Awamu ya Mama Samia Suluhu Hassan itakuwa kama ya Mzee Ruksa

Awamu ya Mama Samia Suluhu Hassan itakuwa kama ya Mzee Ruksa

Kwa jicho la tatu nauona utawala wa Samia Suluhu Hassan (SSH) ukienda kufanana ama kushahabiana na utawala wa awamu ya pili wa Mzee Ruksa. Samia Suluhu Hassan ni Mzanzibari na Mzee Mwinyi pia alikuwa Mzanzibari. Hata kimuonekano tu na jinsi wanavyoongea, wote hawa wawili wana haiba fulani hivi ya "upole".

Hii itakuwa neema kubwa sana kwa "wafanyabiashara" hasa ikitokana na ukweli kwamba kipindi cha marehemu JPM, biashara nyingi "zilikufa" ama "kudumaa". Hii inafanana na kipindi cha Mwalimu Nyerere, mliokuwepo wakati ule, kuanzia mwaka 80 mpaka 85 biashara nyingi zilikufa Sana, lakini alipoingia Mzanzibari, Mzee Ruksa, biashara zilishamiri kama uyoga wakati wa masika.

Kwa mtazamo wangu hali hii inaenda kujirudia tena! Kipindi cha "Ruksa" part two, kinajirudia tena! History has a tendency of repeating itself. Historia huwa inajirudia, na Mama Samia atalithibitisha hilo.

Wafanyabiashara, kaeni mkao wa kula, kipindi cha mavuno kinakuja. Tena naona hata yale maduka yakubadilishia fedha za kigeni yakiruhusiwa upya. Kitendo cha kufunga yale maduka (Bureau De Change) kilikuwa ni kitendo cha "dhuluma" na ukandamizaji. Sioni kama Mama Samia Suhusu Hassan atakuwa ni mwenye "dhuluma" kama mtangulizi wake alivyokuwa.

Tena kutokana na uswahiba uliopo kati ya Mama SSH na Jakaya Kikwete, hakika naiona Tanzania iliyojaa furaha na tabasamu. Sasa "pesa" itakuwa mifukoni mwetu.

Farewell Magufuli, till we meet again

AMINAA
 
Nenda zako huko - Watanzania gani wenye akili timamu wanataka kurudi kwenye zama za laissez faire - nani?

Kuwaruhusu wafanya biashara kuteka nyara Uchumi wetu na kutamba is tantamount to Commiting HARA KIRI, ungeangalia watanzania waliokuwa wanasindikiza mwili wa Mzalendo JPM ukawasikiliza walikuwa wanasema nini katika maombolezo kuhusu Uongozi wa JPM, wala usinge kuwa na ubavu wa ku-comments mambo ya kushangaza sana.

Narudia kukumbusha tena kwamba Tanzania haiwezi kukubari kurudi tena kwenye utawala wa everyman for him/herself God for us all. Magufuli ameacha ame-set humane standards kwa mstakabali wa Taifa letu Watanzania hawatakuwa tayari kurudishwa tena kwenye zama za man eat man jungle, kuruhusu mafisadi na majangiri kutamba na kuwafanya Watanzania wanyonge wajione si lolote si chochote kwenye Taifa lao huru.
 
Nimeisikiliza hotuba ya Mama Samia Suruhu kama mara nne, na nimepata hofu kuu.

Kwa kifupi hotuba ya mama ni kama inatoa framework ya kuturudisha kwenye zama za Rais Ali Hassan Mwinyi, zama zilizotawaliwa na ruhusa kufanya chochote kiwezekanacho.

Kwa mfano, ni kama vile alikuwa anatoa maelekezo kwa wizara ya maliasili kuachilia wawekezaji wavamie mbuga za wanyama na kuanza kuchimba madini.

Lakini pia, nimemsikia akifungulia milango ya utayari wake wa kupindisha pindisha sheria za kodi ili tu kukaribisha wawekezaji huku akikataza kuwabuguzi na kugusia kwamba yeye binafsi ameisha anza fanya nao vikao.

Nimemsikia mama samia akisema hataki kuona maongezeko ya kodi, anategemea kuona makusanyo yakishuka miezi hii miwili mitatu. na tena kaelekeza apelekewe cheque asign Tax Refund. Yaani TRA waache kuchukua kodi, waanze kulipa kodi.

Tena nimemuangalia machoni, poor Samia, nimeona machoni mwake amejawa na matumaini makubwa sana kwamba wafanyabishara wanapenda na wako tayari kulipa kodi kama sheria iwatakavyo kama ambavyo walikuwa wakifanya huko nyuma.

Kwa kurudia rudia, jana, Rais wetu ameitangazia Dunia kwamba Tanzania HAINA SKILLED LABOR, na HIVYO WAWEKEZAJI WOTE WAJE NA SKILLED LABOR WAO na ameishaagiza wasibuguziwe.

Watanzania tuwe makini na huyu mama.
 
Mmefeli na mpango wenu.
 
Hela mtaani hazikuonekana kwa sababu zifuatazo...
Kwa hiyo ili pesa iingie kwenye mzunguko hadi ufisadi uwepo? pumbavu kama hili Bora dingi yake angeota ndoto ya unyevu akalibamiza kwenye taulo
 
Back
Top Bottom