Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,929
Salaamu wakuu.
Niende Moja kwa moja kwenye mada.
Utakuta mtu anasifia gari ; "Hii gari kiboko kweli mainjinia wake walikuna vichwa balaa katika usanifu na gari hii haina mpinzani kwani katika kila nyanja ipo okay", ilmuradi tu gari litasifiwa hata kama linazo kasoro na mapungufu fulani.
Hao hao ma atheists utawasikia tena wakisifia; "Hii computer achana nayo, inakasi kubwa balaa utadhani haikundwa na.binadamu bali imedondoka kutoka mbinguni".
Ma atheists hawaishi hapo tu, hebu wakaribishe kwenye pilau utawasikia; "Aise huu msosi kiboko, mtamu kweli, sijui kapika nani !!? Mpishi katoka wapi??!, pasi shaka umepikwa na mtu kutoka pwani kwani watu wa bara hawawezi mapishi ya aina hii !! ".
Huyo atheist anatoa madai kana kwamba huyo mpishi anamjua na kamuona!!, sasa kwa utani tu jaribu kumwaambia kwamba msosi huo umejipika wenyewe!!, utashambuliwa kwa kejeli na matusi na kupewa majina mabaya ya kukutoa akili, utawasikia wakisema; wewe unamatatizo kichwani mwako inawezekanaje chakula kijipike chenyewe??!!.
Sasa njoo kwenye uumbaji wa dunia na uwaulize; je hawaoni uzuri wa dunia na vilivyopo juu yake, navyo havijaumbwa??, hakuna nafsi iliyoumba dunia.na ulimwengu??, endelea kuwahoji; kama wapo Ma engineers waliounda lile gari, ile computer na yupo mpishi aliyepika lile pilau safi vipi akosekane Yule aliyeumba dunia safi na vilivyomo??--- hapo akili zao zinashikwa na wazimu kwani wanajua ni lazima Mungu atajwe katika uumbaji wa dunia na vilivyomo na wao kusikia jina "Mungu" kwao ni ugonjwa wa mzio (allergy), sasa watakuuliza; Huyo Mungu yuko wapi??!, ukiwajibu; Mungu huwa haonekani, waona wamepata silaha, watahoji; tutaaminije kitu kisichoonekana ndio kimeumba hii dunia??-- wanasahau kwamba hata ile pilau waliokula hawakumuona mpishi wake lakini wanaamini ilipikwa na mtu-mpishi lakini wakiambiwa Kuna muumba, Mungu wa dunia na ulimwengu hawataki kusikia.
Ewe Mungu wasamehe hawa viumbe wako na uwaongoze katika njia zako na uwaondoshee kibri na majivuno.