Ati ni kweli kuwa kuna kada hata wafanye Kazi miaka mia hawezi kuwa na nyumba kama ya Mwijaku?

Akili kubwa sana mkuu,watoto hawawezi kuelewa ila tuliojenga namna iyo nyumba za ndoto zetu tunajua🙌🙌
 
Unauliza jibu? Alafu hiyo nyumba ya mwijaku haiwezi kuwa chini ya mill 600 labda kama unampigia mahesabu kwa kujenga tandahima
 
Ukiwa unalipwa take home ya 1M (ambayo kwa bongo ni wachache wenye nayo) na ukafanya kazi kwa miaka 35, utakuwa umelipwa jumla ya 420M, kwa kuwa mshahara unapanda utakuwa umelipwa kama 500M hiv,

Kwa 500M unajenga nyumba kama ile, changamoto ndugu zangu walimu, manes, polisi, na wengine wenye take home ya 500k
 
Acheni tu tuendelee kusoma mpaka tupate madigrii hata kama hayana hela nyingi kwa kazi zake inatosha. Hawa wanaofanya kazi za ajabuajabu na kupata mafanikio makubwa kuliko sisi wasomi wapate tu. All in all wasomi wawepo tu
 
Wewe si ndio Kuna waraka wako Ulikuwa unakataza watu wasiwe machawa?unaona Sasa unavyolipa uchawa?umeonaaa?

Uchawa ni umavi huo ndio msimamo wangu.
Hasa kwa mwanaume.
Bora Mwanamke akiwa Chawa japo najua wanawake kiasili wao ndio wanataka tuu kusifiwa na sio kusifia.

Hata Chawa ajenge Jengo refu zaidi duniani bado kwangu atakuwa katika nafasi ya hadhi ya chini Daima
 

Ukilipwa Milioni moja huwezi kuwa na nyumba ya milioni mia mbili hata ufanyaje, labda uwe na vyanzo vingine vya mapato.

1 month = 1M
1 Year = 12M
10 Years = 120M
30Years = 360M

Hapo hujala, hujavaa, hujaoa, hujasaidia ndugu, hujanunua gari, hujasomesha. Thubutu!
 
Bila vyanzo vingine kutoboa ngumu sanaaaa
 
Aaah Kwa hiyo hujaziheshimu Juhudi za Mwijaku?
 
Ufaransa, China....!! Ana haki ya kusema Kuna kada haziwezi kujenga hiyo nyumba.... Mwijaku ni agent na dealer wa mtu mkubwa kwenye Mambo ya unga!. Achana na watu kujifyatua akili wana mengi usiyoyajua.
 
Una dharau sana Robert 🤔🤔

Hapana!
Kuwaweka Watu katika makundi yao sio dharau.kwenye biolojia nilifundishwa Classification na hiyo ndio Application yake Mkuu.

Mbona mimi sijali wengine wakiniweka vile waonavyo (mitazamo yao ilivyo) na sioni kama wamenidharau?
 
Hapana!
Kuwaweka Watu katika makundi yao sio dharau.kwenye biolojia nilifundishwa Classification na hiyo ndio Application yake Mkuu.

Mbona mimi sijali wengine wakiniweka vile waonavyo (mitazamo yao ilivyo) na sioni kama wamenidharau?
🤣🤣🤣🤣🤣Kwa hiyo Mwijaku yupo kwenye kingdom animalia ,class Insecta au vipi?...(ilinisumbua sana hii topic😁😁)
 
Well said mkuu
 
🤣🤣🤣🤣🤣Kwa hiyo Mwijaku yupo kwenye kingdom animalia ,class Insecta au vipi?...(ilinisumbua sana hii topic😁😁)

Ile topic NI rahisi,nzuri, na Applicable.
Ukiijua hiyo na kuitumia hakuna mwanadamu atakayekuchezea wala hutamlaumu yeyote.

Kwani Kunguru utamuweka kwenye Kunguru wenzake
Njiwa kwa njiwa
Kenge kwa kenge
mbzui kwa mbuzi
Popo kwa Popo
N.k

Kosa kubwa ni kumlazimisha Mbwa awe paka. Yaani mtu ushamuona yupo class Hii alafu unataka utumie mawazo na matamanio yako awe vile utakavyo. Hilo ni kosa.

Mbwa m-treat kama mbwa
Paka m-treat kama paka
Kuku m-treat kama kuku.
Wote ni muhimu ila zingatia matumizi yao tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…