Athlete Crown sio gari la kubishana nalo ukiwa barabarani acha liende

Na ndiyo maana wengi wanalia lia...kisa class mate wake kanunua, na yeye anajaa humo humo bila kuzingatia vigezo na masharti....kwa kweli bongo tunaoenda sana fashion...

Sent using Jamii Forums mobile app
Fasheni ya sasa ni Dualis na Subaru Forester. Imetoka Crown na Harrier tako la nyani.

Ikitoka hapo sijajua ipi inafuata.
 
😂😂😂Mbavuuu zangu mieee.....Eti Mabengo😂
 
Best yangu anamiliki hili bati asee anateseka na kugonga chini huyo

Yaan tuta kidogo utasikia paraaaa,

Mi namwambiaga endelea kuburuza chini[emoji28][emoji28]
Huyo sio dereva! Madereva wa kweli hawawezi kukwaruza Crown au Mark X hususani kwenye barabaraba za Bongo. Labda kama lingekuwa linaendeshwa huko Busimbiti.
 
Sasa hizo perfomance Cars utafananisha na Commuter?

Crown its a basic car, nenda ka google Lexus LFA V10 ndio walau unaweza ukaiweka sambamba na hizo gari hapo. Au Lexus GS-F
Comment niliyoi-quote haiongelei unachokisema.
 
Sawa mkuu, usigombe sana
 
Comment niliyoi-quote haiongelei unachokisema.
Lakin mlengo ni uleule tu, Bentley bentayga ni Suv performance car..huwezi ukailingisha na Crown ambayo Basic car. Kilichoongezeka hapo ni Performance. Ulinganifu mzuri ingekuwa Bentley bentayga(Suv performance car) vs Porsche Taycan(Sedan performance car) je bentayga unagusa huo mziki wa taycan. Jibu ni lilelile mkuu sedan cars kwa kasi ndio zenyewe ukilinganisha na suv. Gari yenye ground clearance ndogo uwa na stability nzuri sna
 
hizo gari sio mahususi kwa barabara zetu.
Best yangu anamiliki hili bati asee anateseka na kugonga chini huyo

Yaan tuta kidogo utasikia paraaaa,

Mi namwambiaga endelea kuburuza chini[emoji28][emoji28]
 
Wengi wetu hatujafikia kununua gari tofauti kwa matumizi tofauti, utakuta mi nina hela yangu ya mawazo nataka kununua gari ya kutembelea na mizunguko yangu mingine. Sasa inapokuja swala la barabara zetu, kiukweli hizi gari za chini hasa crown hazifai. Hapo DSM tu siku pakinyesha mvua kubwa huwezi kuitaka hiyo crown. Ukija kwenye uimara wa mashine na suspension, bado huwezi kulinganisha walau na Subaru Forester ama Suzuki. Ila kwa vile kipenda roho hula nyama mbichi, we nunua hilo crown lako, wacha mi nikomae na Subaru...
 

Na ndiyo maana wengi wanalia lia...kisa class mate wake kanunua, na yeye anajaa humo humo bila kuzingatia vigezo na masharti....kwa kweli bongo tunapenda sana fashion...

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo hivi hivi wengi walikimbilia Brevis, na sahivi hawazitaki tena. Wabongo wengi ni watu wa hype tu.
 
Huu ukweli mchungu[emoji848][emoji122]
 
Sawa mkuu, ila mada inazungumzia nini?! Speed au gari kuwa chini?! Kama issue ni barabara kipindi cha mvua basi kwa mazingira yetu hakuna sedan car yoyote inayoweza kuvumilia iwe Benz, Bmw, toyota na n.k hapo kwenye uimara wa mashine bado sababu zako sio za kitaalam na inawezekana huna sababu za kitaalam. Ukitaja engine bora za toyota huwezi kuiacha 4GR, ni moja ya engine yenye maboresho ya hali ya juu, hapo kwenye suspension inategemea gari unaipitisha wapi gari yoyote ukiipitisha sehem isiyo sahihi lazima italeta shida. Kabla hujanunua gari tafakari unataka kuitumia kwa matumizi yapi? Crown ni sedan luxury car huwezi ipeleka mashambani kwa kuwa sio gari iliyotengezezwa kwa matumiz ya namna hyo.
 
Alaf tujitahid ku stick ktk mada, thread inazungumzia swala la speed wengine mda mnaleta habari ya gari kuwa chini ama kwel wabongo hatukosagi sababu😂😂. Alaf utafikiri Crown pekee ndio ipo chini kuna hizi subaru impreza hatchback ambazo zimejaa sana hapa mjini zipo chini zaid ata ya hiyo crown, subaru B4 nayo ipo chini. Kila mtu na mapenz yake tunaopenda gari za kasi na zenye stability tunakimbilia sedan.
 
Hahah daah mzee baba kumbe muda wote huo unaiponda crown kumbe ww mwenyewe unaendesha Subaru?hahahah kwangu haya yamekua ni maajabu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…