Augustino Lyatonga Mrema ndiye aliyeasisi vuguvugu la mageuzi nchini kwenye ngazi za uchaguzi na ile 1995 wale mliokuwepo mnajuwa kabisa bila Nyerere kuingilia Kati Nccr Mageuzi ingekuwa Chama Tawala
Mrema amekuwa msema kweli asiyetawaliwa na tamaa
Mrema hakuwa mbinafsi ndio sababu alipowasapoti Kikwete na Maguful kwenye Uchaguzi hakuwalazimisha wanachama wa TLP kufuata Msimamo wake
Lyatonga atakumbwa kwa zile purukushani za 1995 na NCCR kama ilikuwa kweli na sio project CCM, alitikisa sana.
Mabucha ya nguruwe yalileta shida sana na kufikia hatua ya kusomewa itikafu misikitini na waislamu.
Naibu waziri mkuu wa kwanza na mwisho katika nchi hii kama sijakosea.
Waziri asiye na wizara maalum wa kwanza na mwisho katika nchi hii kama sijakosea.
Mwisho wa siku akaupiga mwingi dakika za mwisho na kufunga pingu za maisha, Mzee hakupenda uzinifu kama wengine, amekufa akiwa kwenye ndoa.
RIP mwamba Lyatonga, mwendo umeumaliza, Mungu akurehemu.
Nakumbuka mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi 1995, uwanja wa shule ya uhuru palivyofurika,
Hofu iliwajaa watawala hadi kuchakachua matokeo yaliyompa Ben ushindi,
Pumzika kwa amani meku Mrema
Pia walimfanyia kampeni chafu, walipandikiza mwanamke mmoja akadai amezaa na Mrema kisha akamtelekeza,
Akawa anashinda getini kwa Mrema masaki kwanye nyumba aliokuwa anakaa,
Kabla ya Mrema kufukuzwa na kuhamia Sinza,
CCM ni mabingwa wa siasa chafu na fitna,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametuma Salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mwanasiasa Mkongwe nchini Tanzania
"Nimesikitishwa na kifo cha Mwenyekiti wa chama cha TLP Bw. Agustino Lyatonga Mrema kilichotokea leo asubuhi Jijini Dar es Salaam. Nitamkumbuka kwa mchango wake katika mageuzi ya siasa, uzalendo na upendo kwa Watanzania. Pole kwa familia na wana TLP. Mungu amweke mahali pema.Amina"
==
==
Mwanasiasa Mkongwe nchini Tanzania, Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo Jumapili Agosti 21,2022 saa 12: 15.
Mrema alizaliwa Desemba 31, 1944, Vunjo mkoani Kilimanjaro na amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, mgombea Urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na amewahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.
Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki duninia leo Jumapili, Agosti 21, 2022, saa 12.15 asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Mrema aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alizaliwa Desemba 31, 1944, Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Msemaji wa MNH, Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo.
Enzi za uhai wake, mwanasiasa huyo aliwahi kuwa mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.
Ninaandika haya huku nikiwa natafakari kwa kina uelekeo wa Siasa za nchi yetu hasa kuelekea uchaguzi Mkuu wa Tanzania utakaofanyika mwezi Oktoba.Katika tafakuri yangu pia nimetazama yanayojiri katika siasa za Tanzania kipindi hiki na hili limenifanya niandike kidogo kumhusu Mheshimiwa Augustine...
HAKUNA mwanasiasa wa upinzani katika miaka ya karibuni aliyefikia umaarufu wa Augustine Lyatonga Mrema wakati alipohama kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwenda NCCR Mageuzi, Februari mwaka 1995. Mikutano yake na wananchi, mabomu ya machozi yaliyokuwa yakipigwa, khanga zilizokuwa...
Augustino Mrema ni mwanasiasa wa Tanzania aliyezaliwa tarehe 31 Desemba 1944 na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania. Alibadilisha uanachama wa chama Februari 1995 na kujiunga na NCCR-Mageuzi na baadaye akabadilika tena na kuwa Tanzania Labour Party (TLP) ambako aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama. Aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo mara kadhaa kabla ya kushindwa katika uchaguzi wa kitaifa na James Mbatia wa NCCR MAGEUZI mwaka 2015. Kisha akachaguliwa na Rais John Joseph Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Tanzania mwaka 2016.
Augustino Mrema ni wa pili kati ya ndugu watano na ni wa kabila la Wachaga wa Kijiji cha Kiraracha karibu na Mlima Kilimanjaro.
Augustino Mrema alisoma shule ya msingi na sekondari mjini Moshi mwaka 1955 hadi 1963, kisha akajiunga na Chuo cha Ualimu cha Mtakatifu Patrick ambako alimaliza elimu yake ya sekondari mwaka 1965. Augustino Mrema aliendelea kuandika mitihani ya Chuo Kikuu cha Cambridge O-level mwaka 1968 kisha akaendelea na masomo. kujiunga na Chuo cha Elimu ya Siasa Kivukoni. Baadaye alienda Marangu kuendeleza masomo yake.
Augustino Mrema Nafasi Serikalini
Augustino Mrema ameshika nyadhifa kadhaa katika Serikali ya Tanzania, Shirika la Usalama wa Taifa na chama cha CCM tangu mwaka 1966; nafasi 5 alizoshika ni pamoja na zifuatazo:
Mwalimu wa Uraia Vijijini 1974-1980
Mwalimu katika Chuo cha Usalama cha Taifa 1980-1982
Naibu Msaidizi wa Usalama wa Taifa katika Mkoa wa Dodoma 1982-1984
Naibu Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Dodoma 1983-1984
Naibu Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Shinyanga 1985-1987
Augustino Mrema Katika Kisiasa
Ingawa Augustino Mrema alikuwa akigombea urais nchini Tanzania tangu jimbo hilo lilipoanzisha demokrasia ya vyama vingi mwanzoni mwa miaka ya 1990, maisha yake ya kisiasa yalianza mwaka 1985 alipogombea ubunge katika jimbo alilozaliwa la Kilimanjaro. Ugombea wake ulizuiwa na Mahakama ya Juu, hata hivyo, baada ya mchakato mrefu wa kukata rufaa, alitangazwa rasmi kuwa mshindi mwaka wa 1987. Alifanikiwa kushika kiti chake mwaka 1990 bila ushindani mkubwa. Kuwa Mbunge kulimruhusu rais kumteua katika nyadhifa mbalimbali za Baraza la Mawaziri. Kuanzia 1990 hadi 1995 Mrema alishika nyadhifa mbalimbali za Baraza la Mawaziri na za juu serikalini:
Waziri wa Mambo ya Ndani 1990-1994
Waziri wa Kazi, Maendeleo na Michezo 1994-1995
Mwaka 1995 Augustino Mrema alihama CCM na kujiunga na Mkutano Mkuu wa Taifa wa Ujenzi na Mageuzi-Mageuzi ambacho kilikuwa chama kipya wakati huo. Katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, alisimama kama rais wa NCCR-Mageuzi ambayo ilikuwa ni muungano kati ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa Ujenzi na Chama cha Mageuzi-Mageuzi, alifanikiwa kupata asilimia 27.77 ya kura zote akishika nafasi ya tatu baada ya wakati huo aliyekuwa Rais Benjamin Mkapa aliyekuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Ibrahim Lipumba aliyesimama kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF).
Katika uchaguzi uliofuata alisimama kwa tiketi ya TLP na kupata asilimia 7.80 ya kura zote. Katika uchaguzi wa Desemba 14, 2005 alichaguliwa tena kuwa rais wa TLP na kumaliza wa nne na kupata 0.75% ya kura. Hayati Magufuli alimteua kushika wadhifa wa mwenyekiti wa bodi ya parole kuanzia 2016 hadi 2019.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.