TANZIA Augustino Mrema, Mwenyekiti wa chama cha TLP afariki dunia

TANZIA Augustino Mrema, Mwenyekiti wa chama cha TLP afariki dunia

Umeumaliza mwendo Mzee wa Kiraracha Augustino Lyatonga Mrema. Nenda Baba. Hakika Kwake Tutarejea. Pole Kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki na wengineo wote walioguswa na kuondoka kwake.
 
Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki duninia leo Jumapili, Agosti 21, 2022, saa 12.15 asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Mrema aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alizaliwa Desemba 31, 1944, Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Msemaji wa MNH, Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo.

Enzi za uhai wake, mwanasiasa huyo aliwahi kuwa mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.

giphy.gif
 
Mke wake WA Kwanza kumbe akifariki mwaka Jana...mwezi wa Tisa ...so wakati anajianda kuazimisha kifo cha mke wake Naye kafariki..hospital Ike Ile ya muhimbili
 
Jiwe kama kiongozi wa malaika ampokee rafiki yake salama
😂Yule anaweza Anza zile zake "nilikua nachomekea kidogo" katika Hotuba ya kumpokea mrema akajikuta anataja dhambi za mwenzie

Nasikia aliwahi kwenda msibani akajikuta ameropoka marehemu alikuwa na watoto wa nje😂
 
Lyatonga atakumbwa kwa zile purukushani za 1995 na NCCR kama ilikuwa kweli na sio project CCM, alitikisa sana.

Mabucha ya nguruwe yalileta shida sana na kufikia hatua ya kusomewa itikafu misikitini na waislamu.

Naibu waziri mkuu wa kwanza na mwisho katika nchi hii kama sijakosea.
Waziri asiye na wizara maalum wa kwanza na mwisho katika nchi hii kama sijakosea.

Mwisho wa siku akaupiga mwingi dakika za mwisho na kufunga pingu za maisha, Mzee hakupenda uzinifu kama wengine, amekufa akiwa kwenye ndoa.

RIP mwamba Lyatonga, mwendo umeumaliza, Mungu akurehemu.
 
Siasa za Tanzania baada ya Uhuru na kuelekea mfumo qa vyama vingi haiwezi kuelezewa kwa usahihi bila kutaja mchango wa kipekee alioutoa Augustino Lyatonga Mrema. Nimepokea kwa huzuni taarifa za kifo cha Mrema kwa masikitiko makubwa. Nawapa pole wafiwa wote ndugu, jamaa, na marafiki. Apumzike kwa Amani. Amina. JINA la Bwana Libarikiwe.
 
Back
Top Bottom