Atheists wana mtindio wa ubongo

Atheists wana mtindio wa ubongo

Narudia tena Sayansi ni nini?
Maana bila uelewa wa pamoja inawezekana usielewe walichojaribu kukueleza waliopita.
Ngoja nikujibu swali hili kwanza, Kisha tunaiweka kiporo unijibu maswali yangu. Baada ya hapo tutarudi hapa.

Tamko Sayansi lina maana zaidi ya Moja, kama linavyo fasiriwa na wahudika, japokuwa Mimi siyo muumini sana wa Fasiri (Definitions),

1. Sayansi ni aina yoyote au Fulani ya taaluma au ujuzi. Yaani taaluma yoyote huitwa Sayansi, ndiyo maana tunaambiwa Social Science, Environmental Science na mfano wa hivyo.

2. Science is The systematic study of the structure and behaviour of the physical and natural world through observation, experimentation, and the testing of theories against the evidence obtained.
"the world of science and technology"

Sasa weka hiki kiporo, Kisha tutarudi hapa.
 
Safi kabisa, dosari ya Dunia ipo wapi ? Je kila kilicho pinda mathalani kina dosari au ukamilifu ?
Anha.. tuongelee dosari ktk kusupport uhai wa viumbe wa dunian
UV rays kutoka juani inatuongezea athari za kupata saratani ya ngozi, sio ukamilifu huo kwa viumbe wa dunia..
muda wowote kimombo kinaweza kukudondokea kikakuua, hakuna ukamilifu hapo
forest fires,
matetemeko
radi inaweza kukuchapa ikakuua

Life generally iko katk delicate balance. Ukiondoa kiumbe mmoja (au mmea) ktk eco system, anaweza kusababisha viumbe wengine wengi zaid kutoweka..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikikuuliza swali, onyesha Jua limetengenezwa vipi na Sayansi au Sayandi Ina nafasi gani katika Sayansi ?
Jua limetengenezwa na sayansi kivip sasa ww? Hapa hatuko mahakamani, hatuongelei kila kitu literally. Most man-made things vimetengenezwa kwa uwezo wa sayansi... sasa unapoipinga sayansi na kusema sayansi ni theory tu skuelew

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi kabisa, dosari ya Dunia ipo wapi ? Je kila kilicho pinda mathalani kina dosari au ukamilifu ?
Kwenye ulimwengu uliojaa dhiki, dhulma, fitina, kijicho, nuksi, mauaji na kila aina ya ushenzi inaonyesha Dunia ina dosari na ulimwengu kwa ujumla.
 
Haipo hivyo na hata wewe uki-force basi utajikuta unahukumiwa na mfumo huo

Nakupa mfano

Ukiambiwa kuwa kuna binti wa miaka 20 ambaye ana mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 5, utakubali kuwa watu hao wapo?

Au utasema hujui?

Kumbuka ukisema hujui watu hao kama kweli wapo (kuwa neutral), maana yake umekubali kuwa upo uwezekano wa huyo binti na mama yake mzazi mwenye umri ule kuwa wapo vile vile kama ilivyoelezwa ila huna uwezo tu wakutafiti

So kwenye situation hiyo ebu tupe jibu lako

Halafu tuambie kitu gani ambacho kwako wewe unahakika kuwa 100% hakipo tuangalie kama hicho kitu hakina uwezekano wa kuwa tofauti na wewe ulivyokipokea.

Halafu utatupa sababu kwanini haukuchagua kuwa neutral kwenye hicho kitu
Kama haipo hivyo, iko vipi?

Mfano wako una uhusiano gani na uwepo wa Mungu au la?

Hata hivyo, katika mfano wako ameandika sentensi "mama mzazi". Naamini unafahamu kwa undani maana ya sentensi hiyo. Utakuwa unajua zaidi uhalisia, kwa nini mama mzazi amekuwa na umri madogo kuliko binti yake.

Huo mfano sijatoa mimi, umeutoa wewe. Inakuwaje sasa unataka mimi nitoe maelezo ya mfano ulioutoa wewe? Ni wewe wa kutoa maelezo, kwa kuwa unajua ni ujumbe gani unataka kufikisha.

Toa maelezo ya mfano wako na kisha lete maswali yenye majibu yanayowiana na mfano huo.
 
Ukikutana na tuseme mimi sehemu tukiwa wawili tu na hakuna aliyetuona yeyote na ukawa haukuchukua ushahidi wowote baada ya hapo nikawa labda nimefariki, na badae ukaenda kumwambia rafiki yako kuwa tumekutana sehemu fulani, akabisha na kukudai utoe uthibitisho utafanyaje aamini tulikutana..?
Sasa kama hujachukua ushahidi utaaminikaje kuwa ni mkweli?

Ni kweli una miliki nyumba, ila umeenda benki bila hati ya nyumba ukasema uombe mkopo wa milion 100.

Unafikiri utaweza kuaminiwa kuwa umesahau hati nyumbani hivyo wakupe mkopo?

Hiyo inamaanisha kwamba tukiruhusu hilo swala, tunakuwa tumeachia mwanya kwa madai yeyote ya uwongo as long as kila mmoja atakuja na viapo kuwa hicho kitu ni kweli
 
Mnaobisha hakuna Mungu hoja zenu ni kuwa sisi tunao amini tuthibitishe uwepo wa Mungu, labda kuwaonesha huyo Mungu au yeye ajioneshe kuwa yupo..! Mnasahau wanaodai Mungu yupo madai yao yanaeleza Mungu kama Roho (kitu kisicho umbo). Mnasahau Mungu wa waaminio haonekani, hagushiki, na wala havhunguziki kwa science ambayo nyie mnataka sie waaminio tuitumie kuwaaminisha nyie msioamini.
Kama imani ni njia ya kweli kujua ukweli wa jambo basi tungekuwa na imani moja yenye kuamini Mungu mmoja

Since tuna bunch of faith tena zinazo pingana basi hoja ya kusema Mungu yupo kwa imani haiwezi kuwa na mashiko
 
Kiufupi sisi Mungu tunaye mwongelea ni

God who's beyond our mind, beyond our reasoning, beyond the human sciences, beyond your thinking capacity and that's why you fail even to understand Him. Wanao mwelewa/kumjua si kwa uwezo wao bali kwa utashi wake amewapa neema kumjua na kumfahamu. Kwa namna unavyosupaza shingo neema yake akiona inafaa anaweza jithihirisha kwako kabla ya kukukata kichwa/kufa)kukata shauri.
Kilicho beyond your grasp, we umekijuaje?

Umejuaje kama amewapa watu neema ya kujua wakati ujuzi wako upo limited kuweza kumuelewa?
 
Kama haipo hivyo, iko vipi?

Mfano wako una uhusiano gani na uwepo wa Mungu au la?
Uhusiano wa mfano wako upo kwenye hoja inayodai sayansi kuna vitu vingi haivijui na kwamba haikupaswa iseme havipo badala yake ikubali haivijui kwasababu haiwezi kuvithibitisha havipo.

Ndipo nikakuambia kwa hoja yako hiyo hakuna kitu ambacho unaweza kudai hakipo na ndio maana nikakuwekea ule mfano
 
Hata hivyo, katika mfano wako ameandika sentensi "mama mzazi". Naamini unafahamu kwa undani maana ya sentensi hiyo. Utakuwa unajua zaidi uhalisia, kwa nini mama mzazi amekuwa na umri madogo kuliko binti yake.
Sawa sawa

Umefanya logical reasoning yenye logical consistency kubaini uongo wa hoja ambayo ina contradiction

Sayansi nayo imetumia njia hiyo hiyo kuonesha Mungu wako hayupo

Mungu huyu tumeambiwa ni omnipotent, omnibenevolent na pia ni omniscient

Omnipotent: ana nguvu ya kuzuia maovu yasiweze kutokea

omnibenevolent: ana upendo wote na mwenye utayari wa kuzuia mabaya

Omniscient: Mwenye ujuzi wote wa kuelewa ni njia gani uovu unaweza ukapenya, na mwenye kujua ni njia gani ambayo inaweza kuzuia huo uovu

Mungu mwenye kujua njia zote ambazo dhambi na maovu yanaweza yakaja kutokea, Mungu mwenye uwezo wa kuzuia hayo yote yasiwepo, mwenye kila sababu ya kufanya hivyo angezuia maovu yasiwepo.

Kama kungekua na Mungu mwenye ujuzi wote, upendo wote na muweza wa yote basi uovu usingekuwepo

Uovu upo. Hiyo inamaanisha hauwezi kuwa na vyote viwili kwa mpigo (contradiction) yani kuwepo na uovu halafu at the same time kuwe na Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na muweza wa yote

Uovu unathibitisha Mungu huyo hayupo

Kusema Mungu mwenye sifa hizo yupo inafanya kusiwe na tofauti na mtu anayesema binti wa miaka 20 ana mama yake mzazi mwenye umri wa miezi 3 wapo
 
Kwenye ulimwengu uliojaa dhiki, dhulma, fitina, kijicho, nuksi, mauaji na kila aina ya ushenzi inaonyesha Dunia ina dosari na ulimwengu kwa ujumla.
Kivipi na kila kitu hapo kina sababu. Kingine hakuna nuksi duniani hili ondoa.

Hayo yote yamepangwa yawepo katika ulimwengu si kwamba yametokea tu bahati mbaya. Ndiyo maana nataka mnipe dosari na kwanini na mmejuaje Hilo ?
 
Uhusiano wa mfano wako upo kwenye hoja inayodai sayansi kuna vitu vingi haivijui na kwamba haikupaswa iseme havipo badala yake ikubali haivijui kwasababu haiwezi kuvithibitisha havipo.

Ndipo nikakuambia kwa hoja yako hiyo hakuna kitu ambacho unaweza kudai hakipo na ndio maana nikakuwekea ule mfano
Sawa, kwa hiyo Mungu yupo.
 
Sawa, kwa hiyo Mungu yupo.
Kwa hiyo binti wa miaka 20 ambaye ana mama mzazi wa miezi 3, yupo?

Hivyo ndiyo nilivyotaka kumaanisha

Mungu wako ana contradiction kama huyo binti na mama yake
 
Kivipi na kila kitu hapo kina sababu. Kingine hakuna nuksi duniani hili ondoa.

Hayo yote yamepangwa yawepo katika ulimwengu si kwamba yametokea tu bahati mbaya. Ndiyo maana nataka mnipe dosari na kwanini na mmejuaje Hilo ?
Kapanga nani na yamepangwa na nani?
Sifa za Mungu wenu si mwenye huruma, upendo na mpenda haki?

Sasa huoni hiyo inakinzana sifa tajwa?
 
Kapanga nani na yamepangwa na nani?
Sifa za Mungu wenu si mwenye huruma, upendo na mpenda haki?

Sasa huoni hiyo inakinzana sifa tajwa?
Umenikumbusha hii meme..

Genesis 7:4 // Mwanzo 7:4

Screenshot_20230221-151615_Quora.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom