Atheists wana mtindio wa ubongo

Atheists wana mtindio wa ubongo

Haya tuambie wewe kama sio mvua inaitwa nini?

Ili utengeneze binadamu basi kupitia Cloning na anakuwa binadamu aliye kamilika.

Nao sio binadamu?
Maana ya mvua inajulikana kijana, hiyo waulize wenyewe wakwambie ni nini na kama wamenipa jina Mvua nasi wanajidanganya wao wenyewe. Na kuwadanganya wenzao.

Mwanadamu hatengenezwi kijana, muwe mnajifunza lugha na usahihi wa maneno, kisichokuwa na roho ndiyo kinatengenezwa, mwanadamu anaumbwa na mwenye kuumba ni Mola pekee.
 
Hiyo haiitwi mvua, ni sawa na sanamu la Sophia ukasema yule ni Mwanadamu. Muwe mnafikiria haya mambo kiundani siyo juu juu tu, kama mnavyo fanya nyinyi mnafikiri hii ni Falsafa, au Logic au Sayansi ukiamka tu unafikiria kitu Kisha mnaleta Assumptions kibao. Kwenye dini hakuna huo upuuzi, kwenye dini ni uhalisia tu.

Kingine akili ya mwanadamu Ina ukomo na kutojua kutowezekana kwa mambo Fulani huo ni wendawazimu mwingine, kwahiyo hao Wachina ni mazuzu wasio jua asili ya mvua, kama wale wanaotafuta dawa ya Kifo, huku hawajui hakika ya kifo na kwanini Kuna kifo, huu ni uzwa uzwa mwingine.

"Kingine akili ya binadamu ina ukomo na kutojua..."

Nyie wenyewe ndio mnajilimit, mnajipa ukomo wenyewe. Sasa hio kama sio mvua ni nn? Maana wamefanya utafiti kua mvua inatengenezekaje afu kisha wakafanya ivoivo ili kutengeneza mvua na inanyesha... haina utofaut na mvua za kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maana ya mvua inajulikana kijana, hiyo waulize wenyewe wakwambie ni nini na kama wamenipa jina Mvua nasi wanajidanganya wao wenyewe. Na kuwadanganya wenzao.

Mwanadamu hatengenezwi kijana, muwe mnajifunza lugha na usahihi wa maneno, kisichokuwa na roho ndiyo kinatengenezwa, mwanadamu anaumbwa na mwenye kuumba ni Mola pekee.
Ni kwamba, mamilioni ya matone ya maji yanapojikusanya nakutengeneza mawingu kisha yakadondoka hio ndio mvua. Na tunajua kabisa namna haya matone yanavojikusanya na kuleta mvua. Na tunaweza kuzuia lisifanyike hilo na mvua isinyeshe, na tunaweza kuspeed up hio process ili kupata mvua nyingi zaid. Hakuna kitu anafanya Allah hapo. Saudi Arabia mbona wao hawaruhusu dini iwafanye kua wajinga hivi, wakat huko ndio kati ya sehem uislam ulipoanzia...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya umeyapata wapi ? Ndiyo nasikia kwako, naomba unionyeshe umepata wapi hizi habari.

Hili lishajadiliwa zaidi ya mara Moja humu ndani. Shida yenu hampo kwa ajili ya kujifunza zaidi ya ubishani, ndiyo maana mnakuwa wajinga na wavivu wa kufikiri. Kitu msichokijua Qur'aan Ina aya nyingi za kuwahimiza watu wafikiri na kutafakari. Ukiona huilewi Qur'aan ujue wewe huzingatii na hufikiri kiundani kile kinachosemwa.

Hayo niliyo kuuliza umeyapata wapi siyajui mengine nakubaliano nayo. Sasa ni wajibu wako uniambie umeyapata wapi.
Kuangamiza dunia nzima kwa mvua: Quran Ayah 11:40

Kugawa mwezi katikati: surah al-qamar 54:1-na kuendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
It's by chance/ randomnesss

Hatuchagui wazazi ila pia wazazi hawatuchagui.

The universal law ndio inayo govern kila kitu kwenye huu ulimwengu.

Ni vinasaba utakavyorithi toka kwa watu wawili walipokutana in randomness ila wakaamua kuzagamuana ndio ukatokea kenge wewe.

Ila kiukweli ulimwengu ni chaotic kama alivyosugest mdau.

Ni Binadamu tu ndiye anaweza kuwa chaotic or disciplined na sio vitu vingine ambavyo ni governed by natural laws, Who then put the laws into play??-- that is the question you need to ask yourself.

Angalia, thermal nuclear Bomb katika intermediate stage kuna Hydrogen gas inalipuliwa na neutrons kutoka kwenye stage ya kwanza ( atomic bomb), hiyo hdrogen gas ina ji-fuse (fussion reaction) kutengeneza Helium gas ambapo joto kubwa sana na nuru pamoja na radiations hutolewa, mambo yote hayo yanatokea kwakuwa yamepangwa kitaalamu na nuclear scientists, tunaweza kusema ni; a conscious plan of conscious minded people to make a disciplinary machine in order to excute a desired purpose/ goal, sasa muundo huo huo wa stage hiyo ya thermonuclear bomb ndio muundo unaofanyika kwenye jua, Jua ni fussion reaction ya Hydrogen gas kuwa Helium gas, hiyo ni Nuclear reaction ndio maana tunapata the desired goals ya joto na mwanga wa jua hapa duniani, sasa kama huwezi kusema hiyo reaction katika thermonuclear bomb ni Chaotic utawezaje kusema the fussion reaction katika jua kitu ni chaotic?? ,Kama jambo limepangwa na wanasayansi kitaalamu lifanye kazi kusudiwa in disciplines tunaliita a disciplined thimg bila shaka mtu mwenye akili chaotic ndiye anayeweza kusema jua ni chaotic reaction ya hydrogen. ,

Kumbuka jua limekuwepo hata kabla ya sayansi ya nuclear na sayansi zingine kuwepoo na ndio maana nasema jua ni lazima limeumbwa na A conscious Supernatural being ili jua litende the non chaotic desired goals ambazo naamini unazijua, na ipo mifano hai lukuki ya non chaotic objects with desired goals ambazo ni mtu kichaa tu aliyejitoa akili atapinga kwamba hizo Objects hazikuumbwa.

Kumbuka ni binadamu ndiye ameumbwa ama achague chaotic au disciplined life na sio vitu vingine ambavyo uwepo wao ni governed by natural laws or instincts put in place by Supernatural Being namely God.
 
"Kingine akili ya binadamu ina ukomo na kutojua..."

Nyie wenyewe ndio mnajilimit, mnajipa ukomo wenyewe. Sasa hio kama sio mvua ni nn? Maana wamefanya utafiti kua mvua inatengenezekaje afu kisha wakafanya ivoivo ili kutengeneza mvua na inanyesha... haina utofaut na mvua za kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulijia kama Uturuki kutatokea Tetemeko la ardhi ? Au unaijua kesho yako ? Ukitaka kujua ukomo wa akili ya mwanadamu waangalie Wanasayansi wanavyofikia hitimisho katika mambo Yao. Ushawahi kujiuliza kwanini kwenye Sayansi au Scientific Calculation zina "Assumptions". Kwanini kwenye Projectile Motion Calculation Kuna Assumptions, kwenye Universal Law Of Gravitational Kuna Assumption, kwenye Thermodynamics na kwingine ? Maana yake akili imekomea pale.

Sisi hatujilimit bali hayo ni maumbile ili kuepuka uongo na kidanganya watu.
 
Ni kwamba, mamilioni ya matone ya maji yanapojikusanya nakutengeneza mawingu kisha yakadondoka hio ndio mvua. Na tunajua kabisa namna haya matone yanavojikusanya na kuleta mvua. Na tunaweza kuzuia lisifanyike hilo na mvua isinyeshe, na tunaweza kuspeed up hio process ili kupata mvua nyingi zaid. Hakuna kitu anafanya Allah hapo. Saudi Arabia mbona wao hawaruhusu dini iwafanye kua wajinga hivi, wakat huko ndio kati ya sehem uislam ulipoanzia...

Sent using Jamii Forums mobile app
Mawingu ya asili na haya ya kutengeneza Yana usawa kiasi gani ?

Ukiona unaweza kuzuia mvua ujue hiyo siyo mvua.
 
Kuangamiza dunia nzima kwa mvua: Quran Ayah 11:40

Kugawa mwezi katikati: surah al-qamar 54:1-na kuendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa soma katika aya Kisha urudi katika yale uliyo yaandika uniambie Yana fanana ? Wewe ulisema Mtume alishika huo mwezi. Sasa huu mtindo ndiyo nitakuwa napenda nao Sasa hivi, yaani nawaachia mjielezee ili mzidi kuonekana mlivyo waongo na msio fatilia mambo. Yaani mnafanya khiyana mpaka kwenye kunukuu habari.

Sasa nakupa kazi nenda kafute ule uongo ulio uandika.
 
Sasa kama hujachukua ushahidi utaaminikaje kuwa ni mkweli?

Ni kweli una miliki nyumba, ila umeenda benki bila hati ya nyumba ukasema uombe mkopo wa milion 100.

Unafikiri utaweza kuaminiwa kuwa umesahau hati nyumbani hivyo wakupe mkopo?

Hiyo inamaanisha kwamba tukiruhusu hilo swala, tunakuwa tumeachia mwanya kwa madai yeyote ya uwongo as long as kila mmoja atakuja na viapo kuwa hicho kitu ni kweli
Hiyo nyumba unakuwa nayo au hauna..? So why mlazimishe lazima kuwepo kwa kitu kuweze kuthibitika...? Na uwepo wa Mungu hauhitajiki kuthibitika kwa vigezo vya kibinadamu imani inayotokana na vitu visivyo na majibu kama chanzo binadamu na uhai, na vitu vingine kama jua na hiyo science mnayosoma function zake bila kujua chanzo. Mfano unaweza niamboa chanzo/asili ya jua ni nini...!
 
Kama imani ni njia ya kweli kujua ukweli wa jambo basi tungekuwa na imani moja yenye kuamini Mungu mmoja

Since tuna bunch of faith tena zinazo pingana basi hoja ya kusema Mungu yupo kwa imani haiwezi kuwa na mashiko
Kila imani ina chanzo/asili yake na ukiifuatilia vyema utagundua Mungu au mungu(muungu) anayezungumziwa katika imani hiyo anathibitika. Sisi watu wa monotheism (single and only One God) tunaamini katika Mungu mmoja ambaye ni chimbuko la kila kitu, ata hiyo miungu.

Imani si lazima iwe ni kuhusu Mungu tu, hujawahi ambiwa na mtu au wewe kumwambia huna imani na naye..?? Kuwa au kukosa matarajio ya kitu kwake..? Sasa Mungu wetu tunao amini si lazima awe tangible (physical) ndipo awe Mungu ata katika hali ambayo hana umbo (intangible) still ni Mungu wetu maana katika imani (matarajio) tunaamini kupokea aliyotuahidi.
 
Hiyo nyumba unakuwa nayo au hauna..? So why mlazimishe lazima kuwepo kwa kitu kuweze kuthibitika...? Na uwepo wa Mungu hauhitajiki kuthibitika kwa vigezo vya kibinadamu imani inayotokana na vitu visivyo na majibu kama chanzo binadamu na uhai, na vitu vingine kama jua na hiyo science mnayosoma function zake bila kujua chanzo. Mfano unaweza niamboa chanzo/asili ya jua ni nini...!
Umesahau kwamba hata kitu ambacho hakipo nacho hakiwezi kuthibitishwa kuwa kipo

Sasa ukaletewa madai ya kitu ambacho hakipo, we utajuaje kuwa hiki kitu hakipo au kipo ila kimekosa uthibitisho wa kuonesha kipo?

Utaamua vipi kwenye jambo hilo?

Ukisema kitu fulani kipo bila ushahidi au uthibitisho, hayo yanakuwa madai

Madai sio ushahidi

***********†**************

Nimekuambia imani ingekuwa njia ya kweli ya kujua ukweli wa jambo basi kila kitu kilichodaiwa kuwa ni imani kingekuwa kweli

Na mind you, tungekuwa na imani moja kwasababu wote ingetulengesha kwenye jibu moja.

Uwepo wa imani nyingi tofauti tofauti na zenye kupingana kunaonesha imani sio njia ya kweli kwenye kujua ukweli wa jambo.
 
Kilicho beyond your grasp, we umekijuaje?

Umejuaje kama amewapa watu neema ya kujua wakati ujuzi wako upo limited kuweza kumuelewa?
Just because of His Graceful, sababu anaweza yasiyowezekana kwa akili zetu, ameweza kutuwezesha kuyafahamu yaliyo nje ya uwezo wa uelewa wetu kwa jinsi apendavyo na aonavyo inafaa si kadri ya mapenzi yatu.

Reason: He is reasoningless, his mind is incomperable.
 
Kila imani ina chanzo/asili yake na ukiifuatilia vyema utagundua Mungu au mungu(muungu) anayezungumziwa katika imani hiyo anathibitika. Sisi watu wa monotheism (single and only One God) tunaamini katika Mungu mmoja ambaye ni chimbuko la kila kitu, ata hiyo miungu.
.
Kwa hiyo kumbe imani nayo inatatizo inaweza ikakufikisha kwenye jibu la uongo?

Halafu sio kweli kuwa imani za Miungu tifauti na imani yako zinaabudu Mungu anayethibitishika.

Dini ya Summerian ni kongwe kuliko hata hiyo dini yako, na imekuwa ikiabudu Enlil ambaye ni unseen

Na ukija katika hoja yako kuwa miungu inaabudu Mungu zaidi ya mmoja bado utafungwa na kauli yako kwa wakristo ambao wanaabudu Mungu katika utatu

**********************†******************

Mnao amini Mungu katika umoja mko wangapi?
 
Just because of His Graceful, sababu anaweza yasiyowezekana kwa akili zetu, ameweza kutuwezesha kuyafahamu yaliyo nje ya uwezo wa uelewa wetu kwa jinsi apendavyo na aonavyo inafaa si kadri ya mapenzi yatu.

Reason: He is reasoningless, his mind is incomperable.
Umejuaje kuwa sababu ni neema yake wakati hata uwezo wa kuthibitisha huna?

Umetumia nini kujua ilihali uelewa wako uko limited?

Hayo yote kuhusu nje ya uwezo wa uelewa wenu, umetumia kitu gani kuyajua?

Unaweza ukajibu hayo maswali bila kutumia circular reasoning?
 
Umesahau kwamba hata kitu ambacho hakipo nacho hakiwezi kuthibitishwa kuwa kipo

Sasa ukaletewa madai ya kitu ambacho hakipo, we utajuaje kuwa hiki kitu hakipo au kipo ila kimekosa uthibitisho wa kuonesha kipo?

Utaamua vipi kwenye jambo hilo?

Ukisema kitu fulani kipo bila ushahidi au uthibitisho, hayo yanakuwa madai

Madai sio ushahidi

***********†**************

Nimekuambia imani ingekuwa njia ya kweli ya kujua ukweli wa jambo basi kila kitu kilichodaiwa kuwa ni imani kingekuwa kweli

Na mind you, tungekuwa na imani moja kwasababu wote ingetulengesha kwenye jibu moja.

Uwepo wa imani nyingi tofauti tofauti na zenye kupingana kunaonesha imani sio njia ya kweli kwenye kujua ukweli wa jambo.
Unaleta reasoning ya logic, syllogism ina makosa makubwa mno..! Huwezi draw conclusion kwa logic siyo kila kitu kinafuata huo mtririko wako wa logic.

Umeenda bank kukopa ukiwa na nyumba ila umesahau hati, hukupewa mkopo sababu hukutoa ushahidi wa nyumba ila haimanishi huna nyumba.

Chukua hii mifano miwili

Binadamu wote lazima wanakufa.
John ni binadamu hivyo John atakufa.

Mbwa wanatumika katika ulinzi.
Wamasai wanatumika katika ulinzi.
Kwahiyo wamasai nao ni mbwa...?

UKWELI siyo lasima uthibitike kwa logic kama unavyotaka, Imani ya Kikristo ambayo ni moja kati ya imani katika kundi la Monotheism (believers in one God) wao uthibitisho wa Mungu wao hauthibitiki kwa logic tu kuna msururu wa vitu katika kutaka kuthibitisha hilo.

Kuna matukio ambayo historia inathibitisha kutokea kwake, mfano uwepo wa mtu aliyezaliwa kimuujiza na kuishi duniani kwa miaka 33. Si muda mrefu sana only 2023 yrs ago. Lakini pia kuna archeological and historical facts nyingi mno zinazoelezea taarifa zinazoelezea habari za MUNGU. Make nyingine utasema ni miujiza ya uongo.
 
Kwa hiyo kumbe imani nayo inatatizo inaweza ikakufikisha kwenye jibu la uongo?

Halafu sio kweli kuwa imani za Miungu tifauti na imani yako zinaabudu Mungu anayethibitishika.

Dini ya Summerian ni kongwe kuliko hata hiyo dini yako, na imekuwa ikiabudu Enlil ambaye ni unseen

Na ukija katika hoja yako kuwa miungu inaabudu Mungu zaidi ya mmoja bado utafungwa na kauli yako kwa wakristo ambao wanaabudu Mungu katika utatu

**********************†******************

Mnao amini Mungu katika umoja mko wangapi?
Sijasema kuhusu kukufikisha kwenye uongo, Mungu anayeongelewa ni True God (Mungu mmoja). Imani usichanye zipo imani nyingi. Imani ya Mungu mmoja inajipambanua vyema.
 
Umejuaje kuwa sababu ni neema yake wakati hata uwezo wa kuthibitisha huna?

Umetumia nini kujua ilihali uelewa wako uko limited?

Hayo yote kuhusu nje ya uwezo wa uelewa wenu, umetumia kitu gani kuyajua?

Unaweza ukajibu hayo maswali bila kutumia circular reasoning?
Unadhani haya nayo yasema na kuandika nimepata shuleni..? Najua kwa kuwa tofauti na wewe, na hakika si kwa uwezo wala utashi wangu maana najibu si kwa ufahamu wangu pekee .
 
Maana ya mvua inajulikana kijana, hiyo waulize wenyewe wakwambie ni nini na kama wamenipa jina Mvua nasi wanajidanganya wao wenyewe. Na kuwadanganya wenzao.

Mwanadamu hatengenezwi kijana, muwe mnajifunza lugha na usahihi wa maneno, kisichokuwa na roho ndiyo kinatengenezwa, mwanadamu anaumbwa na mwenye kuumba ni Mola pekee.
Ukisema inajulikana basi unaikataa kwa vigezo Gani kuwa hiyo sio mvua?
Ndiyo nikakuuliza utupe maana ya mvua?

Hakuna roho kwenye mwili wa binadamu.
Human Cloning unaifahamu?

Base yote ya Maisha ulimwengu ni Carbon, hata binadamu ni carbon based living organisms.
 
Back
Top Bottom