Autoimmune disease

Autoimmune disease

Acha kula aina zote za wanga hasa ngano, nina hii hali ila mm inakuwa triggled na vyakula vyote vya ngano, but mimi huwa napata fatique nusu saa baada ya kutumia ngano so nliacha kuvila nipo sawa tu
Yah gluten ni hatari sana kwa mwili... Ni kitu ambacho ma practitioners wanatahadharisha sana watu.
Ina triger matatizo mengi sana
 
Mtu anaweza ishi na ugonjwa flan kwa mda mrefu kama tu haufanyi ukamdumaza. Doctors walikushauri nini?
Wamenishauri niendelee na immunoglobulin therapy + nizingatie diet, mazoezi pamoja na kupunguza stress
 
Tumia zaidi protini maharage, soya, samaki,
Achana na read meat replace na samaki ama mbogamboga, ukiwa na ham ya nyama ule kuku ila ondoa ngozi. Mm sikwenda hospital ila dadangu ninayemfuata naye anaumwa kakak zangu2 figo zishafeli, so najitibu kwa experience ya wengine
Najitahidi sana kuzingatia anti inflammatory diet but sometimes nashindwa najisahau naanza kula carbs.
Vp kuhusu tiba asili?! Una info zozote
 
Ni ugonjwa mbaya sana sababu mwili unakosa nguvu, akili inachanganyikiwa, mwili wote unauma yaan mm huwa nalala tu. Nlienda masomoni india nikiwa sijui naumwa nn. Ilibidi nipelekwe apollo hosptal cha kushangaza naambiwa siumwi kitu
Hata mm ilichukua muda mpaka kugundua nna huo ugonjwa. Nilikaa hospital kama miezi miwili hivi ndio baadae wakagundua hili tatizo
 
Habari za hapa. Mwaka jana nilipata tatizo la Autoimmune disease ambapo kinga za mwili zina over react na kushambulia mishipa midogo ya fahamu(nerves).
Kitaalam unaitwa Chronic inflammatory demyelinating polyneuropathy (CIDP).
Wakuu hii hali imenitesa sana almost mwaka mmoja sasa nashindwa kufanya shughuli za kawaida kwa sababu mikono na miguu haifanyi kazi vizuri kama hapo mwanzo.
Nilienda hospital kwa mtaalam wa magonjwa ya mishipa(neurology) akanianzishia dozi ya immunoglobulin mara moja kwa mwezi. Hii therapy imenisaida kidogo kunipa nafuu ila bado ile hali hali inanirudia sometimes.
Wakubwa naomba msaada wenu maana hali ni tete, huu ugonjwa umesababisha nipoteze kabisa furaha ya maisha.
Napata maumivu karibu kila siku.
Miguu inawaka moto, inakufa ganzi sometimes ngozi inawasha na kuchoma mwili mzima.

Naomba msaada wenu wakuu hali tete
Umewahi tumia vitamin b complex au neuroton? Kama bado take it
 
Mwingine anaongelea mambo ya gluten ambayo haihusiani na unachoumwa (yenyewe inasababisha celiac disease) ! Kiufupi humu ni upotoshaji mkubwa umejaa kwa watu wa sio Madaktari kuongelea magonjwa ilhali hawana hata a,b,c
 
Yaani unaacha kumsikiliza Neurologist wako anayekutibu unataka uwasikilize watu random wa humu ndani ! Are you serious? Nchi hii kweli ina wajinga wengi sana
Namsikiliza mtaalamu wangu na ndio maana naendelea na matibabu ya immunoglobulin.
Lakini pia nimekuja hapa Jukwaani kuomba ushauri, Au kama kuna mtu alishawahi kutibiwa kwa TIBA ya asili akapona kabisa anaweza kuwa msaada.
Pia hata maombezi ya watumishi wa Mungu yanaweza kunisaidia.
Kumbuka hii tiba nnayopata sasa hivi ni kwa ajili ya kumaintain hii hali na sio kwamba inaponyesha
 
Yah gluten ni hatari sana kwa mwili... Ni kitu ambacho ma practitioners wanatahadharisha sana watu.
Ina triger matatizo mengi sana
Gluten haina shida isipokuwa kwa wachache ambao ni allergic! Acha upotoshaji tena gluten allergic wengi ni wazungu sio sisi watu weusi
 
Gluten haina shida isipokuwa kwa wachache ambao ni allergic! Acha upotoshaji tena gluten allergic wengi ni wazungu sio sisi watu weusi
Mimi sio daktari ila mapractitioner wengi wanasema ni hatari sana.
haya mambo mimi sikuwa na habari nayo mpaka nilipoanza kuwa nafanya subtitling ya summit moja inafanyika nchini canada inaitwa Get well Summit, ina involve ma practitioners wengi wanazungumzia tiba mbadara za kansa, sijui ugumba, hashmotos, kureverse kisukari n.k. kwakuwa napewa video zao za summit kuzisubtitle najikuta in the process nasikiliza nakujua vitu vingi.
hivyo ndivyo nilikuja kufahamu uhatari wa gluten.
yes, sio kila mtu yuko sensitive na gluten, ila kwake yeye itakuwa vizuri akiacha kutumia chakula chenye gluten.
 
Namsikiliza mtaalamu wangu na ndio maana naendelea na matibabu ya immunoglobulin.
Lakini pia nimekuja hapa Jukwaani kuomba ushauri, Au kama kuna mtu alishawahi kutibiwa kwa TIBA ya asili akapona kabisa anaweza kuwa msaada.
Pia hata maombezi ya watumishi wa Mungu yanaweza kunisaidia.
Kumbuka hii tiba nnayopata sasa hivi ni kwa ajili ya kumaintain hii hali na sio kwamba inaponyesha
Kwa akili yako unafikir kuna mganga wa kienyeji au mitishamba anaujua ugonjwa unaitwa chronic inflammatory demyelinating polyneuropathy mpaka ajue dawa ya kuutibu? Au huyo mganga anatibu ugonjwa ambao haujui wala hajawahi hata kuusikia?
 
Back
Top Bottom