TANZIA Augustino Mrema, Mwenyekiti wa chama cha TLP afariki dunia

Mrema alikuwa mpigaji tu kama wapigaji wengine. Kapokea sana rushwa kutoka kwa makampuni aliyokuwa anayaita Kiraracha ili kuyahoji kwenye tuhuma za kukwepa kodi
 
Mrema alikuwa mpigaji tu kama wapigaji wengine. Kapokea sana rushwa kutoka kwa makampuni aliyokuwa anayaita Kiraracha ili kuyahoji kwenye tuhuma za kukwepa kodi
Kama alikuwa mpigaji Mbona hata nyumba ya kuishi pale sinza alinunuliwa na chama
 
Mwendo ameumaliza na ameitendea mema Nchi yake .ni baba wa demokrasia ya vyama vingi pamoja na mapungufu ambayo binadamu wote tunayo alijenga msingi kipindi kigumu kupita vyote.
RIP Agostino Lyatonga Mrema...mzee wa Kiraracha, mzee wa siku saba na mzee wa upigaji...

Pamoja na hayo naomba kukuuliza wewe makorere, hivi Mrema anakuwaje baba wa demokrasia?

Je unajua upepo wa mageuzi ulianza lini na wakati huo Lyatonga Mrema alikuwa wapi?

Je unajua madai ya demokrasia yalishika kasi lini na nyakati hizo Lyatonga Mrema alikuwa na msimamo gani?

Je unajua wana mageuzi walivyopambana kung'oa visiki miaka hiyo huku Lyatonga Mrema akivilinda vising'olewe?

Je unamjua aliyeendesha mapambano dhidi ya wana mageuzi na kuviongoza vyombo vya dola kutetea status quo?

Je unamjua aliyeapa kutoruhusu mfumo wa vyama vingi na kudai yeye si kichaa akiapa kulinda utawala wa kimla wa CCM?

Je unajua Lyatonga Mrema alijipa ukamanda wa vikosi vya FFU vilivyotumia silaha za moto, moshi na mbwa kuwatawanya wana mageuzi.

Je unajua kuwa hadi leo tupo ambao tulijeruhiwa na kuwa vilema tukidai demokrasia kupitia mkono wa kamanda Lyatonga Mrema?

Je unajua wakati mfumo wa vyama vingi unapitishwa rasmi mwaka 1992, Lyatonga Mrema alikuwa nani katika serikali ya CCM?

Pamoja na hayo...

Pumzika kwa amani Agostino Lyatonga Mrema, utakumbukwa kwa namna ulivyopambana kuzuia mfumo wa kidemokrasia lakini ukashindwa.

Utakumbukwa kwa namna wana mageuzi walivyokuwa wakihangaika juani kudai demokrasia ila wewe ukaja kula matunda yake kivulini.
 
Pumzika mzee wa kiraracha

Ila yule mjane vp hata ndoa haha enjoy wajameni
 
Na inaonekana hatutakuja kupata ukweli hasa ilikuaje mpaka msikiti wa mwembechai,pale Magomeni Dar warming kuuliwa pale wakiwa in a peaceful protest
 
R.I.P Lyatonga..tulipigwa bomu tukiwa na Lema Mwaka 2005 Pale Friends Corner Arusha Nikampa maji ya Kunawia Uso,Sijapost kitu kupitia ID hii nadhani toka 2017.Kwa heshima yake Nimejitokeza
 
Kumbe Kweli mrema alikuwa Ni Mtu wa Tiss( usalama wa Taifa) hakuwai kuwa mpinzani wa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…