Mkuu nakubaliana na wewe kiasi ila jeshi la sungusungu lilikuwepo toka enzi za vijiji vya ujamaa miaka ya 70 likafifia, sema Mrema likuja kulifufua upya miaka ya 80 alipokuwa waziri wa mambo ya ndani.Naendelea...
1. Ndiye muasisi wa dhana nzima ya 'polisi
jamaa' akiita 'sungu sungu'..mzaz gan
ambaye hakuwah kuwa mlinz kipnd kle?
2. Kiongoz pekee mwenye uwezo wa
kuzururura usiku akiwa na kibukta katika
maeneo ya madada poa na wachoma
nyas..ili kutengeneza 'pschological unrest
ili waache uhalifu!
- Ni mtu pekee ambaye amekuwa mbunge katika majimbo mawili tofauti. Alikuwa mbunge wa Jimbo la Temeke mkoani Dar Es Salaam mnamo mwaka 1996 baada ya mahakama kutengua ubunge wa Ally Kihiyo, ambaye alighushi elimu yake katika wasifu wake, na kwa sasa Mrema ni mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro
mkuu mamdenyi inaelekea tumetoka sehemu moja, mbonyi mbee
hii naikumbuka ilikua saaafi saanaNi waziri pekee aliyekuwa anaingilia maamuzi wa wizara zingine,
Aliamuru wenye maduka kupanda miti mbele ya maduka yao na kulazimisha wahindi
wa mtaa wa Samora na uhuru dar kutoboa velanda za zege ili wapande miti na alifanikiwa.
Amina mkuuna wuro meeku,
mimi nilipita hiyo njia nikiwa naenda kilema kuchukua mwili wa mzee wangu
ndo nikaipata hiyo, ila kwetu ni kumoja mkuu.
Nendeni mkajifunze kiswahili upya jamani lol, hamua=amua, hacha=acha, hogopa=ogopa.......mko wengi na mnakera sana.
Mnyonge Mnyongeni, lakini haki yake mpeni.
Katika kikao cha saba cha bunge lilohitimishwa jana, kamati yake ya Hesabu za serikali a mitaa ilitoa ripoti moja nzuri sana juu ya ubadhirifu mkubwa ulioonekana katika serikali za mitaa. Kamati yake, tofauti na kamati nyingine za bunge, ilithubutu kutaja kwa majina na mahali walipo wahusika wa ubadhirifu wa mali za halmashauri na kutoa mapendekezo mazuri sana ya hatua za kuchukua dhidi ya wahalifu hao na namna ya kuzuia wizi huo kwa siku zijazo. Mheshimiwa huyu aliongea kwa uchungu sana namna anavyoumizwa na wizi huu, huku huduma za kijamii zikizorota kwa kukosa pesa.
Behind the Scene (vibwagizo)
- Mrema ni mtu pekee ambaye amewahi kupewa cheo kisichotambulika katika katiba ya nchi (Naibu waziri Mkuu), enzi za mzee Ruksa. Enzi hizo pia alikuwa ni waziri wa mambo ya ndani na utendaji wake ulijulikana sana.
- Ni mtu pekee ambaye amekuwa mbunge katika majimbo mawili tofauti. Alikuwa mbunge wa Jimbo la Temeke mkoani Dar Es Salaam mnamo mwaka 1996 baada ya mahakama kutengua ubunge wa Ally Kihiyo, ambaye alighushi elimu yake katika wasifu wake, na kwa sasa Mrema ni mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro
- Ni mtu pekee ambaye amekuwa mwenyekiti wa vyama viwili tofauti vya kisiasa kwa nyakati fofauti na amegombea uraisi kupitia vyama hivi viwili tofauti. Alikuwa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mnamo mwaka 1995 enzi hizo Mabere Marando akiwa katibu mkuu na aligombea ubunge mwaka huo. Alihama NCCR na kuhamia TLP ambako alimpindua Leo Lwekamwa na kumtimua Thomas Ngawaiya aliyemkuta hapo, na amegombea uraisi mara mbili kwa tiketi ya chama hiki.
- Ni mmoja wa wabunge waliokunywa 'Kikombe' cha Babu Ambilikile Mwasapile wa Loliondo
Mwenye vibwagizo zaidi aongezee
Nawasilisha
Nendeni mkajifunze kiswahili upya jamani lol, hamua=amua, hacha=acha, hogopa=ogopa.......mko wengi na mnakera sana.
Mrema =Jembe ,hana Tamaa