Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Ndejembi ameyasema hayo mkoani Iringa alipokagua maendeleo ya awamu ya pili ya mradi huo inayohusisha ujenzi wa jengo la abiria na maegesho ya magari, akieleza kuwa uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kukuza uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania.
Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wa uwanja huo, iliyohusisha barabara ya kuruka na kutua ndege (runway), barabara za maingilio ya ndege (taxiways) na jengo la huduma za umeme (powerhouse), imekamilika kwa asilimia 100 kwa gharama ya Shilingi bilioni 68.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta, amesema ujenzi wa jengo la abiria na maegesho ya magari umefikia asilimia 49 na unagharimu Shilingi bilioni 41.