Pre GE2025 Aubrey Silayo mtumishi wa TRA anayefanya ulaghai kusaka ubunge Vunjo

Pre GE2025 Aubrey Silayo mtumishi wa TRA anayefanya ulaghai kusaka ubunge Vunjo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

MTANZANIA620

Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
65
Reaction score
81
Kuelekea uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Urais mwaka 2025 joto kumeanza kuchangamka maeneo mbalimbali ya Nchi kwa watu wenye nia ya kujitosa kwenye udiwani au ubunge kuanza kupitapita.

Moja kati ya maeneo yanayoshuhudia vikumbo vya wenye nia ya ubunge ni Jimbo la Vunjo ambako moja kati ya watia nia wanaopita kwa kuwalaghai wanaCCM kwamba amepata idhini ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri wa Fedha kuanza kampeni katika Jimbo hilo ni Ndg Aubrey Silayo.


Katika vikao vyake vya wiki iliyopita mbali na kugawa fedha shilingi elfu 20 na elfu 30 kwa wajumbe aliokutana nao aliwaeleza yeye ana baraka zote za viongozi wa juu wa CCM Taifa ikiwemo Halmashauri kuu kitu ambacho ni uongo wa wazi kabisa na anafanya ulaghai.

Tunamshauri Ndg Aubrey Silayo aachane na ukiukwaji wa taratibu na asubiri muda ufike.

Tutawasilisha video zake akiwa anagawa fedha na audio alizorekodiwa maeneo mbalimbali kwa ushahidi kwenye vikao vya maadili vya CCM, TAKUKURU pamoja na kwa Kamishina wa mapato (TRA). Muda wa kampeni bado wasituletee siasa za makundi zinazoidhoofisha CCM na kuwabugudhi viongozi waliopo katika kuendelea na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025 kwa utulivu.
 

Attachments

  • 1735366814106.jpg
    1735366814106.jpg
    441 KB · Views: 9
Tra na wachaga ni.kama rejeta na.maji. akina.kimario. silayo. Temba. Mzava. Shio. Matemba. Wote walikuwepo.
 
Back
Top Bottom