Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!

Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!

Hivi Mrema alifanya kipi cha maana haswa maanake mimi sielewi?..
Your Answers:
1. He was the first Minister to catch a bust of Gold belonging to the President spuase and telling the President I can't bow! "You're corrupt". And he quit his position as a Deputy Prime Minister!
2. What did Mkapa or Kikwete achieve before being a President? At least we saw what Mkapa did, the macros, the country was in shit before him. What does this present guy doing what Mrema couldn't accomplish?
3. WE are judging the guy; but we fail to know in a country like Tanzania, if at that time Mwl Nyerere had backed Mr. Mrema then he could be our President.
There are more factors than these factors; we in Tanzania are in a different world, and don't forget we are in Africa.
 
Lula wa Brazil si msomi, na nchi yake iko katika nchi kumi zenye uchumi bora duniani.

Eva Morales wa Bolivia si msomi lakini anaendesha nchi na kinaeleweka.

Ni Waafrika pekee tunaopenda Prestige za Usomi kama vile ni tija na njia ya kuleta maendeleo!

Rev. Kishoka:

Si kweli kabisa kuwa waafrika wanapenda prestige za USOMI. Kumbuka kuwa Mrema alikuwa mbunge wa kuchaguliwa. Na kama sikosehi alikuwa mbunge wa Kutoka mkoa wa Kilimanjaro.

Kilimanjaro ni mkoa unaongoza kwa kutoa wasomi. Lakini pamoja na hayo alichaguliwa kuwa mbunge.

Mzee Mwinyi naye hakuogopa kumpa uwaziri wa mambo ya ndani. Hivyo, ndugu Mrema alikuwa one step away kuwa President.

Kwa mujibu wa katiba yetu. Waziri mkuu, spika na mawaziri ni wabunge. Na mbunge yoyote yupo karibu sana na kushika madaraka ya uwaziri mkuu, uspika, uwaziri mpaka urais. Kichotakiwa ni bahati, jinsi ya kuchanga karata na personality.

Mrema ana strength zake kama charisma na guts. Lakini ana kasoro zake kama kutokuwa msikivu, kutofuata ushauri, kutokuwa na elimu.

Na kwa kipindi alichokuwa maarufu alishindwa tools za ku-minimize weakness zake.
 
So after all he needed Nyerere's backing to become president.
 
- Mkuu nimefika mahali sasa umenipoteza, katika miaka 45 ya uongozi wa taifa letu viongozi walikua wamefungwa midomo, suddenly ametokea rais wa kuwafungulia midomo and the first thing wanatakiwa kuanza na yeye badala ya kuisafisha system kwanza?

- Eti JF tunaweza kuwapangia strategy wapiganaji? Labda kuwapa ushauri tu so far they are on the right track, na wamefanikiwa kubadilisha mienendo mingi sana ya bunge kwa manufaa ya wananchi, kwa mfano siku hizi shughuli yoyote inayoihusu serikali ikibidi kufanyika nje ya nchi, ni lazima balozi yetu ihusishwe na nchi inayotakiwa kufanyika shughuli hiyo, matokeo yake ni kwamba ile tabia ya baadhi ya viongozi wetu kusaini mikataba mahotelini huko majuu, hakuna tena,

- Kiwira tayari iko njiani kurudi mikononi mwa wananchi, I mean a lot to show for katika kipindi kifupi sana as opposed na Mrema, ambaye hakuna anything cha kuonyesha zaidi tu ya Mrema, Mrema na Mrema, mkuu ukiona kiongozi anatoka sehemu ya uongozi halafu kila kitu kina-fall apart basi huyo sio kiongozi anayefaa ila ni mbinafsi, kama kweli Mrema alifanya mnayosema alifanya basi yangekua yanaendelezwa hadi leo, angalau hata Keeenja ana nafuu sana maana aliyoyafanya City yanafahamika.

- Huenda wapiganaji hawaendi kwa speed unayoitaka, lakini haraka haraka haina baraka mkuu.

Respect.

FMEs!

FMES,

Wewe unakaa Marekani, kwa nini presure groups kama Moveon. Org, na watu kama Rush Limbaugh, Glenn Beck, Bill Maher, Chris Matthews, Bill O'Reily wana msukumo wa nguvu kiasi cha kuangusha Wabunge wa Marekani hata Rais wa Marekani halafu udai kuwa JF haina nguvu hizo au kuainisha kuwa Tanzania ni Mbuge pekee mwenye uwezo?

Hivi leo hii tukiachana na mapenzi yetu kwa watu fulani fulani na uanza kuwadai uwajibikaji mmoja mmoja na kwenda majimboni mwao, unafikiri ni nini kitatokea?

Wabunge wa Tanzania hawana watu ambao ni diversed pool of brains kama JF ilivyo. Hapa you name it, kila watu wapo na wanaweza kumpangia mtu strategy nzuri sana.

Kama huamini, chunguza vizuri sana SSM na Serikali yake pamoja na kujifanya wanachukia JF. Wengi wao wanajifunza hapa kutoka kwa Wana JF mbalimbali hata kama mara ingine tunamwaga upupu. Guess what, CCM wamepevuka kwa kusoma nyakati na kutumia kinachosemwa humu kujijenga.

Upinzani ambao ulitarajiwa uwe upande mmoja na JF kwa kuwa lengo ni kukosoa Serikali, wao badala ya kufanya transformation na kutumia strategies na ideas zinazomwagwa humu ndani, wamebakia na Ubuntu wa kujiona wao ni mali na ndio maana wanapigwa mweleka kila mara especially CHADEMA!

So do not under estimate our power and our strength, maana kama si sisi, hao Wapiganaji wasingekuwa na ammo za kupigana!

Hivyo basi, kama Rush Limbaugh na Bill Maher, sisi huku ndani ambao tunaona mambo yankwenda kinyume na inavyopaswa kufanyika na kule kujivutavuta kisa eti bado nchi changa, iko siku tutachoshwa kutumiwa na na kunyonywa juhudi zetu za kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu uajibikaji na rurawageukia hao wawakilishi majimboni mwao na kuwahoji wamefanya nini la maana tangu wapewe kura za wananchi kuleta maendeleo majimboni mwao.

Nimesema katika vita hii, kama Wapiganaji wanataka kufanikiwa, kwanza ni kumjengea Mtanzania mazingira ya kuwa huru kwa kusukuma maendeleo yatakayoinua hali ya maisha ya Mtanzania ambaye akishaweza kujitegemea na kuridhika, atapanuka mawazo na kuweza kuachana na woga na unyonge wa kuwa mtegemezi wa misaada na hongo na ataamua kwa haki na utu ni nani anafaa kupata kura yake na si nani aliyeleta Pilau na Gagulo!
 
Rev. Kishoka:

Si kweli kabisa kuwa waafrika wanapenda prestige za USOMI. Kumbuka kuwa Mrema alikuwa mbunge wa kuchaguliwa. Na kama sikosehi alikuwa mbunge wa Kutoka mkoa wa Kilimanjaro.

Kilimanjaro ni mkoa unaongoza kwa kutoa wasomi. Lakini pamoja na hayo alichaguliwa kuwa mbunge.

Mzee Mwinyi naye hakuogopa kumpa uwaziri wa mambo ya ndani. Hivyo, ndugu Mrema alikuwa one step away kuwa President.

Kwa mujibu wa katiba yetu. Waziri mkuu, spika na mawaziri ni wabunge. Na mbunge yoyote yupo karibu sana na kushika madaraka ya uwaziri mkuu, uspika, uwaziri mpaka urais. Kichotakiwa ni bahati, jinsi ya kuchanga karata na personality.

Mrema ana strength zake kama charisma na guts. Lakini ana kasoro zake kama kutokuwa msikivu, kutofuata ushauri, kutokuwa na elimu.

Na kwa kipindi alichokuwa maarufu alishindwa tools za ku-minimize weakness zake.

Katiba ya Tanzania inasema mtu anaweza kuwa Rais kama anajua kusoma na kuandika, na hi ni kutokana na kuwa na sifa za kuwa mbunge haisemi lolote kiwango cha elimu!

67​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu
yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa
kuwa Mbunge endapo-
(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa
miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na
kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama
yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote

ya Serikali.

39​
.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika
Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa

kodi yoyote ya Serikali.

So elimu ya juu is a plus but not a requirement per Katiba. CCM that was their preference kubadili katiba na kudai lazima mtu awe na Shahada ya chuo, na guess what, kila mtu kajiendea hata katika vyuo tunavyodai kuwa havina credibility na wamejipatia Shahada mpaka Udaktari!

Hata wewe na mimi na Bwana Mkandara tunaweza kuwa Rais wa Tanzania. Tunachohitaji kuwa nacho ni uwezo wa kuwa watu wa haki na kufuata kanuni (this does not need PHD), zaidi tuwe na busara, hekima, unyenyekevu na wachapakazi (this also does not need a degree).

Maamuzi hufanywa kwa kuaminiana. Ndio maana Rais ana washauri na wasaidizi katika kila nyanja, Sheria, Uchumi, Afya, Siasa, Utamaduni, Biashara, Utawala, Demokrasia, Ulinzi na Usalama na mengineyo.

Kila Rais wa Tanzania ana watu hao ambao ni wataalamu kisomi wa fani hizo, ambao wako kwenye ofisi yake, halafu kuna watendaji wa kazi ambao ni Mawaziri ambao ni Wanasiasa kama Rais, nao wana Makatibu wakuu, wakurugenzi na wafanyakazi wengine ambao ni wasomi na wana utaalamu katika fani zao kutimiliza majukumu na kazi zao.

Narudia kuuliza, kama Elimu ya Chuo Kikuu ni tija, kwa nini mfupa umemshinda Mkapa na Kikwete?

Kama katika mwaka wa Kwanza wa Mchumi Kikwete aliamua kuongeza ukubwa wa Serikali kama njia ya kutoa shukrani kwa kisingizio cha kuleta usawa wa kikabila, kimkoa na kidini ndani ya Baraza la Mawaziri na hivyo kuongeza gharama na matumizi, je Uchumi na usomi wake ulikuwa na maana gani?

Na si hilo tuu la gharama na matumizi, bali kukosekana kwa juhudi za kuhakikisha kuna uchapakazi na uwajibikaji.

Ikiwa mchumi kama yeye anadai kuwa hajui kwa nini Tanzania ni masikini, je Usomi wake una maana gani ikiwa Mdengereko na Mfipa wakiangalia mbingu wakaona anga halina mawingu wanajua kuwa hakuta kuwa na mvua na hivyo mavuno yatakuwa haba?
 
3. WE are judging the guy; but we fail to know in a country like Tanzania, if at that time Mwl Nyerere had backed Mr. Mrema then he could be our President.

God forbid! Na kwa hili daima nitamshukuru Nyerere.

Amandla........
 
Mkuu FMES respect...unajuwa walioibua suala la miakataba kusainiwa hotelini ni mashujaa wa upinzani wakiongozwa na dr slaaa, pamoja na mashujaa wa hapa JF....Waliotoa intelligence support and doziers...

Alichofanya kikwete ni kutumia akili ya kisiasa ...waswahili tunasema ,mchawi mpe mwana alee....,".... alimteua mmoja ya wapinzani aliyeshiriki kuwasulubu bungeni zittt kabwe....nadhani pale kikwete alitaka kuizima hii hoja kisiasa ..na ndio maana hoja ya buzwagi ni kama imekufa ....na utekelezaji wa ripoti ya jaji bomani hatuuelewi...., na wapinzani kuliongelea hawawezi tena ....kwani waziri atawapa jibu rahisi..."vuteni subira ...mlikuwa na wawakilishi wawili kwenye tume ya jaji ,...,waulizeni.

Hawa wapiganaji wa ccm ...ukweli ni kuwa wanapigwa vita sana ndani ya chama hata jk amekiri ...lakini wana ccm lazima kuelewa kuwa kama si wapiganaji hawa kupaza sauti wakiwa ndani basi CCM ilikuwa inakenda na maji .....kwani angalau sasa wananchi waeona kuwa kumbe hata ccm kuna wabunge wanawatetea...ndio maana upepo uendavyo kisiasa inaonekana kundi la mafisadi tayari limemtuma makamba kufanya ziara ya kuomba suluhu kwenye majimbo ya wapiganaji yaliyochafuliwa kama kwa sitta......ba kinafiki amewaomba wana tabora wahakikishe spika sitta anarudi bungeni na kumsifu kwingi.....tukielekea mwaka 2010 ...nadhani hata ..dizaini ya yule mbunge wa kigoma mjini wa ccm na wenzake wa aina hiyo chamani ambao wazi wanajulikana ni pro ufisadi ...watakiunga na vita ya kupinga ufisadi ili wawe na ajenda ya kushinda......mwakani ....
 
Lula wa Brazil si msomi, na nchi yake iko katika nchi kumi zenye uchumi bora duniani.

Eva Morales wa Bolivia si msomi lakini anaendesha nchi na kinaeleweka.

Ni Waafrika pekee tunaopenda Prestige za Usomi kama vile ni tija na njia ya kuleta maendeleo!

Lula aliikuta nchi ikiwa tayari iko juu!

Eva Morales- the jury is still out.

Usomi ukitumika vizuri una faida yake. Lee Kuan Yew wa Singapore ni mfano. Shule inasaidia lakini si panacea.

Tunahitaji mtu mwenye vision, mwenye committment, mwenye integrity, mwenye empathy. Mtu ambae anaweza kutuambia na tukamuelewa ukweli kuhusu hapo tulipo na mtu atakaetuonyesha kwa vitendo kuwa sote tunaweza kutoka hapo tulipo. Hajapatikana bado huyo mtu.

Amandla........
 
Naomba kutoa hoja.

Hapa tuna demokrasia moja nzuri kabla ya vijembe kuanza na laiti vyama vyeetu vya siasa vikianza kutuiga kwa kuruhusu majadiliano ndani yao katiya wanachama wao yawe kama sisi.

Naomba kufafanua: Nimemleta Mrema na nimemjengea hoja na natetea hoja yangu. Kuna wanaounga mkono na kuna wanaopinga. Hii ni demokrasia.

Wanaounga mkono wanatoa sababu zao, wanaopinga wanatoa sababu zao, huu ni utaratibu mzuri na uungwana.

Sasa basi, ombi langu kwa wale wanaopinga na kusema Mrema hafai, naomba watupe majina ya watu wanaofikiri kwa mtazamo wao kuwa wanafaa kutuongoza au ni "Wazalendo" na Wapiganaji wa kweli, ili tuweze kuwachambua na kuwapima uwezo wao kuongoza.
 
FMES,

Naomba kurudi nyuma kwenye swali moja nililokuuliza na ukanijibu.

Niliuliza
FMES,

Let me reverse the order of your post above with my questions.
You have stated we need a strong leasder, any suggestioins that you have that we may start pampering and sell his/her name to public as we prepare for 2010 or even 2015? Can you list at least 5 people that you think are right people to lead Jamhuri right now?

Nduguyo Mchungaji.

Ukajibu
- Ni mapema mno kuanza kurusha majina arround, lakini wapo na ninaye one in mind ambaye binafsi tayari nimeshanza ku-invest in, lakini samahani ni mapema mno wasije wakaanza kupigwa mikwara.

FMEs!

Swali languni hili, tumebakiza mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi Mkuu kufanyika, lakini unasema ni mapema mno kwa unayempigia debe kufahamika.

Je mgombea wako hajajiandaa kukabiliana na pingamizi na uchambuzi juu ya haiba yake na uwezo wake wa kuongoza mpaka awasilishe fomu kwenye Chama alichoko May 2010?

Kwa nini una hofu na kutoamini kuwa ukitupa majina jampo kadha tuyachambue kuwa wagombea wako hawatavuma.

Mwisho, ukiachilia huyo mmoja ambaye ni spesheli, je hao wengine masalia unaweza kutupa majina na kuwajengea hoja kwa nini wawe Rais wa Tanzania?
 
FMES,

Naomba kurudi nyuma kwenye swali moja nililokuuliza na ukanijibu.

Niliuliza

Ukajibu
Swali languni hili, tumebakiza mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi Mkuu kufanyika, lakini unasema ni mapema mno kwa unayempigia debe kufahamika.

Je mgombea wako hajajiandaa kukabiliana na pingamizi na uchambuzi juu ya haiba yake na uwezo wake wa kuongoza mpaka awasilishe fomu kwenye Chama alichoko May 2010?

Kwa nini una hofu na kutoamini kuwa ukitupa majina jampo kadha tuyachambue kuwa wagombea wako hawatavuma.

Mwisho, ukiachilia huyo mmoja ambaye ni spesheli, je hao wengine masalia unaweza kutupa majina na kuwajengea hoja kwa nini wawe Rais wa Tanzania?

- Mchungaji, mgombea wangu nina hakika hawezi kushinda mwaka 2010, lakini ninaamini kwa 100%, kwamba atakapoingia 2015 hapatatosha, nitakuwa mwenda wazimu kujihusisha na kampeni za urais wa 2010 against Rais wa sasa, lakini ninasema hivi 2015 ni uwanja wa wazi kwa anybody,

- Na believe me I have been working my ass off on the project, toka mwaka jana nilipokaa naye chini kujadili hili la urais wa 2015, kwa mapana na marefu, itakuwa ni kampeni of the Century maana kuna wanaoamini kwamba Rais wa sasa atawapa bure tu, wasichoelewa ni kwamba by then atakua so weak that no one will pay him any mind.

- By then wananchi wa Tanzania watakuwa so careful kwamba hawatarudia makosa ya kumchagua kiongozi aliyelala, mkimya na ambaye hajawahi hata siku moja ku-take sides publicly na ishu controversial na serious kwa taifa letu, kama kina Salim, Mwandosya na Membe.

Mchungaji, subira yavuta heri mkuu!

Respect.

FMEs!
 
FMES,

Wewe unakaa Marekani, ![/QUOTE]

- Mchungaji sikai Marekani, na ni makosa makubwa sana ku-speculate location ya another member kwa sheria za JF, nikitaka kusema ninakoishi niache niseme mwenyewe,

- Si nilikuambia hua mnaanza wenyewe ya kunitafuta personal halafu nikijibu on the personal level hampendi, kwani Mchungaji hoja yako isingeeleweka bila ku-speculate my location?

- Ni lini umewahi kuniona niki-speculate location yako au ya member yoyote hapa mkuu? Unahitaji ku-apologize for this maana ni too low and uncalled for! I mean kwa nini siwezi kujadili hoja humu JF bila hizi lows za personal?

FMEs!
 
Your Answers:
1. He was the first Minister to catch a bust of Gold belonging to the President spuase and telling the President I can't bow! "You're corrupt". And he quit his position as a Deputy Prime Minister!

- Baada a kuzikamata then what was next? Hivi ni lini wa-Tanzania tutaweza kujadili ishus mpaka mwisho wa habari, siku zote huwa ni half truths tu,

- Sasa unakua shujaa kwa kuzikamata dhahabu za rais na kuziachia bila maelezo yoyote ya kisheria, halafu eti unajiuzulu cheo ambacho hakipo katika katiba ya Jamhuri, halafu kuna mnaosema hii comedy ni good enough to make Mrema a national hero, na hata a good president, I am missing something here or what?

- Eti Diria akiwa waziri wa nje, alipokuwa anapigwa stop kwenda Ujerumani kwa sababu ya kuhusika na madawa ya kulevya, Mrema alikuwa wapi? Si siku zote huyu alikuwa akiupitisha hapo hapo uwanja alikozikamata hizo dhahabu?

if at that time Mwl Nyerere had backed Mr. Mrema then he could be our President.

- Kiongozi maarufu kuliko wote at the time, akajitoa CCM ili aweze kuwakomboa wananchi, lakini tena akahitaji back up ya muanzilishi wa CCM ile ile aliyoikimbia kuwa rais wetu, what a national hero!

- Thank to God, kwamba Mwalimu was smart enough on this matter, ambapo alimshauri sana kugombea ubunge tu!

Respect.

FMEs!
 
Mkuu FMES respect...unajuwa walioibua suala la miakataba kusainiwa hotelini ni mashujaa wa upinzani wakiongozwa na dr slaaa, pamoja na mashujaa wa hapa JF....Waliotoa intelligence support and doziers...

Alichofanya kikwete ni kutumia akili ya kisiasa ...waswahili tunasema ,mchawi mpe mwana alee....,".... alimteua mmoja ya wapinzani aliyeshiriki kuwasulubu bungeni zittt kabwe....nadhani pale kikwete alitaka kuizima hii hoja kisiasa ..na ndio maana hoja ya buzwagi ni kama imekufa ....na utekelezaji wa ripoti ya jaji bomani hatuuelewi...., na wapinzani kuliongelea hawawezi tena ....kwani waziri atawapa jibu rahisi..."vuteni subira ...mlikuwa na wawakilishi wawili kwenye tume ya jaji ,...,waulizeni.

- Hapa tupo pamoja kwa 100%.

Hawa wapiganaji wa ccm ...ukweli ni kuwa wanapigwa vita sana ndani ya chama hata jk amekiri ...lakini wana ccm lazima kuelewa kuwa kama si wapiganaji hawa kupaza sauti wakiwa ndani basi CCM ilikuwa inakenda na maji .....kwani angalau sasa wananchi waeona kuwa kumbe hata ccm kuna wabunge wanawatetea...ndio maana upepo uendavyo kisiasa inaonekana kundi la mafisadi tayari limemtuma makamba kufanya ziara ya kuomba suluhu kwenye majimbo ya wapiganaji yaliyochafuliwa kama kwa sitta......ba kinafiki amewaomba wana tabora wahakikishe spika sitta anarudi bungeni na kumsifu kwingi.....tukielekea mwaka 2010 ...nadhani hata ..dizaini ya yule mbunge wa kigoma mjini wa ccm na wenzake wa aina hiyo chamani ambao wazi wanajulikana ni pro ufisadi ...watakiunga na vita ya kupinga ufisadi ili wawe na ajenda ya kushinda......mwakani ....

- Very strong mkuu, sina kuongeza wala kupunguza.

Respect.

FMEs!
 
Naomba kutoa hoja.

Hapa tuna demokrasia moja nzuri kabla ya vijembe kuanza na laiti vyama vyeetu vya siasa vikianza kutuiga kwa kuruhusu majadiliano ndani yao katiya wanachama wao yawe kama sisi.

Naomba kufafanua: Nimemleta Mrema na nimemjengea hoja na natetea hoja yangu. Kuna wanaounga mkono na kuna wanaopinga. Hii ni demokrasia.

Wanaounga mkono wanatoa sababu zao, wanaopinga wanatoa sababu zao, huu ni utaratibu mzuri na uungwana.

Sasa basi, ombi langu kwa wale wanaopinga na kusema Mrema hafai, naomba watupe majina ya watu wanaofikiri kwa mtazamo wao kuwa wanafaa kutuongoza au ni "Wazalendo" na Wapiganaji wa kweli, ili tuweze kuwachambua na kuwapima uwezo wao kuongoza.

Rev Kishoka:

Huu sio ushabiki wa mpira kwamba kama nafasi nzuri aliyoshindwa Zamoyoni Mogella kufunga goli, basi Kibadeni angeweza.

Hivyo mjadala ni kuhusu Mrema. Na tunamjadili kuhusiana na nafasi zake alizowahi kushika, jinsi alivyo-capitalize hizo nafasi, mchango wake kwa taifa na pale alipo sasa.

Wengi wetu tunaopinga AUGUSTINO LYATONGA MREMA, hatufanyi hivyo kwa sababu kuna kiongozi anayefanya kazi nzuri kuliko MREMA. Na vilevile hatufanyi hivyo kutafuta KIONGOZI MWINGINE mwenye sifa za MREMA.

Wengi wetu tumefikia kwenye conclusion kuwa juhudi za kufatuta kiongozi ambaye atakuwa na charisma na guts za MREMA, au kiongozi hatakayekuwa sio fisadi kwa hiari kama NYERERE, hazisaidia taifa in long terms.

In long term, taifa ni lazima liwe na system nzuri ya utawala wa kikatiba ambao utamwezesha hata asiye na Elimu kutawala kama Professor. Na Fisadi kuongoza kama malaika.
 
Rev Kishoka:

In long term, taifa ni lazima liwe na system nzuri ya utawala wa kikatiba ambao utamwezesha hata asiye na Elimu kutawala kama Professor. Na Fisadi kuongoza kama malaika.
That is the best quote of the day. Kama alivyosema Obama Ghana, Africa does not need strong men. It needs strong institutions.
 
Interesting Observer,
Your Answers:
1. He was the first Minister to catch a bust of Gold belonging to the President spuase and telling the President I can't bow! "You're corrupt". And he quit his position as a Deputy Prime Minister!

Mkuu Unajua hakuna kitu kibaya duniani kama kutunga vitu...Umezungumzia Mrema kwa sifa ambazo hazikuwepo hata kidogo...huu ni uzushi mkubwa kwa sababu Mrema hakujiuzuru toka Deputy Prime Minister...Mrema baada ya hapo alipelekwa wizara ya kazi (1994-95)ambako alifanya kazi kwa mwaka..sielewi hii habari ya kujiuzuru kwake umeitoa wapi! Mrema kaondoka CCM ama uongozi mwaka 1995 kujiunga na NCCR, mwaka ambao Mwinyi alikuwa anamalizia ngwe zake iweje leo wewe uje hapa na story za kutunga ati alimwambia Mwinyi hawezi ku bow!..
Je, sii huyu Mrema aliyekwenda Butiama kumwona Nyerere kabla hajajitoa CCM na kujiunga na NCCR Mageuzi? au Mrema mwingine! Why ikiwa kweli alikuwa na msimamo wake binafsi why kwenda kumwona Nyerere Butiama kupata baraka zake!
Mkuu sisi watoto wa mjini tunayajua mengi yalliyofanyika mjini pale wakati wa Mrema ambayo wewe huyajui na wala hutayajua.. Akiwa Waziri wizara ya mambo ya ndani, Airport yetu ilikuwa pathway ya magendo yote unayoweza kufiiiria wewe tena inasemekamna hata mkewe Mwinyi aliingia biashara haramu.. Nani sitamtaja hapa kwani sina ushahidi mkononi..
 
- Bob ndio maana nilisema hivi in the absence of mashujaa, labda Mrema ndio anaweza kuwa shujaa. I mean alijiuzulu cheo ambacho hakitambuliwi na katiba ya Jamhuri?

- Sasa unaona madhara ya kukosa elimu, angekua nayo walipompa angekataa kwamba siwezi kushika cheo kisichokuwepo kwenye katiba, lakini yeye akakkubali tu tena bila hata kuapishwa na rais, kwamba yeye ni naibu waziri mkuu, no wonder Msuya waziri mkuu mpya alikifuta bila kumfahamisha.

mkuu hata salim ambaye mimi binafsi namuheshimu na namuona kama ndiye aliyestahili kuitwa rais leo...alipata kupewa na mwinyi cheo cha NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA ULINZI [CHINI YA WARIOBA]...KABLA HAJAENDA OAU...na hakukataa ..

kukikubali hicho cheo ni heshima tu!!!
 
Back
Top Bottom