Wengi mmeongea kwa hisia tu!Kiukweli kwa barabara zetu huwezi kukimbia zaidi ya kasi ya km 140/saa.Na hapo gari yako inatakiwa iwe katikati ya barabara na huo mwendo hauzidi umbali wa km 15.
Na ni barabara zifuatazokutoka DSM.
Barabara ya Morogoro
Ni kuanzia Chalinze kuitafuta bwawani,hapa unaweza kuona mbele kwa umbali wa km 15 na zaidi pamenyooka sana.
Barabara ya Morogoro -Iringa
Hapa ni kuanzia Sangasanga(njia panda ya kwenda Mzumbe university) kuitafuta kijiji cha doma(kabla hujaingia hifadhi ya mikumi)
na sehemu nyingine ni kuanzia Ruaha mbuyuni(Al Jazira hotel) kuelekea kijiji kimoja kinaitwa mahenge.
Iringa -Mbeya(TANZAM road)
Hapa ni igurusi
Morogoro -Dodoma
Hapa ni kuanzia Kibaigwa kuelekea Dodoma.
Dodoma - Singida
Hapa ni kuanzia manyoni,na ndio sehemu ya pekee kulikuwa na kibao kinachorohusu km100/saa miaka ya nyuma.
Dodoma - Iringa
Hapa unaanzia sehemu moja inaitwa chipogola hadi makatapora (Mpwapwa)
Babati- Arusha
Hapa ni kuanzia Babati hadi Magugu.
Same - moshi(Kilimanjaro)
Hapa ni same na pana upepo mkali sana.