Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,720
- 6,957
Kwa jicho la tatu nauona utawala wa Samia Suluhu Hassan (SSH) ukienda kufanana ama kushahabiana na utawala wa awamu ya pili wa Mzee Ruksa. Samia Suluhu Hassan ni Mzanzibari na Mzee Mwinyi pia alikuwa Mzanzibari. Hata kimuonekano tu na jinsi wanavyoongea, wote hawa wawili wana haiba fulani hivi ya "upole".
Hii itakuwa neema kubwa sana kwa "wafanyabiashara" hasa ikitokana na ukweli kwamba kipindi cha marehemu JPM, biashara nyingi "zilikufa" ama "kudumaa". Hii inafanana na kipindi cha Mwalimu Nyerere, mliokuwepo wakati ule, kuanzia mwaka 80 mpaka 85 biashara nyingi zilikufa Sana, lakini alipoingia Mzanzibari, Mzee Ruksa, biashara zilishamiri kama uyoga wakati wa masika.
Kwa mtazamo wangu hali hii inaenda kujirudia tena! Kipindi cha "Ruksa" part two, kinajirudia tena! History has a tendency of repeating itself. Historia huwa inajirudia, na Mama Samia atalithibitisha hilo.
Wafanyabiashara, kaeni mkao wa kula, kipindi cha mavuno kinakuja. Tena naona hata yale maduka yakubadilishia fedha za kigeni yakiruhusiwa upya. Kitendo cha kufunga yale maduka (Bureau De Change) kilikuwa ni kitendo cha "dhuluma" na ukandamizaji. Sioni kama Mama Samia Suhusu Hassan atakuwa ni mwenye "dhuluma" kama mtangulizi wake alivyokuwa.
Tena kutokana na uswahiba uliopo kati ya Mama SSH na Jakaya Kikwete, hakika naiona Tanzania iliyojaa furaha na tabasamu. Sasa "pesa" itakuwa mifukoni mwetu.
Farewell Magufuli, till we meet again