AUDIO: Hili ni tatizo gani kwenye engine?


Sawa mkuu chilubi , shukrani kwa insights zako.

Taa ya oil haijawaka bado.

Engine oil natumia 5w30 quartz 9000 (full synthetic) ya TOTAL.

Yes, hiyo knocking ni mpaka engine inapochemka ndo inaanza, at idle only, pia at low rpm only (max rpm 1,200). Mfano napowasha gari asubuhi na kuiacha tu kwenye silencer, inachukua dakika 20 hivi ndipo knock inaanza.
 
At cold start engine revs ziko juu kwa ajili kupasha engine (pump inazungushwa kwa speed), ikiwa warm, revs zinapungua, pump inapunguza speed, kama bearing ya pump mbovu itagonga (inakua na play ndogo)

Kwenye cold start (asubuhi) revs za kupasha engene hushuka haraka mbona. Napowasha asubuhi, rpm huanzia kwenye 1,600 hivi kisha inashuka taratibu within two minutes hivi rpm inarudi chini kwenye normal idling (rpm 500).

Lakini kuhusu hiyo knocking, napowasha gari asubuhi (at cold start) na kuiacha tu kwenye silencer/idle, inachukua dakika 20 hivi ndipo hiyo knock inaanza.
 
So far, kwa maoni ya wadau katika uzi huu, yaonekana hiyo knocking sound suspect kuu ni tatu:

1. Oil pump.
2. Water pump bearing.
3. Tapet.
 
Mkuu Chamoto , tafadhari nakuomba upitie uzi huu. Mawazo yako yanahitajika hapa.
 
Mkuu Chamoto , tafadhari nakuomba upitie uzi huu. Mawazo yako yanahitajika hapa.
Kelele hizo zinatoka ama kwenye injectors au lifters. Sasa kwakuwa umeshabadilisha hizo injectors, basi inabidi uangalie kama oil yakutosha inapanda kwenye heads.

Mara nyingi kelele kwenye engine huwa zinatokea wakati iko cold, ikipata joto kelele zinapotea, hii ni kwasababu at cold start, vyuma vinakuwa vimesinyaa na hivyo kuwa na friction kubwa.

Sasa kwa kuwa gari yako inafanya tofauti na hivyo na hasa ikiwa kwenye idle, jaribu kufanya oil pressure test. Kuna uwezekano gauge yako haifanyi kazi vizuri na kusoma vibaya.

Kama hupati oil pressure yakutosha, engine itatoa kelele kama hizo, ikipata joto, kwakuwa oil ikipata joto inakuwa nyepesi (less viscous) na kusababisha friction kuongezeka.
 

Shukrani sana mkuu kwa insights zako. Ninafuatilia na nitatoa update hapa hapa.
 
Nalifanyia kazi suala hili within this week. I will update.
 
Tafuta fundi mzuri akuangalizie valve clearance mzee

Kwa tatizo main ishu ni Valve clearance

Fsnya hivi tega sikio kwenye kila Top cover cap hizo za cylinder head huku gari ikiwa imewaka then sikiliza mlio unatokea wap mzee
 

"Oil pressure test". Mafundi wetu hawa wa mtaani ukiwaambia kipimo cha Oil Pressure wanaishia kukodoa macho tu, hawakijuwi.
 
Tafuta fundi mzuri akuangalizie valve clearance mzee

Kwa tatizo main ishu ni Valve clearance

Fsnya hivi tega sikio kwenye kila Top cover cap hizo za cylinder head huku gari ikiwa imewaka then sikiliza mlio unatokea wap mzee

"Valve Clearance"... sawa mkuu. Changamoto ni namna ya kumpata huyo 'fundi mzuri'. Hawa mafundi wetu ni matatizo tu, wanachokonoa tu engene kwa kubahatisha na kupiga ramli.
 
Mkuu new generation , pitia hapa.

Kama unatumia simu, jaribu kusogeza spika sikioni ndipo unaweza isikia vyema hiyo engene knocking.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…