Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Raia mmoja Mkenya amepoteza zaidi ya KSh2.8 milioni sawa Tsh Milioni 57 kwenye jukwaa la kamari la Aviator, pesa ambazo zilikusudiwa kufadhili masomo yake nchini Uingereza.
Dismas Mutai, ambaye alikuwa amejiandikisha katika Chuo Kikuu cha Anglia Ruskin huko **London Uingereza**kwa kozi ya mwaka mmoja ya Usimamizi wa Miradi ya Kimataifa, sasa ameachwa bila makazi, bila senti yoyote, na bila matumaini.
"Nimenaswa na mtego. Mtego mbaya ambao sikuwahi kuutarajia maishani mwangu. Msongo wa mawazo unanipeleka kaburini polepole. Aviator iliruka na zaidi ya KSh2.8 milioni pesa za watu," Dismas alisema katika chapisho moja la mtandao wa kijamii.
Sasa anaomba msaada wa kumwezesha kuendelea na masomo yake kama jinsi alivyopanga hapo awali.
**"Tafadhali usiniache nife nikiwa mdogo kama nilivyo. Nina udhaifu kama binadamu mwingine yeyote. Pengine Uingereza haikukusudiwa mimi bali ilinipa tu nafasi ya kuishi ili niwe ushuhuda hai kwa wengi," Dismas anasema.
Katika chapisho lake, amewatag watu mbalimbali hususani viongozi wa umma akiwemo aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko, Mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi, Seneta wa Nandi Samson Cherargei, na Gavana wa Nandi Stephen Sang, miongoni mwa maafisa wengine wa serikali kutoka Kaunti ya Nandi akiomba msaada.