Sasa hao ndio tunawaita wanafki.. Yaani kitu hukifahamu na unakizungumzia...
Ila huwa najiuliza mbona waliweza kututeka na maigizo yao ya kipindi kile.. Miaka ya tisini mwishoni..
Na kuna igizo moja waliigizia bagamoyo.. Uigizaji na uongizaji ulikuwa mzuri sana ingawa sikulifwatilia igizo lenyewe ila nilipenda lilivyopangiliwa.. Ila nilikuja fwatilia baadae nikagundua halikuongozwa na wabongo bali wageni...
Nimelisahau jina kidogo ila jamaa alikuwa kiwembe balaa ana afro... Hata sauti ilikuwa poa sana
Unamzungumzia Chuma, nalikumbuka lile igizo.
Issue kubwa kwenye hii industry ni kwamba wengi wanaoingia kwenye hiyo fani shule iliwashinda, ma-director walio kwenye hiyo fani pia shule siyo kiviile, kiasi kwamba ubunifu ni mdogo sana hivyo wanaishia kufanya copying, tena hata kile wanacho copy wanapunguza standard. Unakuta eti movie owner ndiye director, ndiye main editor, ndiye mtungaji, ndiye location manager etc etc na mtu huyo ndo Auntie Ezekiel au Madam Sepetu, kwa nini isiwe famba?
Marehemu Kanumba kama angeendelea kuwepo leo hii tungekuwa na industry ya movie iliyo katika viwango vya juu sana, jamaa alikuwa creative sana, hivyo hata wapinzani wake kina Ray (Vincent Kigosi) ilibidi wa-raise game yao kukimbizana na soko, vinginevyo angeuza Kanumba tu. Toka alivyoondoka hakuna tena ule ushindani na ubunifu kwenye hii tasnia.
Kanumba alikuwa pia anaweza kutrain watu wakaingia kwenye movie hata kama hawana vipaji wakafanya vizuri, watu kama hawa kina Auntie, Wema, Patcho, Jeniffer, Uwoya etc etc ni watu ambao jamaa aliwa-introduce na wakawa wanafanya vizuri.
Kwa sasa tunasubiria kama anakuja mwingine tena kuokoa hili jahazi, ubunifu.