Audio: Americans Describes Kikwete As A Tyrant, 93.1 WIBC USA interview with Dr. Slaa

Audio: Americans Describes Kikwete As A Tyrant, 93.1 WIBC USA interview with Dr. Slaa

Mwanzo niliona kama vile Dr.Slaa leo kaja kizalendo zaidi, duuh mwishoni jamaa hatari.

CDM angaikeni na sababu zitakazo wapa ushindi au kushindwa kupitia sanduku la kura, hizi siasa za kuchochea uhasama ambao upo kwenye imaginary world auna tija kwa sisi raia. Mtwara mmeona kuko shwari mmeanda anzisha uchokozi wa raia tena. Hivi mkipewa serikari nyinyi hela mtatoa wapi za sera za taifa kama kila mtu achukue chake.

Mada ya kufungiwa kwa gazeti la the EA watu wengi waliochangia wa pande zote za siasa waliungana na serikari. Yaani mwanasiasa anapokuwa gullible kiasi kile na kushindwa uzalendo kisa support ya nje inasikitisha sana.
 
Kapwela, kwa maoni yako haya ni wazi huijui Marekani wala siasa zake. Juzi maseneta wa chama cha Upinzani Republican wamemwandikia barua kiongozi Mkuu wa Iran wakimtahadharisha kukaa chonjo na Raisi wao Obama kwa sababu eti haaminiki; je hii ingewezekana Tanzania bila watu kukamatwa na kuwekwa ndani bila kujali nafasi zao ndani ya Upinzani. Mambo yanapofikia hapa ndipo wengine tunapobaki tumeduwaa na kuanza kujiuliza; hivi wengine wetu mnaishi katika sayari gani? Wakati Raisi wao Obama analihutubia taifa, mjumbe moja wa Congress alimwita muongo na hii ilishuhudiwa na wananchi wote waliokuwa wakifuata hotuba hiyo, je itakuwaje siku Kikwete anaitwa muongo live wakati anahutubia taifa kupitia bunge? Hiyo ndiyo Marekani Kapwela na si hiyo unayofikiria ukiwa kibarazani kwako Kariakoo na kikombe chako cha kahawa.

Haa ha ha sasa isijekuwa wewe ndio umepotoka hulijui hili alafu mie wa Kariakoo na kikombe cha kahawa nalijua hili. Dunia ilivyo sasa unaweza ukawa Kariakoo lakini ukajua siasa za marekani kuliko Mtanzania aliyeko Washington DC, ni information tu.

1. Maseneta wa Republican waliandika barua kwenda Iran waligeuka kituko kwa kufanya jambo ambalo ni la aibu kwao kufanya. Ni jambo la ajabu kufanyika katika utamaduni wa siasa za Marekani, na waliumia kisiasa kwa kitendo hicho, Wamarekani wengi walichukiza na kitendo hicho cha fedhea kwa nchi yao.
Refer: http://www.huffingtonpost.com/2015/03/12/poll-iran-letter-inappropriate_n_6857644.html

Na wengine baada ya lawama kuwazidia wengine ilibidi wajitokeze kujilaumu kwa kufanya kitendo hicho

..(Bloomberg) -- At least a few of the Republican senators feeling the backlash from signing an open letter to Iran's leaders are expressing some second thoughts. Amid mounting criticism from allies, home-state editorial boards and colleagues who opted not to sign the missive, U.S. Senator Ron Johnson became the latest Republican to suggest he might do things differently if given another chance.

Sasa unataka Dr Slaa aige kitendo kilichowafedhehesha wananchi wa nchi badala ya kujivunia?

2.Hiyo ya Obama kuambiwa muongo kwenye congress kwani ajabu na tatizo lipo wapi hapo?ni siasa ndani ya nchi. Ila wasingemzomea Rais wao wakiwa Mexico; msingi wa hoja ni kuwa husemi ubaya wa nchi yako nje ya nchi

Otherwise sijui kama umemsoma Mitt Romney hapo chini?hii ndio jadi ya siasa za Marekani, unamsikia kila siku Jeb Bush akimsema Obama kuhusu Israel, lakini akienda ziara nje hutamsikia akimsema Obama, ni ndani ya Marekani tu ndio atamsema.Kama ulikuwa haupo aware na hili fuatilia utajua,huu ni utaratibu wa jadi wa siasa za marekani
Refer hapa: Romney foreign policy attack was disgraceful
Romney foreign policy attack was disgraceful - CNN.com


"Partisanship ought to end at the water's edge" is a longstanding adage of American politics.

Na hapa Romney alikuwa mwangalifu kutosema mabaya na nchi yake;Mitt Romney meets U.K. leaders ahead of London fundraiser - CBS News

"While I'm on foreign soil, I'm very careful not to be critical of my own government's policies," said the presumptive Republican nominee. "I would be even more remiss if I were to be critical of any other government's policies. I will instead look forward to an exchange of ideas."


TOFAUTI ZA KISIASA ZETU ZIISHIE MPAKANI, NJE YA MPAKA KILA MMOJA AENDE AKIIWAKILISHA TANZANIA,NCHI YETU SOTE, HADHI YA TANZANIA NI MUHIMU ZAIDI KULIKO SIASA ZETU. HUKU NDIO KUKUA KISIASA KUFANYA VINGINEVYO HATUAIBISHI NCHI TU BALI TUNAJIAIBISHA WENYEWE

Mcheck na Obama alivyokuwa bado mpinzani alivyoishika hiyo desturi.

http://politicalticker.blogs.cnn.com/2008/07/25/obama-sidesteps-bush-criticism/comment-page-1/

PARIS, France (CNN) - Sen. Barack Obama said Friday he was avoiding criticizing President Bush on his trip through Europe.

Speaking to reporters, the Democratic presidential candidate cited a tradition that "you don't criticize a sitting president while overseas," adding that "it's very important" that U.S. foreign policy is presented "in one voice."

Sasa kwa kumsoma Romney hapo juu na Obama hapa juu utatambua kuwa ni ulivyodhania sivyo na nilivyosema ndivyo ilivyo.
 
Happy Feet; Hebu,tuambie "uzalendo" kwako unaelewaje kwani? Nadhani ni kwa tafsiri yako hiyo hapo juu,siyo?
 
Kapwela
Majibu murua kabisa tatizo Mag3 anadhani siasa za US anazifuatilia peke yake.

Kitendo alichokifanya Slaa si cha kizalendo kabisa.

Nawashangaa wafuasi wa Chadema kishangilia hii interview.
 
Last edited by a moderator:
Kapwela
Nyie watu msilete unafiki hapa, mara ngapi tushaaibika nje huko rais huyu huyu anaulzwa chanzo cha umasikin haju sio aibu hyo? Wote tulo mchagua tunaonekana wajinga.

Mikataba tunayoingia yote ni ya ulaghai wanatuzid ujanja unadhan hatujapata aibu.

Kisa leo Slaa kachangia hali ya kisiasa ya nchi et aibu hakuna aibu hapo labda kama na ww upo ktk utawala n aibu kwako kwasababu utawala unanyanyasa wanyonge alafu unataka ulimwengu ucjue et siasa safi na kulinda nchi, upuuz mnaumia ndani alafu nje mnasema nchi ina utawala bora,
Tufikie wakat tuache kufarijiana lazima tupinge maovu wakati wowote na mahali popote.
 
Last edited by a moderator:
Kapwela

Umesikiliza au unaongea tu? Kama huelewi lugha sema wakusaidie Mkuu. Maana siku hizi MTU anashahada lakini hajui lugha ndio mazao ya shule za kata. Acheni kupotosha maana audio IPO mmepewa fact kaeni kimya.so kila siku mnaenda kuomba huko Leo vipi tena?
 
Last edited by a moderator:
Rais wetu anaitwa tyrant wewe unaona ni sawa tu? Tena na Wamarekani? Serious!

Mkuu hapo wamarekani unaosema sio Rais wao alikuja mkampigia deki barabara na mtaa ukaitwa jina lake?
 
Nyie watu msilete unafiki hapa, mara ngapi tushaaibika nje huko rais huyu huyu anaulzwa chanzo cha umasikin haju sio aibu hyo? Wote tulo mchagua tunaonekana wajinga,
Mikataba tunayoingia yote ni ya ulaghai wanatuzid ujanja unadhan hatujapata aibu,
Kisa leo Slaa kachangia hali ya kisiasa ya nchi et aibu hakuna aibu hapo labda kama na ww upo ktk utawala n aibu kwako kwasababu utawala unanyanyasa wanyonge alafu unataka ulimwengu ucjue et siasa safi na kulinda nchi, upuuz mnaumia ndani alafu nje mnasema nchi ina utawala bora,
Tufikie wakat tuache kufarijiana lazima tupinge maovu wakati wowote na mahali popote

Msome mgombea urais Mitt Romney hapo na mgombea urais Barack Obama utaelewa.Kufanya vinginevyo ni kujidharirisha mwenyewe na kudharirisha nchi

Mitt Romney "While I'm on foreign soil, I'm very careful not to be critical of my own government's policies," said the presumptive Republican nominee. "I would be even more remiss if I were to be critical of any other government's policies. I will instead look forward to an exchange of ideas."

PARIS, France (CNN) - Sen. Barack Obama said Friday he was avoiding criticizing President Bush on his trip through Europe.

Speaking to reporters, the Democratic presidential candidate cited a tradition that "you don't criticize a sitting president while overseas," adding that "it's very important" that U.S. foreign policy is presented "in one voice."

Obama hapa wakati huo akiwa hajaingia ikulu anasisitiza kushika utamaduni huyo,HUPASWI KUMPINGA RAIS UKIWA NJE YA NCHI, twende nje ya nchi tukiwa na sauti moja, tuilinde hadhi ya nchi yetu.
 
tyranic-selfsh for personal gain this is according to six types of governments by aristotle
 
Kapwela

Kwa nini msisikilize wenyewe? Kila kitu kipo sikiliza mkuu kabla ya kuanza kulaumu.
 
Last edited by a moderator:
Majibu murua kabisa tatizo Mag3 anadhani siasa za US anazifuatilia peke yake.
Kitendo alichokifanya Slaa si cha kizalendo kabisa. Nawashangaa wafuasi wa Chadema kishangilia hii interview.
Ha ha haa Mshume Kiyate, hilo jina...mmm hilo niliache! Huyo Kapwela, narudia hajui siasa ya Marekani. Hiyo mifano miwili niliyoitoa ni michache tu ikilinganishwa na mingine mingi tu iliyowahi kutokea. Je unajua Democrats pia waliwahi kufanya yanayofanana na hayo kwa Raisi Bush? Mara ngapi wapinzani wanaongelea mapungufu ya serikali yao wanapokuwa nje ya nchi yao iwe Ulaya na kwingineko? Je toka barua hiyo imeandikwa ni Republicans wangapi wanaotaka kugombea Uraisi huko Marekani wamelaani hiyo barua? Unachosahau ni kwamba siasa ya Marekani ni habari nyingine kabisa. Huko hata kiongozi wa Democrat atamkosoa wazi wazi Raisi wake na kupinga wazi wazi msimamo wa chama chake. Endelea kufanya google, utajifunza mengi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom