Australia yakataa ofa ya China ya 'kuiunga mkono' kwenye ushuru wa Trump. Inaona kila moja afe kivyake.

Australia yakataa ofa ya China ya 'kuiunga mkono' kwenye ushuru wa Trump. Inaona kila moja afe kivyake.

Imeloa

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
17,999
Reaction score
21,560
Australia yakataa ofa ya China ya 'kuiunga mkono' kwenye ushuru wa Trump.

Australia imekataa haraka ombi la China la "kuungana mkono" dhidi ya ushuru wa Donald Trump, wakati Washington inazidisha vita vyake vya kibiashara na Beijing.

Ikulu ya Marekani hivi majuzi ilitoza ushuru wa kuagiza wa 10% kwa bidhaa za Australia, lakini kwa China - mshirika mkubwa wa kibiashara wa Australia - ilipandisha ushuru hadi 125%.

Balozi wa China nchini Australia Xiao Qian alisema upinzani wa pamoja ndio "njia pekee" ya kukomesha "tabia ya kijeuri na uonevu ya Marekani", akiomba ushirikiano wa Canberra katika maoni aliyotoa siku ya Alhamisi.

Waziri Mkuu Anthony Albanese, hata hivyo, alisema Waaustralia "watajisemea wenyewe", huku waziri wa ulinzi wa nchi hiyo akisema taifa hilo "halitashikamana mkono wa China katika swala hilo".


 
Australia wanajua urais wa Trump utapita na ujinga wa tariff ni wa muda tu.
 
Back
Top Bottom