Augustino Mrema: Behind the Scene

Utaratibu wa one to one ilikuwa ubunifu mzuri sana, na alihakikisha akilianzisha analimaliza ! Hivi kuna waziri unaweza kumuona one to one !?
 
ni mtu pekee aliyempigia debe mgombea wa urais wa ccm badala wa chama chake!ni bogus mwenye njaa kali
 
Ni mbunge mmojawapo baada ya kushinda akachukua wapishi wakapika pilau akawaita akina mama wa vunjo wakasherekea na mbege ya kutosha sijui aliipata wapi mzee yule.
Mamndenyi 'shimbonyi shafo monoama'
 
Ni waziri pekee aliyekuwa anaingilia maamuzi wa wizara zingine,
Aliamuru wenye maduka kupanda miti mbele ya maduka yao na kulazimisha wahindi
wa mtaa wa Samora na uhuru dar kutoboa velanda za zege ili wapande miti na alifanikiwa.
 
ukweli ni kwamba viongozi wetu wanatakiwa sana kuiga yale mazuri aliyokua anayafanya Dr L mrema,
kazi alizofanya hadi kesho zitakumbukwa,
 
nyabhingi
tatizo lako mtu kama wewe unaona mabaya ya mtu tu.altho wewe unamuona bogus bt kunamambo mengi katika utendaji wa viongozi wetu wa sasa wameshidwa kuyasimamia ila yeye akiwa madarakani na waziri aliweza kutetea mali za watanzania dhidi ya viongoz mafisadi miaka hiyo.

yapo mengi sana ya kujifunza kwa huyu unayemwita bogus.
 
Ni mtu pekee aliyetunza NISSAN patrol yake kwa mda mrefu sana
 

aliwahi pia kuwa mbunge wa moshi vijijini na tutamkumbuka daima almost barabara zote za moshi vijijini alizijenga kwa kiwango cha changarawe, na kuhakikisha vijiji vingi vinapata umeme na maji ya uhakika he is a HERO kwa kweli.
 
Alisimamia bei ya kahawa ikapanda hadi Tshs 1400 kwa kilo,
Kiaina ameanza pia kuikubali M4c,
 
Yeye na mbowe ni wenyeviti walioshindwa biashara ya jumla yaan urais na kuamua kufnya biashara ya rejaa reja yaaan ubunge
 
Ni kweli Dr A L Mrema ni aina ya kiongozi wa kuigwa mfano mambo mengi aliyoyafanya yanaonekana mpaka leo ukimwondoa Sokoine na sasa Dr Magufuli Tanzania haijapata kiongozi [waziri] mfuatiliaji na mtekelezaji kama Mzee wa Kiraracha.

Naamini A Mwanri naibu waziri OWM akipewa nafasi anaweza kushangaza watu.
 
Naendelea...
1. Ndiye muasisi wa dhana nzima ya 'polisi
jamaa' akiita 'sungu sungu'..mzaz gan
ambaye hakuwah kuwa mlinz kipnd kle?
2. Kiongoz pekee mwenye uwezo wa
kuzururura usiku akiwa na kibukta katika
maeneo ya madada poa na wachoma
nyas..ili kutengeneza 'pschological unrest
ili waache uhalifu!
 
Ni mtu wa Pili kupewa cheo cha Naibu waziri mkuu [na waziri wa mambo ya ndani] ...ikumbukwe kuwa wa kwanza kupewa cheo hiki ni SALIM AHMED SALIM ....baada ya mwinyi kuingia madarakani alimtafutia cheo cha Naibu Waziri Mkuu Na Waziri Wa Ulinzi...alikifanya kwa mwaka mmoja tu kabla ya kuwa seconded OAU kuwa katibu mkuu wa OAU.......
 

Hapo kwenye bold, lazima tumkumbuke kwamkuanzisha ulinzi huo, ambapo kwa kiasi kikubwa ulipunguza uhalifu sana mijini. Nakubaliana na anayesema Mrema alikuwa "Result Based". Enzi zake ilikuwa akifuatilia kitu lazima jibu litoke, sio hawa mawaziri longolongo wa sasa.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…