungu kuliko watu wenye kuamini Mungu. Tunaoamini uwepo wa Mungu tumetulia tuli na tumeridhika na Imani yetu.

Sasa huwa najiuluza kama wewe huamini Mungu, Wala maisha baada ya kifo, kwanini utumie nguvu kubwa kuwaamisha watu katika hilo. Ni kweli Imani katika Mungu huleta vita, umaskini na Migongani? Hata kama kweli but dunia hii ingekuwa mbaya zaidi bila Imani katika Mungu. Kwasababu hofu ya Mungu Kwa kiasi kikubwa imefanya watu walimit baadhi ya matendo yao.

Si kweli kwamba Imani katika Mungu huleta umaskini. Angalia nchi kama UAE, Qatar, Saudi Arabia na nyengine nyingi asilimia kubwa ya raia wake wanaamini katika Mungu. Hata hizo nchi nyingi ambazo zina atheists wengi, zilipata maendeleo kipindi raia wake wengi walikuwa waamini Mungu, angalia nchi za Ulaya na Amerika.

Angalia hata mabilionea wetu wakina Mo Dewj, Rostam Aziz, Bakhresa na wengine wanaamini katika Mungu. Tajiri namba Moja Afrika ni muumini wa uwepo wa Mungu. Na wamefanikiwa kuliko atheists.

Sasa nini kinawasukuma hawa mabwana kuwa na uchungu sana pindi mtu aletapo habari za Mungu, miujiza na maisha baada ya kifo. Tena wengine hawalali, ni kama marobot, wako active muda wote, ukiandika tu mada kuhusu mambo ya Mungu, basi watakujibu kwa ma-essay marefuu kukupinga.

Kama unaamini hakuna Mungu basi relax kwasababu unaamini hakuna kitakachotokea. Umesha-confirm kile unachokiamini kwanini utake kuwa-drag watu katika msimamo wako.

Kama unahisi kuamini hivyo unavyoamini Kuna faida, basi tumia hiyo fursa wewe, make changes, boresha maisha yako alafu waache wenye kuamini katika tabu zao, na kutapeliwa kwasababu mimi naamini utakuwa na nafasi kubwa ya kufanya makubwa katika group la wajinga wengi kama mnavyosema.

Atheism: Imani nusu na robo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo atheist wakiwauliza maswali hua hamna majibu, mnakimbilia kusema huna imani

1. Naman alijichovya mtoni mara saba akapona ukoma, kuna watu wangapi wamepona kwa staili hiyo..?

2. Kama mbinu sahihi Mungu aliona kuwa kupiga maji bahari inafunguka mbona hao wazungu hawatumii fimbo tena wanapanda meli...😂😂

Mambo ni mengi sana, hamna majibu nayo
 
wa na frustration.
Mungu haitaji kutetewa.
Kama Mungu haitaji kutetewa, Kwa nini kila kukicha huku JF nyuzi za mahubiri ya huyo Mungu haziishii?

Mara nyuzi za kumjua Yesu na kuokoka, Mara wengine kumjua Allah na kusilimu, Mara kupokea wokovu na uponyaji n.k

Yani mnamtetea Mungu kwa nguvu zote za ushawishi na mahubiri.

Sasa swali ni hivi👇

Mungu huyo, Anashindwaje kufahamika na binadamu wote kwa wakati mmoja na kwa namna moja?

Kwa nini kila mtu ana namna yake ya imani ya kumjua Mungu huyo?

Mungu huyo anashindwaje kujidhihirisha kwa watu wote duniani kumtambua yeye yupo pasipo utata?
Amejitambulisha kwa kila kiumbe.
Sisi Atheists mbona ameshindwa kujitambulisha kwetu?

Je sisi sio viumbe?
Ndio maana kila mtu huwa anamsukumo wa kutaka kuabudu higher authorities hata kabla hajajua mambo ya Mungu.
Ili uwe atheist inakubidi ujikane nafsi na Mungu ubebe mzigo wa ujinga wako ujifuate.
Mungu mnayedai ni muumba wa vyote, Aliumbaje binadamu ambao ni Atheists?

Kama Mungu alitaka aabudiwe na kuaminiwa na kila binadamu, Alishindwaje kuumba Binadamu wema tu wenye utii siku zote wakamwabudu na kumwamini?
 
Atheism: Imani nusu na robo

Sent using Jamii Forums mobile app
asante kiongozi, nimeelewa
 
Back
Top Bottom