Rev. Kishoka:
Si kweli kabisa kuwa waafrika wanapenda prestige za USOMI. Kumbuka kuwa Mrema alikuwa mbunge wa kuchaguliwa. Na kama sikosehi alikuwa mbunge wa Kutoka mkoa wa Kilimanjaro.
Kilimanjaro ni mkoa unaongoza kwa kutoa wasomi. Lakini pamoja na hayo alichaguliwa kuwa mbunge.
Mzee Mwinyi naye hakuogopa kumpa uwaziri wa mambo ya ndani. Hivyo, ndugu Mrema alikuwa one step away kuwa President.
Kwa mujibu wa katiba yetu. Waziri mkuu, spika na mawaziri ni wabunge. Na mbunge yoyote yupo karibu sana na kushika madaraka ya uwaziri mkuu, uspika, uwaziri mpaka urais. Kichotakiwa ni bahati, jinsi ya kuchanga karata na personality.
Mrema ana strength zake kama charisma na guts. Lakini ana kasoro zake kama kutokuwa msikivu, kutofuata ushauri, kutokuwa na elimu.
Na kwa kipindi alichokuwa maarufu alishindwa tools za ku-minimize weakness zake.
Katiba ya Tanzania inasema mtu anaweza kuwa Rais kama anajua kusoma na kuandika, na hi ni kutokana na kuwa na sifa za kuwa mbunge haisemi lolote kiwango cha elimu!
67
.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu
yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa
kuwa Mbunge endapo-
(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa
miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na
kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama
yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote
ya Serikali.
39
.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika
Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa
kodi yoyote ya Serikali.
So elimu ya juu is a plus but not a requirement per Katiba. CCM that was their preference kubadili katiba na kudai lazima mtu awe na Shahada ya chuo, na guess what, kila mtu kajiendea hata katika vyuo tunavyodai kuwa havina credibility na wamejipatia Shahada mpaka Udaktari!
Hata wewe na mimi na Bwana Mkandara tunaweza kuwa Rais wa Tanzania. Tunachohitaji kuwa nacho ni uwezo wa kuwa watu wa haki na kufuata kanuni (this does not need PHD), zaidi tuwe na busara, hekima, unyenyekevu na wachapakazi (this also does not need a degree).
Maamuzi hufanywa kwa kuaminiana. Ndio maana Rais ana washauri na wasaidizi katika kila nyanja, Sheria, Uchumi, Afya, Siasa, Utamaduni, Biashara, Utawala, Demokrasia, Ulinzi na Usalama na mengineyo.
Kila Rais wa Tanzania ana watu hao ambao ni wataalamu kisomi wa fani hizo, ambao wako kwenye ofisi yake, halafu kuna watendaji wa kazi ambao ni Mawaziri ambao ni Wanasiasa kama Rais, nao wana Makatibu wakuu, wakurugenzi na wafanyakazi wengine ambao ni wasomi na wana utaalamu katika fani zao kutimiliza majukumu na kazi zao.
Narudia kuuliza, kama Elimu ya Chuo Kikuu ni tija, kwa nini mfupa umemshinda Mkapa na Kikwete?
Kama katika mwaka wa Kwanza wa Mchumi Kikwete aliamua kuongeza ukubwa wa Serikali kama njia ya kutoa shukrani kwa kisingizio cha kuleta usawa wa kikabila, kimkoa na kidini ndani ya Baraza la Mawaziri na hivyo kuongeza gharama na matumizi, je Uchumi na usomi wake ulikuwa na maana gani?
Na si hilo tuu la gharama na matumizi, bali kukosekana kwa juhudi za kuhakikisha kuna uchapakazi na uwajibikaji.
Ikiwa mchumi kama yeye anadai kuwa hajui kwa nini Tanzania ni masikini, je Usomi wake una maana gani ikiwa Mdengereko na Mfipa wakiangalia mbingu wakaona anga halina mawingu wanajua kuwa hakuta kuwa na mvua na hivyo mavuno yatakuwa haba?