Avalon cinema

Avalon cinema

..Avalon Cinema ilikuwa mali ya baba yake Al-Noor Kassum. Nadhani baadae jengo hilo lilitaifishwa na serekali.
JokaKuu,
Baba yake Al Noor Kassum kweli ndiyo alikuwa mmiliki wa Avalon Cinema na akajenga na Amana Cinema Ilala kwa ajili ya Waafrika.

Huyu Mzee Kassum ndiye alikuwa Muki wa jamii ya Ismailia Tanganyika.

Mwanae, Al Noor Kassum ndiye aliyemtetea Ally Sykes 1955 kwenye kesi aliyobambikiwa na Waingereza Moshi kumshikisha adabu kwa kuunda TANU.

Waingereza walimtumia Joseph Kimalando.

Ngoja niingie Maktaba nitakuwekea movie nzima In Shaa Allah.

Kuna kisa kingine very interesting cha Mercedes Benz ya Aga Khan ambayo Ismailia waliamua kuiuza baada ya kumnunulia Aga Khan Benz nyingine.

Iliamuliwa kuwa hii Benz asiuziwe Ismailia yeyote bali iuzwe kwa mtu mtu maarufu na mwenye hadhi yake katika Waafrika wa Tanganyika.

Benz hii alinunua Abdulwahid Sykes na alikaanayo hadi alipofariki 1968.
Mercedes Benz 280S yenye usajili DSQ 666.
 
AVALON%2BCINEMA.jpg


Avalon Cinema

Siku moja nilimtembelea Balozi Abbas Sykes nyumbani kwake Sea -View. Kwangu mimi saa moja au mbili za mazungumzo na Balozi Sykes huwa zinanirudisha nyuma sana katika maisha yangu ya utoto, Balozi siku nyingine akinihadithia yale yaliyopita wakati mimi bado mdogo akitaja majina ya watu ambao wengi wao wameshatangulia mbele ya haki lakini ninawafahamu.

Siku hiyo niliona video cassette kwenye meza yake na nilipoangalia nikaona ni – ‘’High Society.’’

Hii ilikuwa filamu maarufu katika miaka ya 1950 ambayo ndani walicheza wanamuziki nyota wa nyakati zile – Louis Armstrong, Bing Crosby, Frank Sinatra na wengineo. Niliingalia sana ‘’cover’’ ya ile video cassette. Wakati ule ni zile cassette za VHS madude makubwa ya mikanda.

Bwana Abbas kumbe na yeye alikuwa akiniangalia jinsi nilivyochukuliwa na video ile. Sauti yake ndiyo iliyonitoa katika fikra zangu wakati nilipokuwa nimehama dunia hii ghafla nimerudi kwenye dunia ambayo hakuna ajiuaye ila mimi.

‘’Mohamed mimi na baba yako tulitembea kutoka Kipata hadi Avalon Cinema kuangalia filamu hiyo.’’

Balozi Sykes alikuwa kanitoa nilikokua.

Bing Crosby jina hili nililisikia kwa mara ya kwanza mwaka wa 1964 asubuhi siku ya Eid Pili nikinywa chai na baba yangu. Jana yake ilikua Eid Mosi baada ya Mfungo wa Ramadhani na nilikwenda kuona filamu ya Elvis Presley, ‘’Blue Hawaii, Empire Cinema.

Siku ya Eid ilikuwa siku kubwa sana kwetu watoto kwani tulinunuliwa nguo mpya na kupewa fedha kwenda Mnazi Mmoja kusheherekea. Sisi wengine ambao tulijiona, ‘’sophisticated,’’ tulipita njia tu pale Mnazi Mmoja. Tuliliogopa vumbi la pale Sisi starehe yetu ilikuwa kwenye kuangalia senema na kwena kula ''fish and chips,'' baada ya kutoka.senema.

Siku ile Empire Cinema walikuwa wanaonyesha filamu ya Elvis Presley ‘’Blue Hawaii.’’

Hii ilikuwa filamu yangu ya kwanza ya Elvis. Nilimpenda sana Elvis na akawa ‘’hero,’’ wangu katika udogo wangu wote. Hakuna nyimbo yake ambayo nilikuwa siwezi kuimba na nilikuwa na maktaba yangu ndogo nyumbani ya rekodi zake.

Fedha niliyokuwa nikipewa kwa ajili ya shule zilikwenda kwenye vitabu, comics na rekodi za Elvis na nyingine nilitumia Snow Cream Parlour ambayo bado ipo hadi leo na haikuwa mbali na Avalon Cinema.

Miaka ile haikunipitika hata kwa mbali kuwa hili duka la Ice Cream iko siku atalinunua rafiki yangu marehemu Yusuph Zialor na litakuwa mali yetu.

Wakati nikinywa chai nikawa namuhadithia baba filamu niliyoona jana na sifa kem kem za Elvis.

Baba alipozungumza akanambia kuwa wao walipokuwa vijana wakimpenda Bing Crosby.

Sasa pale nilipokuwa naangalia ile ‘’cover,’’ ya High Society nilikuwa nimerudi kote huko nilikoeleza hapo juu na ni kwa hakika ni nyuma sana wakati ule nikiwa mtoto mdogo wa miaka 12.

Nilimkumbuka baba yangu ambae alikuwa keshatangulia mbele ya haki na nikaikumbuka maktaba yake ya muziki ambayo kwa mara ya kwanza nilisikiliza ‘’trumpet,’’ ya Louis Armstrong na yeye mwenyewe akiimba kwa sauti yake nene na kavu na nikakumbuka pia habari za Bing Crosby.

Nilikuwa New York na nikamwambia mwenyeji wangu Abdillah Rijal anipeleke kwenye Louis Armstrong Museum ambayo niliona inatangazwa katika ‘’brochure,’’ bahati mbaya sikupata muda wa kufika kule.

Kumbukumbu yangu ya Avalon Cinema ina mengi. Sikumbuki jina la filamu lakini nakumbuka kumuona Loius Armstrong katika filamu moja hapo Avalon Cinema. Filamu hii ilikuwa ndani yake na wanamuziki wengi na nakumbuka walikuwapo Herman’s Hermits.

Leo hapa ninapoandika inanijia picha ya Dar es Salaam ilivyokuwa katika miaka ya 1960 na nasikia nyimbo za nyakati zile kama ‘’Something Good’’ ya Herman’s Hermits, ‘’Hello Dolly,'' ya Louis Armstrong…

Ilikuwa Avalon Cinema nilipoangalia moja ya filamu zangu nizipendazo sana – Lawrence of Arabia (Peter O’ Toole, Omar Shariff na Anthony Quinn), The Sound of Music (Julie Andrews), Kissin’ Cousins (Elvis Presley), Concert for Bangladesh (George Harrison na Ravi Shankar) The Godfather (Marlon Brando) kuzitaja chache.

Miaka imepita na Dar es Salaam imebadilika sana.

Jengo la Avalon bado lipo lakini sasa si jumba la senema tena. Historia ya Avalon Cinema itabaki katika kumbukumbu yangu ikinikumbusha siku za utoto wangu.
sasa hizo nyimbo na filamu zinamchango gani kwa 'allah'?
badala uende ukaimbe kaswida wewe unaenda kutazama makafiri?hicho ndicho ulichokuwa unafundishwa madrasa??
 
JokaKuu,
Baba yake Al Noor Kassum kweli ndiyo alikuwa mmiliki wa Avalon Cinema na akajenga na Amana Cinema Ilala kwa ajili ya Waafrika.

Huyu Mzee Kassum ndiye alikuwa Muki wa jamii ya Ismailia Tanganyika.

Mwanae, Al Noor Kassum ndiye aliyemtetea Ally Sykes 1955 kwenye kesi aliyobambikiwa na Waingereza Moshi kumshikisha adabu kwa kuunda TANU.

Waingereza walimtumia Joseph Kimalando.

Ngoja niingie Maktaba nitakuwekea movie nzima In Shaa Allah.

Kuna kisa kingine very interesting cha Mercedes Benz ya Aga Khan ambayo Ismailia waliamua kuiuza baada ya kumnunulia Aga Khan Benz nyingine.

Iliamuliwa kuwa hii Benz asiuziwe Ismailia yeyote bali iuzwe kwa mtu mtu maarufu na mwenye hadhi yake katika Waafrika wa Tanganyika.

Benz hii alinunua Abdulwahid Sykes na alikaanayo hadi alipofariki 1968.

Joseph Kimalando alikuwa ni nani?
 
Louis Armstrong museum ipo pale Queens, New York
Nilipata bahati ya kufanya ziara fupi na nilijifunza mengi sana
 
Louis Armstrong museum ipo pale Queens, New York
Nilipata bahati ya kufanya ziara fupi na nilijifunza mengi sana
Sherrif,
Nasikitika sikufika lakini jana Prof. Google kanichukua katika tour u tube.

Nyimbo yangu ya kwanza kuisikia ya Armstrong ni ''Skokian,'' ilikuwa katika
Maktaba ya marehemu baba tena ni yale madisc makubwa 78 RPM kwa
bahati mbaya ikikuponyoka umeivunja.

Hivi sasa nyimbo ninayoipenda ya Satchmo ni ''My One and Only Love.''
 

JokaKuu,
Nilikuahidi kisa cha Joseph Kimalando.

‘’…I was able to convince Hamza Aziz and Iddi Mwajasho to attend the Machame meeting in which Nyerere spoke. Hamza Aziz and Mwajasho were young police officers stationed at the Police Training College. After this meeting the two were reprimanded by the government for getting involved in politics contrary to service regulations. In organising the Machame meeting I had earned for myself the wrath of the colonial administration.

Soon after this meeting I was arrested for allegedly taking bribes. One day a white officer and an African Inspector walked into my office and arrested me. There was no evidence to back the allegations. I was suspended and taken to court for on trumped up corruption charges. One of the people who was used by the government to frame me was Joseph Kimalando, one of the TANU founding members from Northern Province. I had crossed swords with Kimalando when we were transforming TAA into TANU at the headquarters. I had backed Yusuf Olotu and other patriots and advised them to side-line him and register the new party. Kimalando although wasAlthough among the founders of TANU in Dar es Salaam, once back in Moshi he Kimalando refused to register the party in Kilimanjaro.

Reports reaching TANU headquarters were that Kimalando was collaborating with the colonial government to frustrate registration of the party. He was ousted from the party and he joined UTP.

upload_2018-3-18_23-55-59.png

Sheikh Hussein Juma Vice President United
Tanganyika Party (UTP)


Kimalando was a seasoned politician having been in politics since the early days of the African Association. Kimalando He claimed to be among the founder members of the Association together with Sheikh Hussein Juma who was later to be Vice President of the United Tanganyika Party, UTP, an opposition party formed by the British to oppose TANU. When I was transferred to Moshi from Korogwe in 1957 Kimalando, then outside the main stream of the struggle and a member of the UTP, framed me against the government.

upload_2018-3-18_23-52-47.png

Bi Mruguru bint Mussa

My mother, Bi. Mruguru bint Mussa and my brother Abdulwahid contacted Al Noor Kassum recently returned from studies in Britain where he had studied law to defend me. Our parents had known each other in Dar es Salaam for many years. My father in his early business carrier career had tried to join the Chamber of Commerce, which was dominated by Indians at that time. My father could not fit in that all Indian organisation and left to form his own African Traders Association, which was short-lived. It is during that period at the Chamber of Commerce that he came to be acquainted to Al Noor Kassums’s father.

Al Noor Kassum flew to Moshi by a Dakota plane of the East African Airways from Dar es Salaam and appeared in court the following day. The two policemen who had arrested me did not appear in court but the magistrate asked the prosecutor to proceed with the case. Kassum objected to that and insisted that the two police officers who had made the arrest must appear as witnesses. For some unknown reasons the prosecution was not very keen to have the two policemen interrogated by my defense council and the magistrate had no choice but to dismiss the case. By then I had been suspended from work for six months. I was given four months leave from work and I used this opportunity to go to Accra to attend Ghana’s independence celebrations in 1957.''

(''Under The Shadow of British Colonialism: The Life of Ally Sykes,'' by Ally Sykes and Mohamed Said). Unpublished.
 
Aiseee,kweli kitambo sana,miaka zaidi ya 50,ukiangalia sasa palivyo hapo soko la Kisutu karibu na Msikiti wa Mwinyi kheri kama sikosei,ambapo ni hatua chache tu kutoka Starlight Hotel na Pea cock,opposite na Super Market Mpya ya jengo la iliyokua Jengo kuu kuu la Bakwata,basi yatosha tu kusema mambo hubadilika sana. Ukiitazama hiyo picha Mzee Mohamed Said, ni kama ya Kijijini kabisa,lakini kumbe ni Dar,tena City Centre kabisa. Unapozungumzia Barabara ya Bibi Titi,ni moja ya barabara za mijini kabisa,lakini ukiiangalia picha hiyo,hutakaa uamini. Kwako Mzee M Said, lazima ikupe fikra na kukupa hisia kali sana ukikumbuka enzi za ujana wako. Its very long time.
Ukipata picha za zamani za Jangwani barabara ya Morogoro tuwekee,pia Kariakoo.Je mitaa ya Temeke,Kinondoni na Ilala ilikuaje enzi hizo?
Halafu MTU anatokea anasema ccm haijafanya chochote kwa miaka50
 
Halafu MTU anatokea anasema ccm haijafanya chochote kwa miaka50
Mmmmh,mambo yenu ya siasa mi simo kabisa. Halafu mambo mengine hutokea by default tu kwa sababu naamini hata kama siyo CCM,bado kwa kuwa watu wapo,mambo yangefanyika tu,ili mradi tunaishi,tungejiwekea utaratibu na bado tungesonga. Mimi kipekee naamini katika Utaifa kuliko hayo mambo yenu ya Siasa.
 
Qiugley,
Siku zimekwenda.

Mimi huyo hapo chini mwaka wa 1966 nikiwa na umri wa miaka 14.

Hii picha nimepiga Mnazi Mmoja jioni wenzangu Everton FC baadae
Saigon 1967 walikuwa wanafanya mazoezi lakini siku hiyo mimi
nnilikuwa na mipango mingine sikuja mazoezini.

Nyuma yangu ni Soko la Kisutu na hiyo barabara unayoona nyuma
yangu ndiyo leo Titi Street.

ktP0EF1381GGGlxE8kUYu3_rCVTb1A4gLXBq5cr5UJFLYBW-IL8MXPK5EVdBjJP2q1WFTqdlm650dmvNiWKME8SdArotnddx8RSGi9RRpG8thKujMX14LaE_70-HFnkrYtetqwMkkspxgxRb8AhqHp0rYYTvTbrs1vi7j-rHIruSDxiWckK12Ufvzi1LP5EKj4iVqVz4zcQOJT5QxAjwxTdKx_ywYs1mI9R7fRR0So_nb4nGiPeSjbjUGwnU8YDwu6R0K_HB3a_ge4PJo-dCqwR22hB7Z6RtmZaiENOublHNsnFDee-lrzmKvSOP_IN9VZIZ04FfbY3rrYwUd9Y8_xqncpLgf2H4j7EtECLOHhILx3AiKhBPVnYl1zaeUottljAnJRAJpBg8gR00owxv3F9p0qtMBJo9wwUwWBvnAU7cRpU4BuNEbSW7c_oSOd6D3SwoMl-GEefmEwMx5peH6dMleW8lvzyV6miNgCU15fXgArWoSrvj1qFJkpNiHamebxrr-nLZ8sjwo5SfAz5KHekG0zd9RKsXEbhRjSuNNwQyzuWpr50dQTP67HP9GSRjHxoQWLWJimRSioqkwvXp-JPWhPxl7uHc8kwuPzPM=w670-h526-no

Mheshimiwa,

Mbona nyuma yako kunaonekana kama vile kuna nyumba na siyo soko, tena nyumba iliyozungukwa na miti pembeni.
 
Dah! Umenikumbusha mbali sana. Movie yangu ya kwanza hapo Avalon ilikuwa "Love in Goa" na tulipata tickets kwa kulnguliwa maana foleni ilikuwa kubwa na zingeisha. Hii inanikumbusha marehem dada yangu(RIP baby!) alikuwa anafanya kazi Ugawaji (Dar es salaam Distributors Co.) Enzi hizo wakilangua sana sukari na unga wa ngano mahotelini na alikuwa na kisu sana in just her 20s.

Tukimaliza movie Avalon tulikuwa tunapata Ice cream au Cassata pembeni chini, siyo Snow-cream. Uzuri wa ile restaurant chini Avalon kuna kioo mbele na kuna view nzuri ya bandari ya meli za Abiria hasa Mapinduzi na Maendeleo.

Mzee Mohamed Said inaonyesha ume-bse sana Kariakoo na Mnazi mmoja. Je, unaweza kutupa habari za City Center hasahasa maeneo ya Posta? Nadhani maeneo haya yamebeba Culture kubwa sana ya mji wa Dar hasa migahawa ya nje ya pale New Africa Hotel na Salamander. Ni watu wa aina gani Enzi za sixties walikuwa wakivinjari mitaa hiyo?

Umenikumbusha Mithun akiimba love in Goooooah....Ooooh oooooooh.
 
Umenikumbusha Mithun akiimba love in Goooooah....Ooooh oooooooh.
Subir...
Dunia yangu yote ilikuwa kwanza Mtaa wa Kipata...
Dunia yangu ilikuwa unazunguka hapo na kama vile naiona katika 1950s.

Nilipopata makamo nikawa sasa nakuja mjini tukiita Uzunguni tukipita
Uhindini.

Huko tukipita njia tu na ndiyo maana sina kumbukumbu unazotaka kusoma.
 
Back
Top Bottom