Audi A4 vs Toyota Crown nipe maoni yako

Sawasawa
 
Mimi ni muumini wa kuamini mtu anunue kile akipendacho,ingawa pia ni JDM fan dam dam.

Audi/Bmw/Benz ningeshauri mtu anunue akiwa anaishi kwny hii miji mikubwa Dar/Mwz/Arusha/Dodoma kwa ajili ya kupata spea kwa urahisi na upatikanaji wa mafundi wake lkn uko unaishi wilaya ya Tanganyika mkoani katavi aisee utajua haujui.
 
Afadhali leo nimekutana na wataalamu wa haya mambo hapa jukwaani. Nina mpango wa kuagiza hii ndude Siku za usoni, ebu nipeni ushauri wenu ndugu wataalam. Premio new model
 
Na hiyo miji mikubwa mtu usipojiongeza, bado ni msala kwa hizi gari...
 
Ahahaaaaa, wote tunapenda kuwa na unique cars tatizo linakuja maintenance ya hizo gari. Najijua na hela ya mkopo siwezi chuka Europoean cars, nitavimba na Mjapani hata siku nataka kuuza siumizi kichwa, nitakapo hitaji spare pia niipate kwa gharama nafuu.
 
Mimi sijasema AUDI ni gari nzuri kwa mazingira yetu, namaanisha pamoja na kuwa AUDI ni Cheap kuliko CROWN bado watu wananunua zaidi CROWN kuliko AUDI na sababu kubwa ni uwezo wa kumudu matengenezo na gari kuvumilia mazingira yetu..
Na umasikini unachangia hamna ambae hapendi European car

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utasikia, "naomba tukutane kwa fundi Mudi wa pale chini ya mwembe tuifanyie sevisi tukufurahishe"...tatizo huwa tunatoa ushauri kwa mazoea kuliko uhalisia, hata gereji zetu walishazoea kuandika "spear zinapatikana hapa" Na watu wanaona ni sawa tu, cha muhimu nunua kitu roho inapenda na itunze
 
Afadhali leo nimekutana na wataalamu wa haya mambo hapa jukwaani. Nina mpango wa kuagiza hii ndude Siku za usoni, ebu nipeni ushauri wenu ndugu wataalam. Premio new modelView attachment 1661559
Premio ni gari ambazo ukinunua unajenga bifu na mafundi... Maana wanajua wamekosa kazi hapo... Hizo gari haziendi gereji kama ni mtunzi mzuri kwahiyo mafundi wanakosa kazi😅😅😅
Vuta haraka usiwaze kabisa
 
Kwa kifupi tu:

Audi ni Slayqueen mrembo sana mbwembwe nyingi na gharama za hali ya juu. Havumili shida hata kidogo.

Crown ni wife material ila mrembo asilia au natural. Anavumilia hata wakati wa shida.

Ni hayo tu...kama una akili utajiongeza.
Well Said
 
Ukisikiliza sana wadau unaweza amini hakuna spares za european cars bongo, kumbe ni pesa yako tu, kila spea ipo. Gharama kubwa ya spea ni kutokana kuwa ni genuine. Hata ukitaka spare og ya toyota utapata kwa gharama kubwa kama hizi. Spea og zinaku offee mileage kubwa sana.
 
Ndo nilichojaribu kazia..haina tofauti na mark x tofauti tu ndo Toledo jipya....ukiacha ugharama wa vifaa ni ujinga kufananisha German machine kama AUDI na crown
Crown ni toleo jipya kuanzia lini ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…