Atheists wana mtindio wa ubongo

Katika yale maelezo yako mawili yanayopingana nataka nijue moja

Majibu ya maswali yangu unayo au maswali ambayo nimekuuliza ni Mungu pekee ndiye mwenye majibu hivyo wewe huwezi kujibu?
 
Utajuaje kwamba kukosa kwako majibu kunatokana na akili zako tu kukosa ufunuo na sio kwamba hicho kitu hakipo na ndio maana unakosa ufunuo ambao ungekufikisha kwenye majibu?
 
Hata dini pia inaendeshwa kwa msingi wa imani

Kwasababu wewe umesema huamini katika dini, basi naomba nianze mwanzo kabisa kwenye premise ya hoja yangu

Naomba uniambie ni nini kilikufanya mpaka ukaanza kuamini Mungu yupo?
 
Kwani Mungu wako yupo perfect kila idara?

Ana weakness yeyote ambayo inaweza ikakufanya u-doubt sifa zake?

Kwako wewe unaona ni sawa, Mungu kuwa na limited power?
 
Sijajua unasomaje ila nimekuwekea mfano hapo tena niliokuhusisha wewe

Nilikuambia kabla hujazaliwa, Mungu alijua kuwa utazaliwa?

Alijua ni lini, wapi, na mzazi gani ambaye atakuzaa?

Au hakujua?

Siku yako ya kufa anaijua?

2025 kuna uchaguzi je Mungu ashajua yatayojiri mwaka huo au naye anasubiria mpaka watu wapige kura, wahesabu na Nec watangaze ndio naye ajue?
 
Katika yale maelezo yako mawili yanayopingana nataka nijue moja

Majibu ya maswali yangu unayo au maswali ambayo nimekuuliza ni Mungu pekee ndiye mwenye majibu hivyo wewe huwezi kujibu?
Sikimbuki kama nimetoa majibu yanayopingana.

Vilevile hakuna swali ambalo sijakujibu. Una tatizo la kuelewa, na kuelewa ni jukumu lako, sio langu.
 
Utajuaje kwamba kukosa kwako majibu kunatokana na akili zako tu kukosa ufunuo na sio kwamba hicho kitu hakipo na ndio maana unakosa ufunuo ambao ungekufikisha kwenye majibu?
Kukosa jawabu hakumanishi kwamba swali halina jawabu. La hasha. Kuna maswali mengine majawabu yake hayajulikani, lakini yapo.
 
Hata dini pia inaendeshwa kwa msingi wa imani

Kwasababu wewe umesema huamini katika dini, basi naomba nianze mwanzo kabisa kwenye premise ya hoja yangu

Naomba uniambie ni nini kilikufanya mpaka ukaanza kuamini Mungu yupo?
Ni kweli dini inaendeshwa kwa msingi wa imani. Lakini Mungu alilkuwapo hata kabla ya dini.
Nilianza kuamini Mungu yupo kutokana na historia yake. Nina imani kubwa sana katika historia.
 
Kwani Mungu wako yupo perfect kila idara?

Ana weakness yeyote ambayo inaweza ikakufanya u-doubt sifa zake?

Kwako wewe unaona ni sawa, Mungu kuwa na limited power?
Maswali yako yote yamelenga niyajibu kwa niaba ya Mungu! Kwani nimekuambia mimi ni msemaji wa Mungu? Usipende kuniuliza maswali yenye majibu ya nafsi ya Mungu.
Halafu pia ni maswali yaleyale kwa namna tofauti. Sijui una maana gani!
 
Sikimbuki kama nimetoa majibu yanayopingana.

Vilevile hakuna swali ambalo sijakujibu. Una tatizo la kuelewa, na kuelewa ni jukumu lako, sio langu.
Kama hukumbuki hilo ni tatizo lako binafsi la kumbukumbu

So usije na hitimisho kuwa nina tatizo la uelewa kwenye kitu ambacho hukumbuki hata ulivyokiandika

***********

Nilikuuliza swali kuhusu ujuzi wa Mungu kama una mipaka au hauna mipaka

Ulichonijibu ni kuwa Mungu ni mjuzi wa uumbaji (irrelevant to my question)

Kisha ukaja kujikanusha kuwa jibu la swali hilo anayejua ni Mungu

Sasa nashindwa kuelewa katika hizo statement mbili niichukue ipi na niiache ipi, ndio maana nikakuuliza "Majibu ya maswali yangu unayo au maswali ambayo nimekuuliza ni Mungu pekee ndiye mwenye majibu hivyo wewe huwezi kujibu?"
 
Ni maswali yanayohusu uumbaji wa Mungu na tabia tabia za binadamu.
Kuhusu uumbaji, naamini Mungu anajua kila kitu.
Yanayohusu tabia, Mungu alitupa dira na mwelekeo tukitumia akili zetu.
 
Kukosa jawabu hakumanishi kwamba swali halina jawabu. La hasha. Kuna maswali mengine majawabu yake hayajulikani, lakini yapo.
Ndio maana nimekuuliza, utajuaje kukosa kwako majibu kunatokana na wewe kukosa majibu na sio kwamba unakosa majibu kwasababu uhalisia wa hicho kitu haupo?
 
Ni kweli dini inaendeshwa kwa msingi wa imani. Lakini Mungu alilkuwapo hata kabla ya dini.
Nilianza kuamini Mungu yupo kutokana na historia yake. Nina imani kubwa sana katika historia.
Historia yake kutoka wapi?
 
Maswali yako yote yamelenga niyajibu kwa niaba ya Mungu! Kwani nimekuambia mimi ni msemaji wa Mungu? Usipende kuniuliza maswali yenye majibu ya nafsi ya Mungu.
Halafu pia ni maswali yaleyale kwa namna tofauti. Sijui una maana gani!
Ni kwasababu hata wewe unamuelezea Mungu kwa niaba yake

Kwa niaba yake umeamua kumsemea kuwa yeye ni mjuzi wa uumbaji

Kama unakataa kujibu maswali ya msingi kwasababu ya kudai "ni kwa niaba ya Mungu" basi kanusha madai yako yote uliyoyasema mwanzo ukimuelezea Mungu, kubali kuwa ni ya UONGO ili kweli isionekane kuwa unaongea kwa niaba yake.

Vinginevyo.....

Nilikuambia kabla hujazaliwa, Mungu alijua kuwa utazaliwa?

Alijua ni lini, wapi, na mzazi gani ambaye atakuzaa?

Au hakujua?

Siku yako ya kufa anaijua?

2025 kuna uchaguzi je Mungu ashajua yatayojiri mwaka huo au naye anasubiria mpaka watu wapige kura, wahesabu na Nec watangaze ndio naye ajue?
 
Ni maswali yanayohusu uumbaji wa Mungu na tabia tabia za binadamu.
Kuhusu uumbaji, naamini Mungu anajua kila kitu.
Yanayohusu tabia, Mungu alitupa dira na mwelekeo tukitumia akili zetu.
Okay kumbe saizi ni simple kutoa jibu kwa niaba ya Mungu?

Halafu sijajua kwanini unajitangulizia mpira kwa mbele kama Twisila

Kwasababu hakuna sehemu nimetaja mambo ya tabia wala uumbaji kwenye hoja yangu.

Kama Mungu ni mjuzi wa kila kitu, na aliona kila kitu kitachoenda kutokea kwenye ulimwengu atakaokwenda kuumba, ikiwemo mabaya, kwanini pamoja na kulijua hilo kuumba ulimwengu usioweza kuruhusu uovu?
 
Maswali yako yote yamelenga niyajibu kwa niaba ya Mungu! Kwani nimekuambia mimi ni msemaji wa Mungu? Usipende kuniuliza maswali yenye majibu ya nafsi ya Mungu.
Halafu pia ni maswali yaleyale kwa namna tofauti. Sijui una maana gani!
Itoshe kusema pumzika sasa, hoja zako zote tokea mwanzo umezizimia hapa. Kwisha habari yako
 
Teknologia yote unayoitumia ni kazi ya Atheists, kweli wana mtindio wa ubongo? Hapo umesema kinyume. Do you understand in order to believe or you believe in order to understand?
Si kweli hata kidogo kuwa technology yote ni kazi ya atheist! Hapo umetudanganya! Rudi shule, soma historia za wana'science na teknolojia' wacha Mungu waanzilishi wa hiyo unayoiita technology achana na hawa wahuni waliodandia train kwa mbele!
 
Einstein, Galileo, Isaac Newton. Hawa walikua hawaamini japokua walizaliwa katika misingi ya dini. Na hawa watu wamesaidia kwa kiwango kikubwa sana ktk kukuza technologia iliopo mpaka leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutokumbuka ni jambo la kisayansi na lina umhimu wake pia.
Uliniuliza mipaka ya ujuzi wa Mungu. Hujawa specific ni ujuzi wa nini. Lakini nilikujibu specifically, Mungu ni mjuzi wa uumbaji wa viumbe vyote.

Pia nilikujibujibu swali hilo anayejua ni Mungu kwa sababu hukuridhika na specific answer. Ulitaka general answer ambalo mimi silijui.

Kwa hiyo, kuna maswali najua majibu yake na mengine sijui, kwa kuwa ni ya nafsi ya Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…