Audi wamezindua EV Brand China inaitwa AUDI, bila zile "rings" nne tulizozizoea!

Audi wamezindua EV Brand China inaitwa AUDI, bila zile "rings" nne tulizozizoea!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Hawa Wajerumani sijui wamepaniki na speed ya Mchina kwenye EV?
arenaev_002 (1).jpg

Ili week Audi wamezundua brand specifically kwa EV uko China inaitwa AUDI, kwa herufi kubwa na bila zile rings za siku zote.
arenaev_003 (1).jpg

Brand hii ni muungano wa Wajerumani Audi na Mchina SAIC, na kuanza wameanza na kutoa gari lao la AUDI E.
arenaev_004 (1).jpg

Makampuni mengi wanajitahidi kushift kwenda EV na kupeleka biashara zaidi China kwasababu soko lake ni kubwa sana Duniani.

Ngoja tuone kama AUDI atafanikiwa kwa kuanza na hii AUDI E.
 
Audi ipo china kwa miaka 30 sasa
Trump anaposema ataongeza kodi kubwa sana kwa bidhaa za mchina basi anawalenga hawa wanaopeleka makampuni yao huko na mchina pia
MAGA ndio moto yake na anamaanisha haswa
Anataka awe juu sana 🇺🇸

Ila Audi ya umeme imetulia ndani daa
 
naona imekaa kama maybach. ila kwa tz tutaishia kuziona kwenye picha. ukiachana na ughali,hakuna mafundi hapa.weng wamezoea kwa mazoea
 
Wameqmamua kujiunga na wenye nguvu kwenye huo uwanja, partnaship itawasidia kuimarisha technology yao na soko lao.
 
naona imekaa kama maybach. ila kwa tz tutaishia kuziona kwenye picha. ukiachana na ughali,hakuna mafundi hapa.weng wamezoea kwa mazoea
Zitakuja lakini ni baada ya muda. Ulimwengu wote unahamia kwenye magari ya umeme hivyo baada ya miaka kadhaa kutakuwa hakuna tena magari haya ya mafuta. Na mafundi nao itabidi wabadilike.
 
Yaani imegeuka sana, mwenyewe sikutegemea aisee. Nilijua Tesla atakua dominant
Kwa ukaribu wa trump na musk naona basi Tesla atakimbiza tu marekani in the long run, trump anakuambia ukitaka akushushie Kodi Jenga kiwanda marekani hapo hapo, wazungu wanaendelea kwasababu ni wabinafsi, sisi mpaka ndala tunaagiza china, Hawa ilitakiwa tuwabane walete viwanda huku in the long run na sisi tujitegemee
 
itakuwa ngumu kui_transform dunia nzima kutumia magari ya umeme kwa ghafla, labda huko mbeleni karne ijayo, haswa Africa itachelewa mno.
*mimi binafsi huo mfumo bado haujaniingia moyoni wala akilini mwangu siupendi, angalau GAS lakin umeme hapana, tena ndio ukizingatia na hawa mafundi nyundo wetu ni hatari tupu kuna mtu kulala road.
 
Kwa ukaribu wa trump na musk naona basi Tesla atakimbiza tu marekani in the long run, trump anakuambia ukitaka akushushie Kodi Jenga kiwanda marekani hapo hapo, wazungu wanaendelea kwasababu ni wabinafsi, sisi mpaka ndala tunaagiza china, Hawa ilitakiwa tuwabane walete viwanda huku in the long run na sisi tujitegemee
mchina anapowaumiza kichwa wamagharibi ni kwenye gharama za uzalishaji wa bidhaa,,hapo ndo pagumu........atatoza kodi kubwa viwanda vya china ila ndo vinavyoleta bidhaa nyingi nchini mwao na kwa gharama nafuu,,,hapo jamaa anataka kuwatoa raia wake kwenye msoto, uongeze mishahara/kipato cha mwananchi halafu hapohapo bei ya bidhaa nchini kwako inaongezeka unakua bado hujasolve kitu,,,,,,,,mshahara anaolipwa mfanyakazi anaekua nchi za magharibi ni tofauti kabisa na mishahara inayolipwa china na bado gharama nyingine za uzalishaji.....,ndo maana makampuni mengi yalikimbilia china
 
naona imekaa kama maybach. ila kwa tz tutaishia kuziona kwenye picha. ukiachana na ughali,hakuna mafundi hapa.weng wamezoea kwa mazoea
Kusema la haki sisi bongo tuko nyuma kwa kila kitu zaidi ya ujuaji na utapeli
Siwasifii Wakenya ila wametuacha mbali kwenye haya mambo
Kuanzia pikipiki za umeme mpaka magari na hata daladala za umeme wanazo na wanazitengenezea nchini kwao au kuziundia hapo
Sisi bla bla nyingi
Acha gari za umeme hata Benz au BMW ni ngumu kupata mafundi wa maana
 
Sisi tunauza nickel + lithium (new gold) deposits tulizona kwa hao wachina, jamaa wanaunda betri zinazotumiwa na magari, mwisho wa siku ndinga kali zinauzwa Uropa na Uamerika...
 
Back
Top Bottom