Avalon cinema

Avalon cinema

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
AVALON%2BCINEMA.jpg

Avalon Cinema

Siku moja nilimtembelea Balozi Abbas Sykes nyumbani kwake Sea -View. Kwangu mimi saa moja au mbili za mazungumzo na Balozi Sykes huwa zinanirudisha nyuma sana katika maisha yangu ya utoto, Balozi siku nyingine akinihadithia yale yaliyopita wakati mimi bado mdogo akitaja majina ya watu ambao wengi wao wameshatangulia mbele ya haki lakini ninawafahamu.

Siku hiyo niliona video cassette kwenye meza yake na nilipoangalia nikaona ni – ‘’High Society.’’

Hii ilikuwa filamu maarufu katika miaka ya 1950 ambayo ndani walicheza wanamuziki nyota wa nyakati zile – Louis Armstrong, Bing Crosby, Frank Sinatra na wengineo. Niliingalia sana ‘’cover’’ ya ile video cassette. Wakati ule ni zile cassette za VHS madude makubwa ya mikanda.

Bwana Abbas kumbe na yeye alikuwa akiniangalia jinsi nilivyochukuliwa na video ile. Sauti yake ndiyo iliyonitoa katika fikra zangu wakati nilipokuwa nimehama dunia hii ghafla nimerudi kwenye dunia ambayo hakuna ajiuaye ila mimi.

‘’Mohamed mimi na baba yako tulitembea kutoka Kipata hadi Avalon Cinema kuangalia filamu hiyo.’’

Balozi Sykes alikuwa kanitoa nilikokua.

Bing Crosby jina hili nililisikia kwa mara ya kwanza mwaka wa 1964 asubuhi siku ya Eid Pili nikinywa chai na baba yangu. Jana yake ilikua Eid Mosi baada ya Mfungo wa Ramadhani na nilikwenda kuona filamu ya Elvis Presley, ‘’Blue Hawaii, Empire Cinema.

Siku ya Eid ilikuwa siku kubwa sana kwetu watoto kwani tulinunuliwa nguo mpya na kupewa fedha kwenda Mnazi Mmoja kusheherekea. Sisi wengine ambao tulijiona, ‘’sophisticated,’’ tulipita njia tu pale Mnazi Mmoja. Tuliliogopa vumbi la pale Sisi starehe yetu ilikuwa kwenye kuangalia senema na kwena kula ''fish and chips,'' baada ya kutoka.senema.

Siku ile Empire Cinema walikuwa wanaonyesha filamu ya Elvis Presley ‘’Blue Hawaii.’’

Hii ilikuwa filamu yangu ya kwanza ya Elvis. Nilimpenda sana Elvis na akawa ‘’hero,’’ wangu katika udogo wangu wote. Hakuna nyimbo yake ambayo nilikuwa siwezi kuimba na nilikuwa na maktaba yangu ndogo nyumbani ya rekodi zake.

Fedha niliyokuwa nikipewa kwa ajili ya shule zilikwenda kwenye vitabu, comics na rekodi za Elvis na nyingine nilitumia Snow Cream Parlour ambayo bado ipo hadi leo na haikuwa mbali na Avalon Cinema.

Miaka ile haikunipitika hata kwa mbali kuwa hili duka la Ice Cream iko siku atalinunua rafiki yangu marehemu Yusuph Zialor na litakuwa mali yetu.

Wakati nikinywa chai nikawa namuhadithia baba filamu niliyoona jana na sifa kem kem za Elvis.

Baba alipozungumza akanambia kuwa wao walipokuwa vijana wakimpenda Bing Crosby.

Sasa pale nilipokuwa naangalia ile ‘’cover,’’ ya High Society nilikuwa nimerudi kote huko nilikoeleza hapo juu na ni kwa hakika ni nyuma sana wakati ule nikiwa mtoto mdogo wa miaka 12.

Nilimkumbuka baba yangu ambae alikuwa keshatangulia mbele ya haki na nikaikumbuka maktaba yake ya muziki ambayo kwa mara ya kwanza nilisikiliza ‘’trumpet,’’ ya Louis Armstrong na yeye mwenyewe akiimba kwa sauti yake nene na kavu na nikakumbuka pia habari za Bing Crosby.

Nilikuwa New York na nikamwambia mwenyeji wangu Abdillah Rijal anipeleke kwenye Louis Armstrong Museum ambayo niliona inatangazwa katika ‘’brochure,’’ bahati mbaya sikupata muda wa kufika kule.

Kumbukumbu yangu ya Avalon Cinema ina mengi. Sikumbuki jina la filamu lakini nakumbuka kumuona Loius Armstrong katika filamu moja hapo Avalon Cinema. Filamu hii ilikuwa ndani yake na wanamuziki wengi na nakumbuka walikuwapo Herman’s Hermits.

Leo hapa ninapoandika inanijia picha ya Dar es Salaam ilivyokuwa katika miaka ya 1960 na nasikia nyimbo za nyakati zile kama ‘’Something Good’’ ya Herman’s Hermits, ‘’Hello Dolly,'' ya Louis Armstrong…

Ilikuwa Avalon Cinema nilipoangalia moja ya filamu zangu nizipendazo sana – Lawrence of Arabia (Peter O’ Toole, Omar Shariff na Anthony Quinn), The Sound of Music (Julie Andrews), Kissin’ Cousins (Elvis Presley), Concert for Bangladesh (George Harrison na Ravi Shankar) The Godfather (Marlon Brando) kuzitaja chache.

Miaka imepita na Dar es Salaam imebadilika sana.

Jengo la Avalon bado lipo lakini sasa si jumba la senema tena. Historia ya Avalon Cinema itabaki katika kumbukumbu yangu ikinikumbusha siku za utoto wangu.
 
Simulizi nzuri wengine habari za avalon,empress na empire tunahadithiwa sana na wazee wetu watoto wa mjini
 
Sheikh naomba uniwekee hizo comics za zamani
Una madini yamelala hapo
Story nzuri sana imenikumbusha maisha ya 70s
 
Asante kwa simulizi babu yetu

Qiugley,
Siku zimekwenda.

Mimi huyo hapo chini mwaka wa 1966 nikiwa na umri wa miaka 14.

Hii picha nimepiga Mnazi Mmoja jioni wenzangu Everton FC baadae
Saigon 1967 walikuwa wanafanya mazoezi lakini siku hiyo mimi
nnilikuwa na mipango mingine sikuja mazoezini.

Nyuma yangu ni Soko la Kisutu na hiyo barabara unayoona nyuma
yangu ndiyo leo Titi Street.

ktP0EF1381GGGlxE8kUYu3_rCVTb1A4gLXBq5cr5UJFLYBW-IL8MXPK5EVdBjJP2q1WFTqdlm650dmvNiWKME8SdArotnddx8RSGi9RRpG8thKujMX14LaE_70-HFnkrYtetqwMkkspxgxRb8AhqHp0rYYTvTbrs1vi7j-rHIruSDxiWckK12Ufvzi1LP5EKj4iVqVz4zcQOJT5QxAjwxTdKx_ywYs1mI9R7fRR0So_nb4nGiPeSjbjUGwnU8YDwu6R0K_HB3a_ge4PJo-dCqwR22hB7Z6RtmZaiENOublHNsnFDee-lrzmKvSOP_IN9VZIZ04FfbY3rrYwUd9Y8_xqncpLgf2H4j7EtECLOHhILx3AiKhBPVnYl1zaeUottljAnJRAJpBg8gR00owxv3F9p0qtMBJo9wwUwWBvnAU7cRpU4BuNEbSW7c_oSOd6D3SwoMl-GEefmEwMx5peH6dMleW8lvzyV6miNgCU15fXgArWoSrvj1qFJkpNiHamebxrr-nLZ8sjwo5SfAz5KHekG0zd9RKsXEbhRjSuNNwQyzuWpr50dQTP67HP9GSRjHxoQWLWJimRSioqkwvXp-JPWhPxl7uHc8kwuPzPM=w670-h526-no
 
bro mo'd miaka ile nipo dar tech nikipewa posho ya mwezi jioni avalon.
 
Dah! Umenikumbusha mbali sana. Movie yangu ya kwanza hapo Avalon ilikuwa "Love in Goa" na tulipata tickets kwa kulnguliwa maana foleni ilikuwa kubwa na zingeisha. Hii inanikumbusha marehem dada yangu(RIP baby!) alikuwa anafanya kazi Ugawaji (Dar es salaam Distributors Co.) Enzi hizo wakilangua sana sukari na unga wa ngano mahotelini na alikuwa na kisu sana in just her 20s.

Tukimaliza movie Avalon tulikuwa tunapata Ice cream au Cassata pembeni chini, siyo Snow-cream. Uzuri wa ile restaurant chini Avalon kuna kioo mbele na kuna view nzuri ya bandari ya meli za Abiria hasa Mapinduzi na Maendeleo.

Mzee Mohamed Said inaonyesha ume-bse sana Kariakoo na Mnazi mmoja. Je, unaweza kutupa habari za City Center hasahasa maeneo ya Posta? Nadhani maeneo haya yamebeba Culture kubwa sana ya mji wa Dar hasa migahawa ya nje ya pale New Africa Hotel na Salamander. Ni watu wa aina gani Enzi za sixties walikuwa wakivinjari mitaa hiyo?
 
Qiugley,
Siku zimekwenda.

Mimi huyo hapo chini mwaka wa 1966 nikiwa na umri wa miaka 14.

Hii picha nimepiga Mnazi Mmoja jioni wenzangu Everton FC baadae
Saigon 1967 walikuwa wanafanya mazoezi lakini siku hiyo mimi
nnilikuwa na mipango mingine sikuja mazoezini.

Nyuma yangu ni Soko la Kisutu na hiyo barabara unayoona nyuma
yangu ndiyo leo Titi Street.

ktP0EF1381GGGlxE8kUYu3_rCVTb1A4gLXBq5cr5UJFLYBW-IL8MXPK5EVdBjJP2q1WFTqdlm650dmvNiWKME8SdArotnddx8RSGi9RRpG8thKujMX14LaE_70-HFnkrYtetqwMkkspxgxRb8AhqHp0rYYTvTbrs1vi7j-rHIruSDxiWckK12Ufvzi1LP5EKj4iVqVz4zcQOJT5QxAjwxTdKx_ywYs1mI9R7fRR0So_nb4nGiPeSjbjUGwnU8YDwu6R0K_HB3a_ge4PJo-dCqwR22hB7Z6RtmZaiENOublHNsnFDee-lrzmKvSOP_IN9VZIZ04FfbY3rrYwUd9Y8_xqncpLgf2H4j7EtECLOHhILx3AiKhBPVnYl1zaeUottljAnJRAJpBg8gR00owxv3F9p0qtMBJo9wwUwWBvnAU7cRpU4BuNEbSW7c_oSOd6D3SwoMl-GEefmEwMx5peH6dMleW8lvzyV6miNgCU15fXgArWoSrvj1qFJkpNiHamebxrr-nLZ8sjwo5SfAz5KHekG0zd9RKsXEbhRjSuNNwQyzuWpr50dQTP67HP9GSRjHxoQWLWJimRSioqkwvXp-JPWhPxl7uHc8kwuPzPM=w670-h526-no
Kwa hiyo shekh na wewe ulicheza sana mpira enzi hizo?
 
Aiseee,kweli kitambo sana,miaka zaidi ya 50,ukiangalia sasa palivyo hapo soko la Kisutu karibu na Msikiti wa Mwinyi kheri kama sikosei,ambapo ni hatua chache tu kutoka Starlight Hotel na Pea cock,opposite na Super Market Mpya ya jengo la iliyokua Jengo kuu kuu la Bakwata,basi yatosha tu kusema mambo hubadilika sana. Ukiitazama hiyo picha Mzee Mohamed Said, ni kama ya Kijijini kabisa,lakini kumbe ni Dar,tena City Centre kabisa. Unapozungumzia Barabara ya Bibi Titi,ni moja ya barabara za mijini kabisa,lakini ukiiangalia picha hiyo,hutakaa uamini. Kwako Mzee M Said, lazima ikupe fikra na kukupa hisia kali sana ukikumbuka enzi za ujana wako. Its very long time.
Ukipata picha za zamani za Jangwani barabara ya Morogoro tuwekee,pia Kariakoo.Je mitaa ya Temeke,Kinondoni na Ilala ilikuaje enzi hizo?
 
Qiugley,
Siku zimekwenda.

Mimi huyo hapo chini mwaka wa 1966 nikiwa na umri wa miaka 14.

Hii picha nimepiga Mnazi Mmoja jioni wenzangu Everton FC baadae
Saigon 1967 walikuwa wanafanya mazoezi lakini siku hiyo mimi
nnilikuwa na mipango mingine sikuja mazoezini.

Nyuma yangu ni Soko la Kisutu na hiyo barabara unayoona nyuma
yangu ndiyo leo Titi Street.

ktP0EF1381GGGlxE8kUYu3_rCVTb1A4gLXBq5cr5UJFLYBW-IL8MXPK5EVdBjJP2q1WFTqdlm650dmvNiWKME8SdArotnddx8RSGi9RRpG8thKujMX14LaE_70-HFnkrYtetqwMkkspxgxRb8AhqHp0rYYTvTbrs1vi7j-rHIruSDxiWckK12Ufvzi1LP5EKj4iVqVz4zcQOJT5QxAjwxTdKx_ywYs1mI9R7fRR0So_nb4nGiPeSjbjUGwnU8YDwu6R0K_HB3a_ge4PJo-dCqwR22hB7Z6RtmZaiENOublHNsnFDee-lrzmKvSOP_IN9VZIZ04FfbY3rrYwUd9Y8_xqncpLgf2H4j7EtECLOHhILx3AiKhBPVnYl1zaeUottljAnJRAJpBg8gR00owxv3F9p0qtMBJo9wwUwWBvnAU7cRpU4BuNEbSW7c_oSOd6D3SwoMl-GEefmEwMx5peH6dMleW8lvzyV6miNgCU15fXgArWoSrvj1qFJkpNiHamebxrr-nLZ8sjwo5SfAz5KHekG0zd9RKsXEbhRjSuNNwQyzuWpr50dQTP67HP9GSRjHxoQWLWJimRSioqkwvXp-JPWhPxl7uHc8kwuPzPM=w670-h526-no
Shukrani mzee wangu, kumbe umri bado, ni rika la akina Kikwete
 
..Avalon Cinema ilikuwa mali ya baba yake Al-Noor Kassum. Nadhani baadae jengo hilo lilitaifishwa na serekali.
 
Back
Top Bottom