attention chitcatters: marekebisho ya sheria ya ukaguzi kabla ya chit chat ndoa

Voice of Wisdom

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
537
Reaction score
240
Kwa mamlaka niliypojipa mwenyewe (naomba msiniulize lini na wapi) na kwa kulinda heshima ya ndoa zinazofungwa hapa chit chat kila siku, mimi Voice of Wisdom napendekeza marekebisho yafuatayo katika sheria ya ndoa ya jamhuri ya chit chat sehemu ya ukaguzi.
Sheria ya zamani ya mwaka 2006 iliyofanyiwa marekebisho yake madogo mwaka 2010 na Chief Judge Mheshimiwa Rutta ina mapungufu na haikidhi mahitaji ya wakati na pia haendani na kasi ya ongezeko la ndoa zinazotangazwa hapa chit chat kila siku.
Hivyo basi baada ya kuridhia mimi na halmashauri ya yangu ya Voice of Wisdom marekebisho yafuatayo yamependekezwa yafanyike katika sehemu hii ya sheria ya ukaguzi


  1. Mkaguzi: Mkaguzi hatakuwa mmoja tena kama ilivyokuwa hapo awali, hi kutokana na ukweli kuwa kuwepo kwa ndoa nyingi zinazotangazwa kila baada ya masaa kadhaa hivyo kupelekea ofisi ya mkaguzi kuwa na majukumu yasiyoisha na hii imepelekea mkaguzi aliyeko kuwa na mgogoro wa ndoa na my wife wake kwani muda wote anakagua na akifika nyumbani yupu hoi bin mfu. hivyo basi
  2. Kuwepo na la jozi tatu (ndoa tatu halali) za wakaguzi ambao watakuwa chini ya mkaguzi mkuu ambaye ndiye mkaguzi wa sasa, na wakaguzi hawa watachaguliwa na chitchaters wenyewe baada ya wao kuomba na kutoa sifa zao hapa jamvini. Sababu ya kuweka jozi ni kuepuka uchakachauaji ambao umekuwa ukifanyika ili kuweza kuwahudumia wanajamvi wengi. na uchakachuaji huu umepelekea ndoa nyingi kufungwa na hatimaye kuvunjwa muda mfupi jambo ambalo si sawa kwa maadili ya jamhuri ya chitchat. Sababu nyingine ya kuwepo kwa jozi (ndoa inayotambulika na chitchat) ni ili kuepuka mkaguliwa/mkaguzi kuchakuchuana wakati wa ukaguzi.

Angalizo: Hakuna mkaguzi atakayeruhusiwa kumkaguwa mkaguliwa kama hayupo na my wife wake wakati wa ukaguzi
Mkaguzi yeyote lazima awe na ndoa isiyokuwa na mizengwe kama ya................(jazeni wenyewe, sitaki ugomvi mimi)

Kila anayetaka kuwa mkaguzi wa wakaguliwa atalazimika kuandika wasifu wake hapa jamvini na wanajamvi watamkubali au kumkataa

Kama wakaguzi wote watakuwa hawapo kutokana na majukumu au kuuguliwa au kuugua mkaguzi mkuu atawateuwa wakaguzi wa muda ili kuepuka ndoa bila ukaguzi kama inavyotaka kutokea kwa ndoa inayopingwa sana ya Mh Ruttashobolwa wakauguzi wa muda lazima wawe na sifa zote za kufanya ukaguzi.

napendekeza mabadiliko haya yaanze kufanya kazi baada ya kupata baraka za Judgement Kipipi, Baba V, Babu Asprin,Preta, CHief Judge Ruttashobolwa, Erickb52, Mamndenyi, FirstLady1 Filipo, nitonye, Arushaone Bishanga ,BADILI TABIA, Kongosho,Madame B, Kaizer, platozoom, Eiyer Young cacico Remmy Vin Diesel Nicas Mtei, BAGAH,marejesho noahism passion lady Mentor, Chilli gfsonwin snowhite Jiwe Linaloishi Arabela YNNAH Zion Daughter tedo Mr Rocky watu8 na AshaDii
Nawasilisha
 
Hee!
Huu ni udikteta mhe. Voice of Wisdom!!
Yaani wewe na halmashauri yako ya kichwa ndio umeamua kututengenezea sheria nchi nzima!!
Ngoja niitishe maandamano!
 
Last edited by a moderator:
Mboni husomeki...!!? umejipa jukumu wewe kama wewe kwa sababu mwenyekiti yuko selo au!??? Afu ujue kuwa wanaokaguliwa sio wanaotaka kufunga ndoa bali ni members wageni tu. Afu sijawahi sikia malalamiko toka kwa wake za Asprin sio cacico , BADILI TABIA wala yule mwingine wa kati. Hoja yako haina mashiko wala makamato. Kaanze upya, tena ikiwezekana ungetafuta uzi unaohusu utaratibu wa ndoa kama ulivyoainishwa na Baba V ingekupa mwanga zaidi
 
Last edited by a moderator:
mkuu samahani kwa kumislead, dhamira yangu ilikuwa ni kuleta mapendekzo ya marekebisho, nieedit
 
mkuu ni mapendekezo tuu, naona niliweka hoja kushoto kidogo
 
Hayo ni mapendekezo tuu si sheria hata wewe unaweza kutoa mapendekezo na tutayapitia!
H

Hee!
Huu ni udikteta mhe. Voice of Wisdom!!
Yaani wewe na halmashauri yako ya kichwa ndio umeamua kututengenezea sheria nchi nzima!!
Ngoja niitishe maandamano!
 
Last edited by a moderator:
mpK Baba V ARUDI NDO ULETE HII MANENO
 
Last edited by a moderator:
Baba V mbona amekuwa mhanga wa Bann kila mara! Au anahujumiwa wajemeni!
 
we mbon unkaba sana hadi penalty, si vizuri bana, ila ukweli ndo huo uliousema
 
Voice of Wisdom huu ushauri ulipita au marekebisho haya yalikubaliwa na loya Ruttashobolwa na kamati kuu ya ndoa za chit chat kwanza ambalo ni baraza la mawaziri la Chit chat
na je mkaguzi mkuu Asprin anakubaliana na haya
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…