Audi A4 vs Toyota Crown nipe maoni yako

Audi A4, spear zake ikimbie Kama ukoma. Ukiinunua ni lako haliuziki tena ni mali yako. Spear zake hazipatikani, mafundi wake hawampo. Kama wapo hawajui Cha kufanya kuhusu ilo gari. Hata disc zake kupata ni shidaaaaa
Mwache afunge nalo ndoa. Na hizi njia zetu za madimbwi sensor zitamfundisha akili tu 🤣🤣🤣 mie wa Crown ntaenda kunyofoa kwenye gari zilizokatwa pale Tandale.
 
Audi, BMW ,vw , nissan, RVR, pajero, ukiinunua umeoa mke wa tisa au umeolewa mke wa tisa. Hayo magari epukaneni nayo .
Daaa, nilivutiwa na VW Tiguan, naona iko poa sana. Sasa hii comment yako, nimechoka hoi.
Tanzania sijui tuna shida gani kung'ang'ania Toyota tu? Nchi nyingi tena zingine ndogo tu wanaendesha magari ya Europe na hakuna shida yoyote na spea zipo. Tanzania ni tofauti kabisa. Kwa mfano, Kenya tu hapo wana spea kibao za Pegeout, BMW,AUDI, RANGE ROVER, VW ET AL!
 
Manake kipato kidogo cha wateja.

Sio kukubalika.

Kwanini hizo Tecno hazikubaliki EU na USA?

Ila ndo bidhaa pendwa ya poor countries.

Sawa na Yutong, Faw au Howo.
Bei ya audi A4 na Toyota Crown zipoje Beforward?
 
Usiogopeshwe na maneno ya wanazi wa Toyota humu. Chukua chuma unachopenda. Mafundi wapo wengi, wauzaji wa spares wapo wengi na ukitaka unanunua spares mwenyewe.
Gari unanunua ili ulitumie, na siyo ati uje uliuze. Furahia maisha ndugu, maisha mafupi hapa tunapita tu.
 
Acha dharau wewe..Crown unafananisha na kigari cha mpito hio verossa! Crown ni executive Sedan. Japan ndio wanatumia mawaziri hizo.Ni gari iliotengenezwa kwa umakini wa hali ya juu.

Watu wanaotumia Crown [emoji146] asee !! Mnapenda masifa asee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…