Aviator yampotezea Dismas Tsh Milioni 57 za kwenda kusoma Scholarship Uingereza

Sasa anaomba msaada wa kumwezesha kuendelea na masomo yake kama jinsi alivyopanga hapo awali.

Angekua huku kwetu afu akawa Chawa hilo mbona jambo dogo sana kwa Mama, ila huko kwao bora ajiue tu.
 
Neno "Kamari" linamaanisha michezo ya kubahatisha au kamari, ambayo ni pamoja na kubeti, kucheza bahati nasibu, na aina nyingine za michezo inayohusisha kushinda au kupoteza mali kwa bahati nasibu.

Katika Qur'an, kamari imeharamishwa kwa sababu ya madhara yake kwa mtu binafsi na jamii. Allah anasema katika Surat Al-Ma'idah (5:90-91):

"Enyi mlioamini! Hakika ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani; basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.
Shetani anataka tu kutia baina yenu uadui na bughudha kwa sababu ya ulevi na kamari, na kukuzuilieni dhikri ya Mwenyezi Mungu na swala. Basi je, mtaacha?" (Qur'an 5:90-91)

Madhara ya kamari yanayotajwa katika Qur'an na Sunnah ni pamoja na:

1. Kusababisha uadui na chuki – Kamari inaweza kuleta ugomvi na chuki kati ya watu, hasa wakati mtu anapopoteza mali yake kwa bahati mbaya.


2. Kuzuia kumtaja Mwenyezi Mungu na kuswali – Inampotosha mtu na kumfanya asahau wajibu wake wa kidini.


3. Kupoteza mali na kuharibu maisha – Mtu anaweza kupoteza pesa zake kwa bahati mbaya na kuishia katika umaskini na madeni.


4. Kukuza uvivu na tamaa ya kupata mali bila kufanya kazi halali – Inawafanya watu kuamini katika njia za haraka za kupata utajiri bila bidii.
 
Nusu kivipi? Mbona kila kitu kiko hapo? Huyo jamaa aliishia kujiua. Extreme addiction. Anakopa pesa, anauza vitu ili tu akarushe kindege. Mwisho maji yakamfika shingoni akaona isiwe kesi....
Sad 😔
 
Sasa anaomba msaada wa kumwezesha kuendelea na masomo yake kama jinsi alivyopanga hapo awali.

Angekua huku kwetu afu akawa Chawa hilo mbona jambo dogo sana kwa Mama, ila huko kwao bora ajiue tu.
Angekwenda tena kucheza
 
Hapa ndio unaanza kumuelewa John Heche na kuwatukana wapuuzi kama Makalla, hao aliowatag wamchangie tu kijana akasome, maana wameweka sera mbaya kiasi kwamba mikampuni ya kamari inajaa tu
Kwani amelazimishwa? Mbona wengine hatuchezi?
 
Huyo dogo hata akipewa msaada anaweza kurudia tena huo upuuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…