Matajiri wengi ni MAFISADI wakubwa mno.
Chukulia mfano Yusuph Manji, anakopa bilioni 10 toka NSSF ananunua na kurabati quality plaza na na Ubungo Godowns, miezi mitatu baadae anawauzi NSSF Ubungo Godowns kwa bilioni 50 then anawauzia PSPF ile Quality Plaza kwa karibia 40 bilioni, jumla ni takriban bilioni 90
Halafu anabaki Kama mpangaji pale Quality bila kulipa mpaka deni linafikia bilioni 13!!!
Au angalia ule Mradi wa dege eco village, mtu kakopa NSSF anenda kununua ekari 300 Kisha anarudi kuuwauzia haohao NSSF kwa Bei ya milioni 800 kwa eka moja Kama hisa kwenye mradi na anakuwa main shareholder..
Manji huyu kachota Dola milioni 29 kupitia kashfa ya kagoda, karibu bilioni 27 za kibongo.
Manji huyu ndio kachukua viwanja vya waislamu na kuuwauzia hao security funds..
Bado Kuna issue ile ya Coco Beach
Kifupi huwezi kuwa na matajiri wanaopata utajiti wao kwa njia za kina Manji..
Ni kuaibika
Ni kudharaulika
Ni kujitukanisha
Ni kashfa
Washughulikiwe