Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!


This is the conclusion:
In long term, taifa ni lazima liwe na system nzuri ya utawala wa kikatiba ambao utamwezesha hata asiye na Elimu kutawala kama Professor. Na Fisadi kuongoza kama malaika.
 
 

- Hiki cheo alipewa as shinikizo kutoka kwa Mwalimu as a sympathy, baada ya zile juhudi za kumfanya rais 1985 kugonga mwamba, infact Mwalimu had to work hard kumtumia Mandela na kumhamishia Addis, maana alijua kwamba pale under Mwinyi Salim wa not safe politically,

- Unasema kukikubali cheo ambacho hakimo kwenye katiba ni heshma tu, sina tatizo kukubali hilo, lakini bado ina-cast a big doubt na uwezo wa kufikiri na hasa uwezo wa uongozi wa yule anayekipokea.

Respect.

FMEs!
 

What about yule anayetoa hiyo nafasi na kuteua?

Hivi leo hii achilia mbali Katiba na kama nafasi iko kwenye katiba au la, ni Wanasiasa wangapi ambao hukubali vyeo alimradi wamepewe madaraka ilhali hawana ujuzi au taaluma katika fani?

Ni kwa sababu, nafasi zao si za kitaalamu bali ni za kisiasa mno.

Mfano mwingine, Aha Migiro na dada yake Mwantumu, waliwekwa kufanya kazi wizara mmoja, mmoja akiwa Waziri, mwingine akiwa Katibu Mkuu, wao walijua kuwa wao ni tumbo moja, lakini bahati mbaya, aliyewateua kumbe alikuwa halijui au washauri wa Rais na hata TISS walipitiwa kuliona, je tutasema kuwa nao Asha na Mwantumu na usomi wao walifumbiaje macho kumtonya Rais kumwambia hili si sawa?

Je Mzee Nyanganyi na Mwakawago ilikuwa ni lazima wawe wana diplomasia ili wawe mabalozi? au Mama Maajar? The answe is nope, they do not need to be career diplomats, wao kazi yao ni kumwakilisha Rais na kufanya kile Rais anachowatuma. Masuala ya kitaaluma wanaachiwa madeputy na wengine ambao wao ndio wasukaji wa kila kitu na kushirikiana na Wizara ya Nje na wizara nyingine husika kama Ulinzi, Fedha, Utamaduni, Biashara nk.
 

Mkuu FEMS hapo kwenye kuhusu Mandela na mwaka 1985 bado sijaelewa maana Mandela si bado alikuwa jela?

Pili kwenye kupewa cheo cha unaibu waziri mkuu kwa maoni yangu ni kuwa Mwinyi aliridhika na kazi za Mrema na akaona kikwazo ni katiba na hivyo ili kuweza kupanua wigo wake wa kimamlaka ilibidi atumie uwezo ama nafasi alinayo kama Rais kufanikisha hilo,sasa hapo sioni ni kivipi uwezo wa aliekipokea ukawa na mashaka kuliko uwezo wa aliyekitoa cheo hicho.
 

Zakumi kuna kitu "Moral obligations" ambapo haijalishi kama kuna system nzuri namna gani ya utawala wa kikatiba kama viongozi tunawaowategemea wata lack hiyo character.....Chukulia kama accounting,system iko lakini kama hakuna moral obligations lazima wizi utakuwepo tu...usichukulie issue hii kama mchezo wa watoto wa merry go round. Kama hakuna uzalendo kwa kiongozi hakuna system itakayofanikisha hayo ya asiye na elimu kutawala kama profesa ama fisadi kama malaika. Na ndio maana kuna wale wanaosuggest tufuate mfano wa wachina kwenye kudeal na ufisadi,yani kuwe na code maalum ya kushughulikia violations za moral obligations.Wachina kosa la ufisadi ni death straight out.
 

- Mushi sikuweka time limit ya when Mwalimu, alimuahimishia Salim Addis, na besdies jaribu kufanya utafiti kujua serkali yetu ilitumia hela ngapi kumpeleka Salim na Mama Mongella kule, Addis.

- Miwnyi angetumie wigo wake kimadaraka then Msuya, asingeweza kumtoa Mrema kama alivyofanya, bila kum-consult yeye Mwinyi. Kiongozi mwenye uwezo mkubwa wa uongozi na kufikiri, hawezi kukubali cheo kisichokuwepo kwenye katiba ya jamhuri ya nchi yake, ndio maana Mandela alikataa kutoka jela mapema kwa sababu aliogopa hiyo fugazz,

Respect.

FMEs!
 

FMES,Mwinyi alipanua wigo wa authority ya Mrema ili aweze kufanya kazi zake vizuri zaidi ikiwa ni pamoja na kupambana na mafisadi,lakini kama cheo hicho hakikuwa juu zaidi ya cheo cha Msuya ambaye aliona kuwa ufanisi wa Mrema unamfunika hata yeye ambaye ni bosi wake....Na pia usisahahu kuwa mafisadi ni viongozi wengi wao wakiwa serikalini... Tuliona yaliyompata Sokoine,kwa kutokujuwa kuwa anaopambana nao ndio hao hao anaokula na kunywa nao kila siku,hakuna tofauti na Mrema kwa wale wote waliokuwa wakifanya naye kazi enzi hizo ndio mafisadi wakubwa ambapo wengine wameshaanza kufikishwa mahakamani leo hii.....Wale waliokuwa wakilalamika na kufanya kila wanaloweza kummaliza ndio hao hao ambao wameprove kuwa mafisadi wakubwa kwenye Taifa letu.
 

- Mushi, cheo cha Mrema, hakikuwa na anything to it kikatiba kwa hiyo asingeweza kupambana na fisadi yoyote kwa kutumia cheo kisichokuwa kwenye katiba ya jamhuri, kama Mwinyi alikua na nia kweli ya unayoyasema basi angeomba ammendment bungeni kwanza ili aweze kumu-accomodate Mrema na hicho cheo kisheria,

- Mrema, alipewa hiki cheo na Kolimba ili kumpunguza ambitions za urais, lakini walipoona Mrema, haelewi ndio wakaweka ishu ya Degree kwanza kua rais.

Respect.

FMEs!
 
Alikuwa jasiri lakini pia kuna wana usalama wengi waliokuwa nyuma yake. Nasikia hata Marehemu Imran Kombe aliyekuwa mkurugenzi wakati huo
 
This mada iz too past oriented, ila mrema anajua afanyacho. Juz kati nilienda bush. Kule kampeni zimechemka si kitoto, na mwakani anachukua ubunge. Bara2 kaipiga greda kitu ambacho mh. Kimaro hakuwahi kufikiria
 

Jmushi1:

Sikatahi kama kuna moral obligations. Lakini kusubiri kupata Kiongozi mwenye Moral obligations ni sawa na kucheza bahati nasibu. And the chances are you won't get one.

Kwa mfano ukichukua Buzwagi, EPA, Richmond ni vitu ambavyo vingeweza kufanyika kwa ufanisi zaidi bila kujali moral obligations za wahusika iwapo tu taratibu za kutangaza tenda, account na procurements zingekuwa transparent.

Vilevile ukumbuke masuala ya moral obligations ni personal level. Masuala ya personal level hayarithishwi kwa vizazi vinavyokuja. Na kama yanarithishwa basi watanzania wengi wangerith moral values za mwalimu Nyerere na nchi yetu ingekuwa mswanu.

Wengine mashuleni tulifundishwa siasa kuanzia darasa la tatu mpaka Chuo. Tulikwenda majeshi lakini tuyatendao hayafanani na mafunzo yetu.

Hivyo short cut ni kuchungana tu. Kwa mfano rais akiteua mtu kuwa waziri, basi bunge limpigie kura. Ardhi inayokuwa alocated kwa investment kama uchimbaji wa madini au mbuga zipitishwe na bunge.

Vitu hivi sio rocket sayansi na moral obligation iwe extra credit.
 


Kwa maoni yangu binafsi cheo cha naibu waziri mkuu ni cheo ambacho hakiitaji kufafanuliwa kikatiba. Ni cheo kinachotumika kuonyesha seniority katika kabinet.

Ni waziri mkuu pekee yake ambaye amefafanuliwa vizuri kikatiba. Katiba yetu hajafafanua miundo ya wizara na nani aongeze wizara hizo. Hiyo ni kazi ya Rais na waziri mkuu.

Tumeshawahi kuwa na mawaziri wasio na wizara maalumu. Na wakati Salimu ni Naibu waziri mkuu, Warioba alikuwa Waziri Mkuu.

Warioba ni mwanasheria na alishawahi kuwa mwendesha mashtaka. Kama Warioba na uzoefu wake wa sheria aliweza kukubali Salim kuwa Naibu Waziri mkuu, sioni sababu ya kuenguliwa Mrema kwenye nafasi.

Kwa upeo wangu naona Mrema alikuwa aivi na mawaziri wenzake. Msuya asingeweza kukubali Mrema kuwa Naibu wake.
 
Kwa upeo wangu naona Mrema alikuwa aivi na mawaziri wenzake. Msuya asingeweza kukubali Mrema kuwa Naibu wake.

Zakumi,

Si uwe mkweli na muungwana kwa kusema Mpare hakutaka kuona Mchaga akiwa akimhemea.. kwi kwi kwi Taa Nyepesi!
 
Zakumi,

Si uwe mkweli na muungwana kwa kusema Mpare hakutaka kuona Mchaga akiwa akimhemea.. kwi kwi kwi Taa Nyepesi!

Uwa sipendelehi kuvinjari sana kwenye mambo ya makabila. Hila kusema kweli Mrema aliweza kuji-connect vizuri sana na watu walalahoi.

Alikuwa anafanya vile walalahoi walivyotaka. Na sio vilivyoandikwa vitabuni. Labda tungemfuata, tungewatia ndani waharifu kwanza na baadaye tukatunga sheria.

Sasa hivi inakuwa vigumu kufanya chochote cha maana. Polisi anakula rushwa. Ukifika mahakama hakimu naye anataka kitu kidogo. Mwendesha mashitaka naye yupo tayari kupeleka kesi mbovu akikatiwa kitu kidogo.
 
Zakumi,Rev.Kishoka,

..namkumbuka Mrema na harakati zake za ulinzi wa sungusungu DSM. sijui kwani Watanzania tunahitaji mtu aliyelazimisha waalimu, madaktari, yaani watu na proffesions zao, walinde sungusungu.

..wakati mnasema Msuya alikuwa hayuko tayari Mrema kuwa Naibu wake, je mmewahi kugeuza swali na kuuliza kama Mrema alikuwa tayari kufanya kazi na kupokea maagizo toka kwa Msuya?

..vilevile Mrema alikuwa 'Naibu Waziri Mkuu' wakati wa Malecela. sasa kuna vipindi Waziri Mkuu anakuwa hayupo na inabidi nafasi yake ikaimiwe. Je, Mrema alishapata kupewa nafasi ya kuwa Kaimu Waziri Mkuu?

..pia ni sababu zipi zilizomfanya Mwinyi asimpandishe cheo Mrema kuwa Waziri Mkuu kamili wakati alipolazimika kumuondoa Cygwiyemwisi John Malecela ktk nafasi hiyo?


NB:

..Katiba yetu imefafanua Waziri Mkuu, Waziri, Naibu Waziri, Waziri wa Nchi. Katiba haijafafanua nafasi ya Waziri Mkuu.

..TATIZO SI MREMA KUTEULIWA KUWA 'NAIBU WAZIRI MKUU.' TATIZO NI MREMA KUSHANGAZWA NA KUCHUKIZWA NA MWANASHERIA MKUU ALIYEMWELEKEZA KWAMBA NAFASI HIYO HAIPO KIKATIBA NA HAITAMBULIWI KISHERIA.

..Mrema pia aliwahi kudai kwamba, kwasababu yeye ni Waziri wa "Mambo ya Ndani," basi anahusika na ana mamlaka na kila jambo linalotokea nchini bila kujali kama anaingilia utendaji wa mawaziri wenzake.
 
wote ni wezi tu. huyu ni pandikizi tu anakula mshara kotoka CCM ile awavuruge wapinzani.
 
Joka Kuu,
He was very right, kama corruption au wizi ikitokea Wizara ya fedha moja kwa moja yeye anahusika; what he had to get was only an official search warrant.
 
Swahiba,
Hapa naweza kusema kama ni ngumi basi umenikosakosa, ingekuwa ana kwa ana basi ingekuwa balaa! Lakini ungechukua picha kubwa hungenisuta kiasi hicho. Maana picha yangu kubwa ni kuwa; baada ya Mrema kushika ule wizi alifanya kile ambacho kilitakiwa. Mkuu wa nchi alipishana na Mawazo ya Mrema. Kweli hii ndiyo sababu kubwa kuwa Mrema ilibidi ahame Chama.

Kuhusu kumfuata Nyerere, Gosh! Nyerere was not an enemy; he has been a friend to everybody who liked him or his advise, he was a friendly and a serious man. Political affiliation is not always enemity. Nyie ndiyo mnashangaa kuona kuwa alimfuata Nyerere. Na ndiyo maana hadi leo wengine mnafikiri kuwa Lowasa ni adui wa Kikwete. These are politics. Learn

Kuhusu nyie watoto wa mjini sawa kabisa, si na yule mzee wa Trianon, wenzetu mliwahi, lakini usiwe na usongo kuona ingawa kutangulia sio kufika. Wewe discuss points, kama wa mjini au wa shamba hiyo shauri yako.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…