Awamu ya Magufuli: Changamoto sugu zimebaki historia, kila pembe ya nchi inashangilia mafanikio yake

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
3,250
Reaction score
5,509
Mzee Mwinyi aliwahi kusema “haya yanayofanywa na JPM hatukuweza kufanya kwa miaka 30”. Ni kauli ya moyoni mwake na hakika ni kauli isiyoweza kubezwa na yeyote kwa sababu zifuatazo: ya kwanza, Mzee Mwinyi aliwahi kuwa Rais, kauli hiyo ameitoa baada ya kuupima urais wake na huu wa JPM na kuona kwamba ndani ya miaka michache JPM kafanya makubwa sana. Ya pili, mzee mwinyi kakaa serikalini muda mrefu na ana uzoefu wa kutosha wa kulinganisha na kutofautisha utendaji. ya tatu, kwa umri aliofikia mzee Mwinyi hana cha kupoteza maishani cha kusema aseme kitu ili apate kitu, chochote anachosema ni kweli tupu ya moyo wake. Unadhani ni kwanini mzee Mwinyi alisema hayo?

Kila mtu ana jibu lake juu ya kauli ya Mzee Mwinyi. katika kutafakari hilo nimeona mzee mwinyi aliyasema hayo baada ya kuangalia changamoto na utatuaji wake wakati wa miaka 30 kabla ya JPM na wakati wa JPM. Awamu ya JPM changamoto sugu za mtanzania zimebaki historia na kwa muono uleule wa mzee Mwinyi ni katika awamu hii changamoto nyingi sana zimetatuliwa tena kwa muda mfupi sana. Tunapoizungumzia awamu ya tano tunazungumzia awamu ambayo tatizo la maji, elimu, umeme, usafiri( nchi kavu na majini), afya na mengine mengi yamebaki historia katika uso wa Tanzania.

Takwimu zinaonesha kuwa upatikanaji wa huduma za maji, umeme, afya na elimu umeboreshwa na kuongezeka marudufu katika awamu hii ya tano na pia kuna unafuu wa hali ya juu wa utolewaji wa huduma hizo katika awamu hii ya tano ya JPM. Kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma hizi ndiko kulikomsukuma Rais wa awamu ya pili Mzee Mwinyi kukiri kuwa hawakuweza kuyafanya haya kwa miaka 30 iliyopita. Tunayoyasema mafanikio haya tunaitwa ‘praise team’, Je mzee Mwinyi naye ni ‘praise team’?

Watanzania wanaona yanayofanyika katika awamu hii ni ya kustaajabisha na kushangaza sana. Mengi mzauri ya kupendeza yamefanyika kwa muda mfupi, nikianza kuyataja naweza kumaliza siku nikiyataja lakini hayo machache yanaonesha ni namna gani serikali hii inavyowajali watu wake hasa linapokuja suala la kuboresha huduma za kijamii ambazo ni muhimu sana. Tunaimani na matumizi ya kodi zetu kwa kuwa yanayofanyika yanaoneka.

Mzee Mwinyi ni sauti ya wengi wenye kufurahia mafanikio haya makubwa ya serikali ya JPM. Kaskazini, magharibi, kusini na mashariki na kila pembe ya nchi hii inashehekea mafanikio haya na sababu za kusheherekea zipo mbili: ya kwanza, tunasheherekea haya kwa sababu zilikuwa ni changamoto sugu ambazo zilikuwa zinaturudisha nyuma na ya pili, tunasheherekea haya kwa kuamini mengine mengi yanakuja na tunafanya hivi kumtia moyo Rais wetu afanye mengine mengi.
 
Praise Team or whatever they call you people, it's right!

Because, your sycophantic behavior has gone supererogatory to the extent that your right thinking has gone astray.
 
Ume generalise sana maoni yako. Kuna sehemu katika nchi hii hali bado. Kweli kuna machache lakini bado kabisa. Mfano ni mkoa wa Kigoma. Huu mkoa awamu zote haikuangaliwa kabisa. Kwa mfano miundo mbinu ya barabara na reli zilizidi kufa. Awamu ya tano hii mpaka sasa mkoa haujaunganishwa na mikoa jirani kwa barabara za lami. Hali kadhalika umeme bado wa ma generator yaliyohamishwa kutoka mikoa mingine. Kweli plan za kujenga barabara hizo za lami na kuunganishwa na umeme wa grid zipo. Lakini sasa cha ajabu ni kwamba hazitekelezwi. Ahadi ni za miaka mingi zingine tangu awamu ya tatu. Na pale mkandarasi anapo tangazwa na kuanza kazi cha ajabu utekelezaji unaenda kwa kusuasua saaana. Mfano barabara ya lami Kigoma to Kasulu yenye km 90 tu imeshachukua siyo chini ya miaka 6 na haijaisha. Kuna barabara ya kutoka Nyakanazi mpaka Kasulu nayo haijaisha. Hivi karibuni ikatangazwa kuwa benki ya Afrika imetoa mkopo ijengwe barabara kutoka Burundi kupitia Kasulu mpaka Kakonko. Dalili zaonyesha nayo inafuata mtindo uleule. Hakuna hata dalili ya kuanzwa. Sasa hivi serikali imeona ni vyema zaidi kujenga SGR kuilekeza Rwanda wakati hata Mjerumani alitathmini akaona aipeleke reli Kigoma kwanza ili kuunganisha na nchi ya Congo ambayo ni uchumi mkubwa sana, maana ni route ya moja kwa moja. Meli nyingi tu zimejengwa ziwa Victoria lakini ziwa Tanganyika hata meli moja hakuna tena. Eti inazungumziwa kufufua Liemba yenye umri wa zaidi ya miaka 100?!!!!. Yaani wananchi wa Kigoma wanajiuliza maswali mengi sana.
 
Back
Top Bottom