WanaJF,
Pamoja na tofauti zangu za kisiasa na mambo mengine ya aina hiyo kwa CHADEMA, lakini linapokuja suala la kitaifa tunapaswa kusimama pamoja na kukemea maovu yanayoweza kuharibu sifa na heshima ya nchi yetu.
Dr Slaa akiwa katika ziara yake nchini Marekani, amealikwa katika kituo cha radio chenye frequency 93.1 WIBC, Indiana, Marekani. Kituo hichi ni moja ya vituo maarufu nchini Marekani kwa kutetea haki za mashoga na ndoa za jinsia moja.
Kwa sasa Dr Slaa anaendelea kufanya mahojiano na kituo hicho na kwa kuanzia mahojiano yao wameanza kumkashfu rais wetu kuwa aheshimu haki za binadamu, kuwa ni katili, kisa tu amekataa kutambua ndoa za jinsia moja.
Je, Dr Slaa kushirikiana na watu wa aina hiyo, watetezi wa ndoa za jinsia moja, huo ndio utaifa?