Athlete Crown sio gari la kubishana nalo ukiwa barabarani acha liende

Hivi huwa mnawahi nini?

Nakumbuka Julius Malema alikuwa na kesi yake baada ya kudakwa akiwa 215km/h Highway ndani ya BMW yake!
 
Wahusika hawana mipango vizuri. Barabara kuu ya kwenda mikoani kwanza ilikuwa uruhusiwe kusukuma tu ata 150km/hr, afu mambo ya uwepo wa vijiji kila baada ya kilomita sifuri yasiwepo watu tusipoteze mda barabarani!
Hahahaha!!!
Madereva wa mabasi wataua Sana watu
 
Mk Mkuu hizi ni fedhea,Crown inakuaje suzuki carry aisee.
 
Hivi huwa mnawahi nini?

Nakumbuka Julius Malema alikuwa na kesi yake baada ya kudakwa akiwa 215km/h Highway ndani ya BMW yake!
Uchizi wa madereva wote tuko hivyo hata uwe mtakatifu kiasi gani ukishaanza Safari ndefu Tu huwezi kutembea kama upo kariakoo-mwenge..
Inafika kipindi Ile speed 50 unaona kama unaendesha baiskel
 
Hahahaha!!!
Madereva wa mabasi wataua Sana watu
Ilikuwa zijengwe highways kama za mbeleni uko. Njia ya kwenda mkoani saivi ni moja tuna share wanaokwenda na kurudi, lazima ajali zisiishe πŸ˜€ Afu madereva wetu uzembe umezidi, ata ukiwaambia watembee 1km/hr watasababisha ajali.

Jana kuna daladala yaani imeforce ku overtake gari nikajikuta nipo nae uso kwa uso ikabidi gari niitoe barabarani. Niliomba kwa Mungu anipe FUSO mie, madereva kama hawa nawapelekea makusudi tu πŸ˜€
 
Au angalau DAR-moro kuwe na barabara mbili itasaidia kupunguza ajali za kizembe.
Huo mfano ambayo umetoa ni Ile ya uzembe Kwa madereva hasa wa malori
 
Mk
Mkuu hizi ni fedhea,Crown inakuaje suzuki carry aisee.
Unajua kuna watu wanajisemea mambo tu.

Ameona Speedometer inasema 240 na nyengine 180 basi anaona kuwa ya 240 iko fasta. Crown inavuka 180, hii michoro tu ujue unaendaje. Chukua gari yoyote ya Uingereza mfano tuseme Toyota avensis utaona kuwa ina 240km/hr ila toyota avensis hio hio lakini kutoka Japan utakuta ina 180 na engine sawasawa.
 
Wahusika hawana mipango vizuri. Barabara kuu ya kwenda mikoani kwanza ilikuwa uruhusiwe kusukuma tu ata 150km/hr, afu mambo ya uwepo wa vijiji kila baada ya kilomita sifuri yasiwepo watu tusipoteze mda barabarani!
Mbaya zaidi vijiji vyenyewe havijasajiliwa ni wale wakimbia mji.Barabara ya segera chalinze ndio vimejaa viingi halafu vibao vinaanzia nyuma sana ni kama vile mtaji wa trafick kwenye hivi vibao,
Napendekeza spidi limit iwe 80Km/h kwa vijiji na 30 Km/h kwa mashule.
 
Umeona mbali Sana aisee kama ningekuwa mbunge ningepeleka bungeni bill ili ipitiwe na wabunge, kwasabb kila baada ya miaka 2 vijiji vinaongezeka na mwisho wa siku inakuwa usumbufu Tu wa kutembea chini ya 50 mwanzomwisho
 
Eeh athlete ukiifanyia mapping inafika 260km/h sababu Lexus sedans zenye engine hio hio ya 4GR-FSE zinafika hio speed! Ndio maana Crown kufika 180kph ni ndani ya sekunde 30 tu very smoothly.
 
Sasa kama Crown si imetiwa disc brakes mbele na nyuma sababu ya fast stop! Haina drum kama sedan za bei rahisi.
 
nyingi nchini ni 12generation ambazo hazina engine yoyote yenye code JZ


UNA UHAKIKA? je nikikuonesha yenye 1/2JZ utacngizia nini?
Crown generation ya sasa nyingi ni chassisi no. inaanza na code ya engine GRS meaning GR engine!

Zile za zamani ni JZX meaning zina JZ engine. Mark 2 zenyewe ni GRX meaning zina 1G engine.
 
Mile 120 ni nyingi mkuu almost kilometre 200! Sasa mizunguko ya siku nzima unamaliza hizo km kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…