Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete amesisitiza kuwa mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai siyo wa kubinafsisha, bali ni ukodishaji wa shughuli za uendeshaji kwa mwekezaji.
Akizungumza jijini Mwanza Julai 30, 2023 wakati wa mkutano wa hadhara wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaofanyika uwanja wa CCM Kirumba, Naibu Waziri huyo amesema ukodishaji huo utahusu baadhi ya gati za Bandari ya Dar es Salaam, lengo ikiwa ni kuongeza tija katika shughuli za bandari nchini.
Amesema kuongezeka kwa tija kutaongeza pia mapato kupitia kodi na ushuru mbalimbali na hivyo kuongeza uwezo wa Serikali wa kujiendesha, kugharamia na kutekeleza miradi ya maendeleo.
Naibu Waziri Mwakibete ametaja ongezeko la mapato kutoka Sh7.7 trilioni zilizokusanywa mwaka 2021/22 chini ya TICTS hadi kufikia zaidi ya Sh26 trilioni ifikapo mwaka 2031/32 kuwa miongoni mwa mafanikio yanayotarajiwa kupitia uwekezaji unaotarajiwa kupitia kampuni ya DP World ya Dubai.
"TPA ilikusanya Sh795 bilioni katika bandari zote na matumizi ya uendeshaji wake yalifikia Sh 791.2 bilioni hivyo tulisalia na faida ya Sh3.3 bilioni. Kwa sababu ya teknolojia isitofaa. Tunatumia muda mwingi kukusanya fedha nyingi na kuzitumia kuendesha bandari ili tukusanye fedha nyingi na zitunufaishe," amesema Mwakibete
Mwakibete amesema mataifa yanayotegemea bandari hiyo kupitisha shehena mwaka 2021/22 yalipitisha mizigo tani milioni 8 kulinganisha na tani milioni 60 zinazotarajiwa kupitia uwekezaji mpya.
Ametaja nchi zinazotegemea bandari ya Dar es Salaam kuwa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Burundi, Rwanda, Zambia, Angola, Malawi na Botswana.
huku akisema uwekezaji huo ukicheleweshwa kuna uwezekano wa mataifa hayo kupitisha shehena katika bandari za nchi washindani ikiwemo Bandari ya Mombasa (Kenya), Beila (Msumbiji) na Durban (South Africa).
"Meli ziazotia nanga katika bandari ya Dar Es Salaam zinasubiri muda mrefu kupakua na hivyo kuongeza gharama kwa wafanyabiashara. Uwekezaji mpya utaongeza ufanisi ikiwemo kupunguza muda wa meli kusubiri kupakua mizigo,’’ amesema Naibu waziri huyo.
Katibu wa Oganizesheni Taifa (CCM), Issa Gavu ameitaka Serikali kukamilisha mchakato wa ukodishaji wa bandari ya Dar Es Salaam kutekeleza ilani ya uchaguzi wa chama hicho tawala.
"Kifungu cha 59(b)(iv) cha Ilani ya CCM 2020-25, Serikali imeagizwa kufanyia ukarabati na maboresho ya bandari zetu kuanzia ya Mwanza, Musoma, Nyamirembe, Bukoba, Dar Es Salaam na nyingine; hivyo CCM inaiagiza Serikali kuendelea na utekelezaji wa miradi yote ya kuboresha bandari zote," amesema Gavu.