Atheists wana mtindio wa ubongo

Naona umeishiwa hoja.
Hiyo ni hoja ya msingi sana na nadhani umeelewa lengo lake na ndio maana unatafuta uvungu wa kujifichia.

Huwezi kusema mtu ameona nyumba bila kuonesha uwezekano wa huyo mtu kuwa na ufahamu au ujuzi wa nyumba

Mtu akiwa na ufahamu wa nyumba maana yake, akiwa msituni akaona nyumba atawaza tu kuwa hii nyumba imejengwa (according to personal experience)

Kwa hiyo ili useme kitu flani ndio chanzo lazima uwe na backup uliyo i-exeperience inayokusapoti

Sasa ukisema ulimwengu upo na hauwezi kuwa umejiumba, je hiyo source ushawahi kui experience wapi ikifanya hivyo kwenye ulimwengu mwingine tofauti na huo?
 
Ni kweli hao jamaa wanazingua ila ukitaka kubishana nao kwa kutumia hoja hii uliyoileta wanakushinda ndani ya sekunde 1 tu
Mimi naamini uwepo wa Mungu. Ila asilimia 95% ya mijadala ya wanaoamini na wasioamini niliyopata kuishuhudia, basi wanaoamini huwa hawana hoja!

Atheists huwa wanajenga hoja za uhakika kuliko hawa waumini wenzangu!
 
uwepo wa Mungu unatambulika katika fahamu za mwanadamu kwa njia ya IMANI...na si logic. Ukitumia logic utafika mahala fulani utakwama.

Upo ushahidi wa kimazingira unaoipa nguvu hiyo IMANI ya juu ya uwepo wa Mungu. Hasa unapoangalia dunia na viumbe vilivyomo. Ukikaa chini ukatafakari kwa kina lazima utatambua uwepo wa huyo MUNGU.

Uwepo wake upo naturally katika fahamu zetu....hawa wanaokana uwepo wake wanadhani ni smart kwa kuleta maswali yenye mitego ya kilojikia...ila hata wao wenyewe hawana majibu ya chanzo chao na cha ulimwengu.
 
Mkuu, vipi kuhusu huyu MUNGU aliyeumba Dunia na huu ulimwengu wote? Kwa mantiki hii uliyotumia lazima atakuwa ameumbwa na MUNGU mkubwa zaidi, na hata huyo MUNGU mwingine naye atakuwa ameumbwa na mkubwa zaidi yake( there is no ending).

Kwa maneno rahisi ni hivi, kama haiwezekani ulimwengu kujitokeza wenyewe basi vile vile haiwezekani MUNGU mwenye uwezo wa ajabu WA kuumba ulimwengu kujitokeza mwenyewe bila kuumbwa.
 
Nilikuambia kuwa sababu ya mimi kunifanya nifikirie kuwa ni sahihi kuwaza nyumba imejengwa imetokana na awareness yangu katika mazingira yaliyonizunguka yanayonifanya nitambue nyumba zipo.

Awareness ndio imejenga personal experience ya kunipa utambuzi wa kujua hii ni nyumba

Awareness ya kujua mechanism ya jinsi nyumba zinatengenezwa ndio iliyonifanya nione ni sahihi kufikiria nyumba haijajijenga.

Those are facts based on personal experience

Sasa ukitoka katika mfano huo ukasema utumie hoja ya universe katika kujua chanzo ishu inakuwa ni irrelevant

Kuna maswali ya kujiuliza kabla ya kuendelea

Je huo ulimwengu ni wapi uliwahi kushuhudia ukiumbwa ili iwe sahihi kufikiria kuwa ulimwengu huu uliumbwa?

Una awareness yeyote based on personal experience ikionesha ulimwengu ukiumbwa?
 
Hatujibu kirahsii hivi. Onyesha huo utoto ulipo fanya kama navyofanya Mimi. Mimi nakosoa hoja yako wewe hatahija yangu huigusi unaruka ruka.
Kisema huo ni utoto ndio kuonesha kuwa ni utoto?
 
Hao walioafikiana ni kina nani?

Mambo yao wanayafanya wakiwa chini ya mwamvuli gani usiohusika na sayansi ambayo wewe unaiita ngano?

Ni ngano kutokana na disprove ipi ambayo umewa challenge?
 
Kijana haya unayo andika hayana maana, naandika kwa Kiswahili chepesi sana. Nyumba inaweza kujijenga au kutokea pasi na chochote ?

Siyo lazima uwe na uzoefu na kitu ndiyo ujue hakika yake. Uwepo wa kitu husika huonyesha uwepo wa mengine.

Kuna ulimwengu ngapi kijana ? Hili sharti la ku experience kitu ndiyo ujue uhakika wa mambo umelipata wap I? Sababu ni sharti mfu mno na halifanyi kazi katika uhalisia ndiyo maana nikasema hivi huna hoja unaleta utoto.

Siyo lazima uwe na backup, unapo ona uwepo wa nyumba kujua uwepo wake unahitajika kuwa na nini ? Kwahiyo wewe unapo dai Mungu hayupo ushawahi ku experience kutokuwepo kwa Mola katika ulimwengu (kama upo huo ulimwengu ) mwingine ?
 
Hao walioafikiana ni kina nani?

Mambo yao wanayafanya wakiwa chini ya mwamvuli gani usiohusika na sayansi ambayo wewe unaiita ngano?

Ni ngano kutokana na disprove ipi ambayo umewa challenge?
Kijana unafatikia mambo ya Sayansi ? Unaweza kunipa jaribuo lolote la Kisayansi lililo fanyika kuonyesha Dunia inazunguka ? Sasa kama huijui Sayansi achana na jambo hili. Utakimbia hii nada kijana.

Au ni jaribio gani la Kisayansi lililo fanyika kuonyesha Jua lipo katikati na Dunia inazunguka jua ?

Naposema ngano namaanisha mambo yakutungwa yakawekwa katika Sayansi. Ushawahi kuniuliza kwanini Einstein alikuja na ishu ya Special Relativity ? Lengo ni kumuhujumu Albert Michelson aliyethibitisha ya kuwa Dunia haizinguki kwa kutumia Light Beams. Sababu Einstein alikuwa muumini wa wa theory ya Copernicus akaamua kumuhujumu mwenzake.

Siyo Mimi tu wenyewe tu walisha chalenjiana kijana kitambo sana. Fatilia haya mambo. Kisha jibu maswali niliyo kuuliza.
 
Ndiyo maana nakwambia unaleta utoto, nilipo kuuliza wewe swali ukiona nyumba unaona nini au unajulishwa uwepo wa nini ni kule kutambua uhalisia, Sasa unakataa nini na unakubali nini ? Haya ndiyo madhara ya uoga na kutofikiria jambo liko wazi unalipinga na kulikiri, kwani hapa nilikuwa naongelea mambo ya maabara ?

Kwa maana hiyo kwa kukiri kwako hili, hayo mengine yote uliyo yaandika yafute hayana maana.

Na ujue tunaposema uhalisia tunamaanisha utambuzi ule wa kawaida kutokana na jambo lilivyo katika dhati yake.
 
What an answer!
Kudos mkuu
 
Awareness ya kujua mechanism ya jinsi nyumba zinatengenezwa ndio iliyonifanya nione ni sahihi kufikiria nyumba haijajijenga.

Those are facts based on personal experience
Maana yake uhalisia na ndiyo unao hukumu huu.

Ndiyo maana nilikwambia huko mwanzo kwa hali hiyo hakuhitajiki mtu kupewa ushahidi ya kuwa baba ni mkubwa kiumri kuliko mtoto, sababu uhalisia wa kimaumbile Usha hukumu na jambo ni lenye kujulikana.
 
Inakuwa Irrelevant kivipi ? Dunia IPO haipo ?

Uhalisia ambao timeutumia katika nyumba ndiyo uhalisia ambao upo katika dunia.

Kwamba uwepo wa kitu huonyesha uwepo wa vingine. Ndiyo maana huwa tunawaomba ushahidi mtuambie kama Dunia haijajiumba basi imejiumba. Je unao ushahidi huo au utuambie imetokana pasi na chochote.
 
Kijana haya unayo andika hayana maana, naandika kwa Kiswahili chepesi sana. Nyumba inaweza kujijenga au kutokea pasi na chochote ?
Hilo unalolizungumza wewe ni jambo la mbele baada ya hatua kadhaa kuzipita huku nyuma.

Hoja yangu imejikita kwenye hatua za mwanzoni kuhusu utambuzi wa kujua hii ni nyumba na inajengwa

Nazungumzia mazingira yaliyokujengea ufahamu wa kujua hii ni nyumba
 
Mimi naamini uwepo wa Mungu. Ila asilimia 95% ya mijadala ya wanaoamini na wasioamini niliyopata kuishuhudia, basi wanaoamini huwa hawana hoja!

Atheists huwa wanajenga hoja za uhakika kuliko hawa waumini wenzangu!
Mimi kwa mtazamo wangu wanaoamini uwepo wa Mungu wana hoja kuliko wale ambao Wanaamini hakuna Mungu
 
Siyo lazima uwe na uzoefu na kitu ndiyo ujue hakika yake. Uwepo wa kitu husika huonyesha uwepo wa mengine.
Kama huna uzoefu hukijui utajuaje kuwa hii ni nyumba?
 
.

Kuna ulimwengu ngapi kijana ? Hili sharti la ku experience kitu ndiyo ujue uhakika wa mambo umelipata wap I? Sababu ni sharti mfu mno na halifanyi kazi katika uhalisia ndiyo maana nikasema hivi huna hoja unaleta utoto.
Hilo ndio swali ambalo unatakiwa ujibu pale unapotaka kutoa tafsiri ya kitu ambacho hakijawahi kufanyika

Mtu anayesema nyumba inajengwa anakuwa na sababu ya kiuzoefu na hicho kitu inayomsapoti hoja yake kuwa nyumba zinajengwa.

Wewe unayesema ulimwengu umeumbwa, wapi uliwahi kushuhudia ulimwengu ukiumbwa ili iwe rahisi kufikiri huu ulimwengu nao uliumbwa?
 
Siyo lazima uwe na backup, unapo ona uwepo wa nyumba kujua uwepo wake unahitajika kuwa na nini ? Kwahiyo wewe unapo dai Mungu hayupo ushawahi ku experience kutokuwepo kwa Mola katika ulimwengu (kama upo huo ulimwengu ) mwingine ?
Kama huna backup inayokusapoti basi utakosa authenticity ya kusema habari za kuumba/kuumbwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…