Aunganishiwa na Tanesco umeme bure na atatumia umeme bure baada ya kutoa eneo la kuweka Transfoma

Aunganishiwa na Tanesco umeme bure na atatumia umeme bure baada ya kutoa eneo la kuweka Transfoma

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Umeme.jpg

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Njombe limefanikiwa kuingiza umeme na kuuwasha bure katika nyumba ya Bibi Esteli Nyalusi mwenye umri wa miaka 62 ambaye ni mkazi wa kata ya Maguvani halmashauri ya mji wa Makambako ikiwa ni kutoa shukrani kwake baada ya kuruhusu bila vikwazo eneo lake kuwekwa transfoma ili umeme uwafikie wananchi wa eneo hilo kwa kuwa watu wengine walikataa huku yeye akiwa hana wazo lolote la kuingiza umeme kwenye nyumba yake.

Akizungumza mara baada ya kuwasha umeme kwenye nyumba hiyo meneja wa TANESCO mkoa wa Njombe Abdulrahman Nyenye amesema wameamua kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kumpatia bibi huyo umeme kwa kuwa aliweza kutoa eneo lake huku wananchi wengine wakikataa transfoma kuwekwa kwenye maeneo yao.

"Lakini bibi alijitolea kwamba naomba ikae hapa na hakuwa na ndoto za kuweza kupata umeme lakini na sisi tumeona ni vema kulipa fadhila kwa kumuwashia umeme ambapo tumesuka waya na malipo yote tumeshamlipia", amesema Mhandisi Nyenye.

Hanana Mfikwa ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako na diwani wa kata hiyo ya Maguvani ameishukuru TANESCO kwa kufikisha umeme kwenye nyumba hiyo ambapo sasa 99.9% kata hiyo imepata umeme huku asilimia moja ikiendelea kushughulikiwa.

"Katika eneo hili pia kulikuwa na changamoto ya uwekaji umeme ambapo zaidi ya transfoma nne ziliungua lakini mamam huyu kwa moyo wake safi akatoa eneo lake na hatimaye tangu mmeweka transfoma moja mpaka iko salama hivyo basi nitoe wito kwa wananchi wengine waone basi na wao ni sehemu ya maendeleo ya taifa hili", amesema Mfikwa.

Awali injinia Amina Ng'imba ambaye ni meneja wilaya TANESCO Makambako amesema bibi huyo amesaidia watu wa Maguvani kupata huduma ya umeme kwa kuweka transfoma katika eneo lake hivyo nao wameona umuhimu wa kumsaidia.

Kwa upande wake Bibi Esteli Nyalusi ameshukuru shirika la TANESCO pamoja na serikali ya awamu ya sita kwa kumfungia nishati ya umeme.

"Hili ni eneo langu na mwenzangu alishakufa kwa hiyo ninyi mliomba ndio maana niliwapatia kwa kweli nashukuru sana kwa wema wenu kwa kuwa sikutegemea kwamba nitapata umeme"amesema Estelia.

Licha ya kumfungia umeme lakini pia TANESCO wamefanikiwa kumnunulia jiko la umeme na mahitaji mengine ya nyumbani ikiwemo mchele na mafuta ya kupikia ili kurudisha kwa jamii katika kuadhimisha kilele cha wiki ya huduma kwa wateja.
 
Hii ni baada ya kutoa eneo lake ili Transfoma ya Tanesco iwekwe.

Wenye akili wakajiunganishe kwa huyo bibi.

Si kosa kisheria kuvuta umeme kutokea kwenye nyumba ya mtu.

Kitongoji au hata nchi nzima tungejiunganisha indirectly kutokea kwake ingependeza zaidi.
 
Awamu ya sita kaishukuru wapi hapo kwenye maneno aliyosema!!

Kila kitu mnaleta siasa ninyi watu aisee
 
Nimeingia haraka sana kwa huu uzi nikajua ni taratibu zao na mimi nikadai umeme wa bure.

Hapa watoto wamnunulie mama jiko la umeme atumie hadi achoke.
 
Wenye akili wakakiunganishe Kwa huyo bibi.

Si kosa kisheria kuvuta umeme kutokea kwenye nyumba ya mtu.

Kitongoji au hata nchi nzima tungejiunganisha indirectly kutokea kwake ingependeza zaidi.
Utauponza.
 
hongera kwake bibi kwa kuwa na moyo wa kujitolea sasa anafurahia malipo ya wema wake tujitahidi tuwe mfano wa kuigwa katika jamii
 
Wenye akili wakajiunganishe kwa huyo bibi.

Si kosa kisheria kuvuta umeme kutokea kwenye nyumba ya mtu.

Kitongoji au hata nchi nzima tungejiunganisha indirectly kutokea kwake ingependeza zaidi.
Daah wahuni sio watu
 
Nina uhakika wa 200% huyu mama Hana vitu vya Electronic hivyo atafaidi bulbs kuwasha usiku na kuzima.

Sasa basi kama Wana mapenzi ya dhati kurudisha shukran iliwapasa wamnunulie majiko ya umeme pasi Tv bufa na vitu vingine ikiwa pamoja na kumjengea nyumba Bora ya kisasa itakayo faidi huo umeme.

NB:Sijasoma Hadi mwisho.
 
Angewauzia eneo angepata fedha ndefu pengine angejiunganishia umeme na kununua hadi gari ....bahati ya Tanesco ni kuingia ubia na mbibi
 
Wenye akili wakajiunganishe kwa huyo bibi.

Si kosa kisheria kuvuta umeme kutokea kwenye nyumba ya mtu.

Kitongoji au hata nchi nzima tungejiunganisha indirectly kutokea kwake ingependeza zaidi.
Una uhakika?
 
Back
Top Bottom