Atheists wana mtindio wa ubongo

Atheists wana mtindio wa ubongo

Kwa uandishi wako nimegundua mambo kadhaa, ikiwemo: kiwango chako cha uelewa wa dini na elimu ni kidogo, huna uvumilivu na imani za watu wengine. Ukiaminicho wewe una ona ndio kiwe kwa wote.
 
Mkuu mi kama atheist nashukuru kwa busara yako kwa namna ulivyoamua kutuita

Ila ulichosahau ni kitu kimoja

Watu wanasifia magari, Pc nk kutokana na comparison walizofanya za kuangalia ufanisi wa bidhaa moja dhidi ya bidhaa nyingine.

Hao atheist wanaosifia magari, computer nk, wanafanya hivyo kwa references.

Kwamba watu wanasema hii bidhaa ni bora kwasababu kuna specs hii ambayo kwenye bidhaa hii nyingine haipo

Viwanda vinavyotengeneza hizo bidhaa vinathibitishika kuwa vipo bila kuhitaji kitu kingine cha ziada kama ishara ya kuonesha ndio source ya hizo bidhaa

Huyo mtu hawezi kushindwa kukuthibitishia kampuni la Dell au Hp kuwa lipo.

Ni maswala ya taaluma ambayo kila mtu anaweza akafanya endapo akifundishwa.

Sasa

Unaposema huu ulimwengu umesababishwa na Mungu, references yako inakuwa nini?

Tunaweza tukathibitisha hicho chanzo bila kutumia kitu kingine kinachopimika kuwa ndio uthibitisho wa Mungu asiyepimika?

Lakini pia

Unaposema huu ulimwengu ni bora au umekamilika unakuwa umeupima na kuufananisha na ulimwengu gani mwingine mpaka ukafikia hitimisho kuwa ulimwengu huu ni mzuri?

Aliyesema laptop Hp omen ya gaming ni bora aliangalia toleo la chini yake au alifananiaha na brand nyingine kwenye maswala ya kiuwezo akaona Hp Omen ni laptop bora

Sasa ulimwengu huu mnaosema ni mzuri au ni bora, ni bora ukiufananisha na ulimwengu upi?
Kuna msemo: usibishane na mpumbavu....
 
Uwepo wa Mungu ni jambo la kihistoria, na historia daima haiongopi. Mungu yupo.
Nani kakwambia history haidanganyi? Hadi imekuwa history maana yake imepita kwenye mikono kadhaa hadi kukufikia wewe na kuendelea. Na kawaida ya history ni lazima iongezwe ama ipunguzwe details.. hiyo ndio sifa ya fasihi.
 
Umesema anayejua ni Mungu

Umejuaje kama anajua?

Unamsemea?
Nilisema hivyo kwa maana ya kuwa muulize Mungu ndiye atakayekujibu. Ni kwa sababu maswali yalikuya ya nafsi ya Mungu na pia nilikuwa sina ufahamu nayo. Kwa hiyo simsemei Mungu.
 
Mtu ambaye amekuambia habari za uongo kwa lengo la kupotosha halafu ukamuuliza maswali ili ku prove habari yake kuwa ni ya kweli au la

Yale maswali akashindwa kuyajibu, we utajuaje kuwa habari hiyo ni uongo au ni ya ukweli ila hana majibu?
Unapohitimisha kuwa ni habari za uongo, utakuwa tayari umethibitisha kuwa ni za uongo. Kuna haja ya kuuliza tena habari za uongo kutoka kwa mtu muongo?
 
Kuna mahali uliniuliza kuhusu twisila? Wapi nimelitoa?

Hukuuliza kwasababu ulielewa

Kuhusu historia nimeshakuambia kuwa hicho ni kitu kipya, kwasababu awali nilikuuliza kuhusu dini ukasema hukubaliani.

Lengo lilikuwa nikujua wapi umepatia hiyo idea ya Mungu

Uliposema historia, lazima uniambie umeitolea wapi ili tuweze kuipima..

Niambie hiyo historia umeitolea wapi?
Usinitie maneno kinywani. Mimi sikusema sikubaliani na dini, bali nilisema siabudu dini.

Wazo la Mungu nimelipata kutoka kwa wahenga wetu na hiyo historia nimeipata kwa wahenga.
 
Wahenga ukimaanisha wazee au una maana yako nyingine?

Wahenga ndio waliotengeneza hiyo historia? au ilikuwaje mpaka hiyo historia wakawa nayo?
Wahenga namanisha kama wahenga, sina maana yangu nyingine.

Historia haitengenezwi na watu, bali huhifadhiwa na watu. Soma historia ili ujue inavyopatikana.
 
Mwingine akija akasema Mungu hayupo, na hiyo ni historia na kwakua historia haisemi uongo hivyo itathibitisha kuwa hayupo?
Historia haijipingi pia haiongopi. Historia ni kumbukumbu za matukio ya kweli. Nje na hapo, haitakua historia, itakuwa ni kitu kingine.
 
Nilisema hivyo kwa maana ya kuwa muulize Mungu ndiye atakayekujibu. Ni kwa sababu maswali yalikuya ya nafsi ya Mungu na pia nilikuwa sina ufahamu nayo. Kwa hiyo simsemei Mungu.
Sijauliza kuhusu nafsi, nimeuliza kuhusu ujuzi wa Mungu

Hapa nafanya mjadala na wewe sio Mungu, na wewe ndio uliyeleta habari za Mungu. Kwa hiyo kila swali hapa kuhusu Mungu litakuwa ni jukumu lako kujibu.
 
Historia haijipingi pia haiongopi. Historia ni kumbukumbu za matukio ya kweli. Nje na hapo, haitakua historia, itakuwa ni kitu kingine.
Akitokea mtu akaja na madai yanayopinga hoja zako kuonesha ulichokiongea ni uongo halafu naye akasisitiza kuwa madai yake ni historia, hiyo itaonesha ni kweli wewe mi muongo?
 
Wahenga namanisha kama wahenga, sina maana yangu nyingine.

Historia haitengenezwi na watu, bali huhifadhiwa na watu. Soma historia ili ujue inavyopatikana.
Nipe maana ya wahenga

Unapima vipi kujua historia hii ni kweli na sio manipulation?
 
Usinitie maneno kinywani. Mimi sikusema sikubaliani na dini, bali nilisema siabudu dini.

Wazo la Mungu nimelipata kutoka kwa wahenga wetu na hiyo historia nimeipata kwa wahenga.
Kwa hiyo unakubaliana na dini gani?

Bado hujatoa maana kuhusu wahenga
 
Sijauliza kuhusu nafsi, nimeuliza kuhusu ujuzi wa Mungu

Hapa nafanya mjadala na wewe sio Mungu, na wewe ndio uliyeleta habari za Mungu. Kwa hiyo kila swali hapa kuhusu Mungu litakuwa ni jukumu lako kujibu.
Huwezi kuuliza ujuzi wa Mungu bila kumgusa Mungu mwanyewe na nafsi yake.

Ni kweli unafanya mjadala na mimi, lakini ni mjadala juu ya Mungu.

Kuleta habari za Mungu hakumaanishi niko nafsi ya Mungu.

Kukuambia Mungu ndiye anayejua jibu la swali lako, pia ni jibu.
 
Back
Top Bottom