Atheists wana mtindio wa ubongo

Kifupi ni study of nature.
Hapa inazungumziwa Natural science.
 
Sijaona maswali yako ila kila kitu ni Nature.
Sayansi ndio kujifunza asili
 
Kwa hiyo binti wa miaka 20 ambaye ana mama mzazi wa miezi 3, yupo?

Hivyo ndiyo nilivyotaka kumaanisha

Mungu wako ana contradiction kama huyo binti na mama yake
Kwa hiyo unakubali kuwa kuna Mungu mwenye contradictions.
 
Kwa hiyo unakubali kuwa kuna Mungu mwenye contradictions.
Kuna dhana ya Mungu yenye contradiction

Contradiction huonesha namna jambo lisivyokuwa na uwezekano wa kuwepo kihalisia
 
Ni kweli uovu upo mwingi tu. Lakini uovu haufanywi na Mungu, bali na binadamu.

Mungu alitoa mwongozo wa kuishi bila kutenda maovu. Sisi ni kuzingatia mwongozo huo, basi. Mambo meema ya kutenda yapo mengi sana, kwa nini uchague maovu na huku unalalama ati kwa nini Mungu hakuzuii!

Sio kazi ya Mungu kuzuia matendo yako, ila utapimwa kwa matendo yako. Sio kazi ya Mungu kukuchunga kama mbuzi. Yeye anaelewa uwezo uliopewa wa kujua meema na maovu. Mungu haigilii uchaguzi wako. Ukichagua uovu, fanya kwa hasara yako.

Ulitaka Mungu akuchemshie chai ndiyo ujue kuwa anakupenda?
 
Mungu anajua mambo yajayo ila still 'anatupima'. Ili iweje sasa? Si anajua kua sitatenda mema tu anyway kwann anilete duniani?
Magonjwa na maafa mbalimbali ni mungu pia anapanga? Ni kwasababu ya maovu ya binadamu, sindio?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alieumba uovu ni nani?
 
Napata mashaka kama umesoma na kuelewa post yangu.

Kwanza ukisema mabaya yanatokana na matendo yetu, itabidi utuambie vipi kuhusu matetemeko ya huko Turkey na Syria yanasababishwa na matendo ya kina nani?
 
Napata mashaka kama umesoma na kuelewa post yangu.

Kwanza ukisema mabaya yanatokana na matendo yetu, itabidi utuambie vipi kuhusu matetemeko ya huko Turkey na Syria yanasababishwa na matendo ya kina nani?
Na tutamtaka ajue kua sayari 'Jupiter' ina vimbunga vikali sana. Kwahio atwambie hio hali mbaya inasababishwa na maovu ya nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kapanga nani na yamepangwa na nani?
Sifa za Mungu wenu si mwenye huruma, upendo na mpenda haki?

Sasa huoni hiyo inakinzana sifa tajwa?
Unarudia swali Moja mara mbili katika ibara Moja, sijui unaharakia wapi. Amepanga Allah.

Hapo umetaja baadhi ya sifa ila kadhalika ni mkali wa kuadhibu.
 
Kifupi ni study of nature.
Hapa inazungumziwa Natural science.
Kijana usiwe unajadiliana na Mimi kama huna Elimu ya haya mambo. Hakikisha unasoma vizuri ninachokiandika kuepusha kukosea na kuandika visivyo hitajika.

Maana nilizo zitoa zipo kamili na zimeweka wazi mambo.

Sasa bila shaka tumeshakubaliana ya kuwa hizo ni maana za Sayansi. Sasa nataka mniambie Sayansi imetengeneza kila kitu kivipi ? Jua likeyengenezwa vipi na Sayansi ?
 
Sijaona maswali yako ila kila kitu ni Nature.
Sayansi ndio kujifunza asili
Kote kwenye alama ya kuuliza Kuna maswali. Hujaona alama za kuuliza ? Zifatilie Kisha ujibu.
 
wewe ndio una mtindio wa ubongo wala sio wao...

nani kakwambia uumbaji alifanyaga an entity called "god"?

Where do you invent that nonsense?
 
Ukamilifu ni kutokua na matetemeko yanayouwa watu, vimbunga, mafuriko etc... cha ajabu hivi vitu haviko duniani pekee...

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo hapo mnasema haya mambo ni nature, maana yake asili inakuwaje na dosari ?

Maana yake haya mambo yanatokana pasi na chochote au yanatokea bahati mbaya ? Kinyume chake huwezi kusema ni dosari vitu ambavyo havitokei kwa bahati mbaya au pasi na chochote.

Kwahiyo Sasa ili uwe sahihi unatakiwa ututhibitishie haya yanatokea pasi na chochote na kwa bahati mbaya.
 
Haya yanatokea pasi na chochote ila bahati mbaya, haiitaji hata akili kubwa kufikiria hili... kwani kuna anaepanga mvua inyeshe au isinyeshe? Kuna anaepanga matetemeko au vimbunga? Ivo ni vitu vinatokea venyewe na ni nature...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…